CAG mstaafu Uttoh: Hakuna Shirika lolote la ndege duniani lililopata faida baada tu ya kuanzishwa, ATCL haijawahi kulipa Gawio Serikalini

CAG mstaafu Uttoh: Hakuna Shirika lolote la ndege duniani lililopata faida baada tu ya kuanzishwa, ATCL haijawahi kulipa Gawio Serikalini

Kuna Mbunge yupo huku anasema hiviii
D449524A-B0AB-4286-A514-B91418EBA6BE.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Usitake kuchanganya alichosema Utooh kisheria na ule utapeli aliokuwa anaufanya Jiwe. Alichokuwa anakifanya jiwe ni kuhadaa umma kuwa ATCL inapata faida. Mwaka jana mwezi Desemba kwa masikio yangu nilimsikia akiuongopea umma kuwa ATCL imeingiza faida ya 28b. Huku mitandaoni kwenye watu waelewa wala usijitokeze kumtetea yule muhuni, maana utajiabisha bure.
Unatafuta ushindi au?

Basi mimi nimekupa kombe, kashereheke!
 
Nataka nikujuze pia mashirika yote ya ndege duniani yanaendeshwa na ruzuka zitokazo serikalini mwao Fuatilia
Ndugu yangu acha kamba.
Mashirika ya ndege duniani mengi ni mashirika ya kibiashara, huwezi kusema unafanya biashara huku unaendeshwa ruzuku. Ruzuku unapewa ili utoe huduma na sio biashara.
 
Kwa hiyo tutegemee faida baada ya miaka 100? Watanzania tulimuonya dikteta kwamba ununuzi wa ndege si kipaumbele cha Watanzania na biashara ni hasara tupu kama ASINGEKURUPUKA hiyo zaidi ya 3 trillions si ingeweza kutumia kuongeza mishahara ya Wafanyakazi nchini!?
Hakuna faida kwenye ndege, faida yake ni kuchochea uchumi tu

Kama ndege sio kipaumbele cha taifa chadema wasingeweka kwenye ilani 2015
 
Hebu acheni kuandika uongo kwenye mambo ambayo hamna ufahamu nayo, ni bora upite kimya kimya. Hawa wanapataje faida kwa zaidi ya miaka 30 continuously!?
Hakuna faida kwenye ndege, faida yake ni kuchochea uchumi tu
 
Ilikua nidhamu ya woga kiukweli jamaa alikua na dhamira ya dhati ila kuna watu waliogopa kumwambia ukweli narudia tena waliogopa kumwambia ukweli ila alikua na malengo sahihi na hii nchi
Siyo kwakua hawakuwa na jipya na yeye alitaka innovation siyo statusquo?

Ila kiukweli walimwogopa wengi...Mie sikupata nafasi ya kukutana naye, nilipanga kukutana naye March kumbe ndiyo anaaga...RIEP!

Nilipanga kuongea kweli ya dhati ya moyo wangu na kwahakika ningemwambia apunguze ukali kidogo kwakua watu wengi walishamwelewa. Kilichobaki ni kujenga mifumo ambayo ingeibua watu wenye merits kiurahisi badala ya yeye kuhangaika kuwatafuta ambapo si rahisi kuwaibua bila plan nzuri...kuna watu ambao walikuwa wanatumia jina lake vibaya, wengi saa hizi wanamgeuka na wengine wamekaa kimya kama vile hawakuwepo...Hawa ndiyo ambao Mama Samia anatakiwa kuwa nao makini sana...Hii recycling ya watu as if ni wao tu ndiyo wapo katika nchi hii siyo nzuri...

Wapo watu wazuri ambao mifumo ikiwekwa vizuri wata compete kwa merits siyo kwakua namfahamu fulani jina langu litaenda...Hao wabovu wengi wao wamejipenyeza na kushika nafasi za juu kisha wapo busy kusuka mitandao ya wao kuendelea kubaki madarakani huku wakikwamisha wale wenye merits kwakuwanyima fursa...Tabia ambazo hazina faida kwao wala kwa nchi...
 
