Mzee uttoh yuko sahihi kabisa, mashirika yote ya ndege huwa hayaleti faida ya moja kwa moja kwa taifa. Biashara ya ndege kama yenyewe huwa haiingizi faida, ila faida zake huja kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo safari hizo za ndege hufanikisha ndani ya nchi husika.
Mfano mzuri shirika kubwa kama la Fly-Emirates au Air-China hayapati faida za moja kwa moja, lakini shughuli za kiuchumi ambazo haya mashirika yamezifanyikisha ndizo huingiza faida. Fly-Emirates linafanikisha shughuli za kiutalii na biashara ya kimataifa ndani ya ile falme ya Kiarabu.
Faida ambazo zinapatikana kutoka kwenye utalii na biashara ya kimataifa ndiyo hutumika kufidia (Compensate) gharama ya uendeshaji wa shirika la Fly-Emirates. Biashara ya ndege ina gharama kubwa sana kuendesha, na mashirika yanayoingiza faida kama Ethiopian Airlines hayaingizi kutokana na safari za anga bali kazi nyingine (Kufundisha marubani na wahudumu, pamoja na kufanya marekebisho ya ndege) ambazo shirika hufanya.
Ambacho sisi hatukukubaliana na Raisi Magufuli ni ile tabia ya kusema unanunua ndege kwa pesa taslimu kuinua UTALII nchini, ilhali umeweka sera mbovu ambazo zinawakimbiza watalii: Hata mpango-mkakati wa biashara (Business Plan) hajatupa wananchi. Kila jambo linafanyikia gizani tu....
Lingine ni hili la kununua ndege kwa pesa taslimu bila kuweka wazi mikataba yake linatia ukakasi sana. Halafu shirika bado liko kwenye majaribio ya kufufuliwa na halijasimama vizuri: Tungejaribu kwanza kuchukua ndege chache chini ya Lease (Dry or Wet Leases ) huku tukipima upepo unaendaje.....