CAG Prof. Assad astaafu, Charles Kichere ateuliwa kuwa CAG mpya

Mkuu hapo subir report ijayo itakavo kuwa safi hapo ndo utajua kuna tofauti kat ya msiba na matanga
Kwa hiyo wewe ulitakaje..embu tupe mawazo yako tukujue unayowaza..ndio baadae utupe tofauti kati ya msiba wako na matanga
 
Charles Kichere kama CAG sasa

- Mwaka wa Fedha 2018/2019 alikuwa Kamishna Mkuu wa TRA
- 2019/2020 alikuwa RAS wa Njombe

Je, atajikagua na kujipa hati safi/chafu na kufuatilia majibu ya maswali yaliyopita kuhusu TRA na Njombe?
Hala kuna tatizo.

1. Wenye uzoefu wamo serikalini.
2. Ukiteua wenye uzoefu walio serikalini, unaweza kuwekewa maswali kuhusu wao kufunika walikopita.

Suluhisho hapo ni kuteua yeyote anayefaa, na kama kuna tuhuma tujenge utamaduni na mfumo wa uwazi kiasi kwamba mtu yeyote anaweza kuwa whistleblower.

Ukitaka kuzuia mtu asiteuliwe CAG kwa sababu alifanya kazi serikalini, utakosa watu wengi sana wenye uzoefu.

Magufuli ana makosa mengi, mengi sana.

Tusimtungie makosa ambayo si yake.

Kufanya hivyo kutazidi kuipa nguvu hoja ya kwamba wanaompinga hawana hoja.
 
Cv yake haijatosha kabisa aisee hajapishana sana na mie mtoto wa mkulima wapo watu wengi wenye elimu uzoefu na weledi mkubwa sana waliofaa kuwa cag huyu sidhani
 
Duh kwahiyo hapo kichere atakuwa na miaka kama kumi hivi mbele kazini mpaka aje kustaafu
 
Ana elimu ya Ku unga unga sana kwenye ofisi ya CAG hatoshi pale panataka kichwa angalau chenye CPA.
 
Kwasababu pale Assad Associates(AA) hua wanasahihisha Booklets sio?

Naona umemchanganya na Palamagamba.
Ndiyo kastaafu miaka yake mitano,Boss hakumuongezea ingawa umri bado unaruhusu. Sasa arudi kusasihisha Booklets.
 
Nakumbuka Kuna Sheria ilipitishwa 2014 ikiwalenga wakurugenzi wote wa taasisi za umma watahudumu kwa vipindi vya miaka mitano mitano renewable Mara mbili tu means baada ya miaka 10 hawezi kuhudumu tena
 
Kichere angeonyesha msimamo wake kama Assad ingependeza sana,after jiwe hana mamlaka ya kutengua nafasi yake,I wish I were him ningefanya kazi yangu with integrity bila kumsikiliza meko

Sent from my Infinix HOT 4 using JamiiForums mobile app
 
Mie najiuliza, hakuonekana kutosha TRA, atatosha u-CAG?
Na kwa yale yaliyotokea, ni kama "keshakatwa mkia", atakuwa na ujasiri wa kusimamia misingi ya kazi yake kweli? Au inawezekana mteuzi nae amelizingatia hilo ili kujiondolea 'usumbufu usio wa lazima'?
 
Mambo ya hii nchi ukiyatafakari sana ni kujitia tu presha..mbaya zaidi hata upige kelele vipi kuna watu wamekaa sehemu wanasanifu tu huku wanakuna vitambi na tooth pick mdomoni..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…