Tatizo lako ndugu yangu ni pingapinga tu! Hata viongozi wako wanakiri tatizo si kununua ndege au kufufua ATCL bali namna manunuzi yalivyofanyika! Siasa zetu zimejaa kelele kuliko kujua watu wanasimamia principles zipi [emoji855]

..hata chadema wanaounga mkono ununuzi wa ndege wamekosea.

..na wanachadema wanaounga mkono wanafanya hivyo kwa kutishika na propaganda za wana-ccm, but deep down they know the govt made a mistake kujiingiza ktk biashara ya hasara.
 
Wanaopenda kusikia wanachokipenda kukisikia hata kama siyo fact watapinga hili
La gawio, lilitamkwa hivyo kwamba wanatoa gawio kwa serikali... Sasa hapa simuelewi kabisaa...

 
La gawio, lilitamkwa hivyo kwamba wanatoa gawio kwa serikali... Sasa hapa simuelewi kabisaa...

Gawiwo lipo kisheria kwa mashirika ya umma na halitokani na faida...
 
Mkuu haikuwa nidhamu ya woga tuwe wakweli dikteta na dhalimu alikuwa HAAMBILIKI kwa kujiona ana Phd na kudhani anajua kila kitu under the sun wakati alikuwa hajui lolote lile zaidi ya ubabaishaji na uongo wa kupindukia.
1618607403114.jpeg

Ilikua nidhamu ya woga kiukweli jamaa alikua na dhamira ya dhati ila kuna watu waliogopa kumwambia ukweli narudia tena waliogopa kumwambia ukweli ila alikua na malengo sahihi na hii nchi
 
Fly emirates halipati faida? Emirates imekuwa ikipata profit mpaka 2019/2020 due to Covid-19 impact before that it has been making big profit.
Ndiyo ndugu yangu, Fly-Emirates haipati faida ya moja kwa moja kutokana na safari za anga pekee. Shirika lao la Emirates linamiliki mashirika mengine madogo-madogo (subsidiaries) yanayohusika na biashara nyingine kama Adventures and Tour-Guiding, Aircraft-Maintenance, Flight-Training, Catering etc. Hivyo wanafanya biashara kubwa na hawategemei safari za anga tu kama ATCL.

Lakini pia wenzetu wanapokea ruzuku kutoka serikalini kwao hasahasa za mafuta na pia hawalipi kodi za ndani. Hili linawafanya wao wawe mbele zaidi kuliko mashirika mengine ya usafirishaji.....
 
Kwa hiyo lile gawio ilikuwa hadaa. Asante Uttoh kwa kueleza ukweli huu wa hadaa za awamu ya tano
 
Kuna jamaa juzi tunapiga soga akaniuliza: "hivi SMU katika hizi shughuli za mazishi ya JPM mbona walikuwa hawaoneshi nyumba ya JPM?"
Ni hekalu kama yale mahekalu ya Mugabe?
 
CPA Uttoh amesema kimsingi mashirika ya umma hayapaswi kulipa dividend kwa sababu hayafanyi biashara na ametoa mfano UDSM wanalipa dividend serikalini kwa biashara gani wanayofanya?!
Hapa mwamba kachemka kidogo
Tanapa ni shirika la umma
Tanesco ni shirika la umma
Dawasa ni shirika la umma
Yote hayo yanafanya biashara
 
Hapa mwamba kachemka kidogo
Tanapa ni shirika la umma
Tanesco ni shirika la umma
Dawasa ni shirika la umma
Yote hayo yanafanya biashara
Hayajawahi toa dividend, yametoa gawiwo ambalo lipo kisheria ila sheria hii ilikuwa haitekelezwi Hayati aliitekeleza...
 
Back
Top Bottom