Nakubaliana kabisa na CAG na hapa tatizo sio kukosa pesa Bali poor planning inayofanywa na wakuu wa taasisi za Barabara ambao ni TanRoads na TARURA.
Kwa sababu haiwezekani Kila mwaka wanakuja na miradi mipya wakati miradi ya zamani imekwama.Hili ni tatizo la wanaohusika na mipango.
Binafsi Huwa najiuliza Kwa nini kusiwe na utekelezaji wa miradi michache Kila mwaka ambayo mnajua kabisa ndani ya miaka 2 itamalizika Kwa pesa hizi hizi zilizopo badala ya kuanzisha vipisi vipisi vya miradi Kila sehemu ya Nchi matokeo yake hakuna kinachomalizika.
Mfano inawezekanaje Barabara ya km 200 ukasaanzisha ujenzi Kwa kilomita 2 Kila mwaka? Hizi ni akili za wapi? Kule Rukwa TanRoads walisaini mkataba wa Ujenzi wa Barabara 2 tofauti za km 25 Kila Moja na zote zimekwama wakati Barabara mojawapo hapo Ina km 50 na nyingine km 200 Sasa Kwa nini wasisaini upande mmja Ili imalizike ndio waje wahamie kwingineko?
Sasa hiki ndicho kinafanyika Nchi nzima wakati ukikusanya hivyo vipande vidogo vidogo ukachagua Barabara chache unaweza zikamilisha vizuri kabisa.
Kuna tatizo kubwa sana la project and transport planning plus Wanasiasa kuingilia.
Tukiendelea na utaratibu huu wa kutapanya Rasilimali bila Mpango hakuna Cha maana tuta achieve kama Nchi.
=============
Mipango dhaifu ya maendeleo ya barabara pamoja na upungufu sugu wa fedha vinaendelea kuchelewesha upanuzi wa miundombinu nchini Tanzania, hali inayoongeza madeni na kuhatarisha utoaji wa huduma, kwa mujibu wa ukaguzi mpya ulioonyesha kuwa ni nusu tu ya maboresho ya barabara yaliyopangwa yametekelezwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Licha ya kuongezeka kwa mahitaji ya miundombinu ya barabara nchini kote, serikali katika miaka minne ya fedha mfululizo imefanikiwa kutekeleza wastani wa asilimia 50 tu ya maboresho ya barabara yaliyopangwa kati ya mwaka wa fedha 2021/22 na 2024/25. Upungufu huu, kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), unaathiri ufanisi wa usafiri, unachelewesha shughuli za kiuchumi na kuongeza malimbikizo ya madeni kwa wakandarasi.
Hayo yameelezwa katika ripoti ya ukaguzi ya mwaka 2024/25 ya CAG, Charles Kichere, iliyochambua upangaji na utekelezaji wa programu za miundombinu ya barabara na kubaini kuwepo kwa udhaifu wa kimfumo katika upangaji wa bajeti, upangaji wa vipaumbele pamoja na utoaji wa fedha kwa taasisi husika.
Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (PO-RALG) pamoja na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), ambazo zinahusika na usimamizi wa sehemu kubwa ya mtandao wa barabara, zimekuwa zikifanya kazi katika mazingira ya bajeti zisizotosheleza na utolewaji wa fedha usio wa uhakika, jambo linalosababisha kushindwa kufikia malengo ya kila mwaka mara kwa mara.
My Take
Hongera CAG Kwa kuliona hili labda Watabadilika.
View attachment 3573337