CAG Prof. Assad astaafu, Charles Kichere ateuliwa kuwa CAG mpya

CAG Prof. Assad astaafu, Charles Kichere ateuliwa kuwa CAG mpya

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 144 kuhusu kumuondoa CAG madarakani

144.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katika ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Jamhuri ya Muungano atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka sitini au umri mwingine wowote utakaotajwa na Sheria
iliyotungwa na Bunge.
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hii.
(3) Iwapo Rais anaona kwamba suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwa ifuatavyo:
(a) Rais atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili. Huyo Mwenyekiti na angalau nusu ya wajumbe wengine wa Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji wa
Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola;
(b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa taarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lote na itamshauri Rais kama huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya ibara hii kwa sababu ya kushindwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya.
(4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote
au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini.
(5) Ikiwa suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu limepelekwa kwenye Tume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, Rais aweza kumsimamisha kazi huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi huo wa kumsimamisha kazi, na kwa hali yoyote uamuzi huo utabatilika ikiwa Tume itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu asiondolewe kazini.
(6) Mtu ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu au aliyepata kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hawezi kuteuliwa kushika au kushikilia madaraka ya kazi nyingine yoyote katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(7) Masharti ya ibara hii hayatatumika kwa mtu yoyote aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu.
 
Charles Edward Kichere

Charles Edward Kichere is a Njombe Regional Administrative Secretary (RAS) and former Commissioner General at Tanzania Revenue Authority (TRA).

He worked as Deputy Commissioner General at Tanzania Revenue Authority (TRA),
Head of Finance and Chief Accountant at Tanzania National Roads Agency (TANROADS),
Principal Internal Auditor at Tanzania National Roads Agency (TANROADS),
Internal Auditor at Tanzania National Roads Agency (TANROADS),
Internal Auditor at Unilever Tea TanzaniaL imited, and Internal Auditor/Treasurer at Unilever Tea Kenya Limited.

Charles E. Kichere holds Bachelor of Laws (LL.B) from Tumaini University College, Dar es Salaam Tanzania, Masters of Business Administration (MBA) in Finance at University of Dar es Salaam,
Diploma in Financial Management of Donor Funded Projects at Africa Renaissance Centre, Mbabane Swaziland,
Bachelor of Commerce in Accounting (B.Com Accounting) at University of Dar es Salaam. He is a member of the Credit and Audit Committees.
CV nyepesi sana.
 
That "Diploma in Financial Management of Donor Funded Project" is a joke. It was conducted in 3 weeks, what sort of a diploma is that? I went through the same "course" but I dare NOT tell people of it.
 
Prof Musa Assad amejiuzulu au amelazimishwa na kitengo kujiuzulu, au amestaafu
Kwa Mujibu wa katiba Muda wake imefikia Ukomo.

Raisi alikua na ridhaa ya kumuongezea muda ama kutomuongezea.
 
Waache wapige sasa jamaa atanunua Rocket la kwenda Mwezini ili kuvutia watalii.
Unajuwa ukiangalia hata hawa wasaidizi wake wakuu Samia na Majaliwa, wote ni wale wale. Sijisikii aibu kusemea nao ni wabovu na hawana hadhi ya kushika madaraka hayo waliyo nayo kama hawawezi kumshauri anapokwenda mrama na akikataa wao kuchukua uamuzi sahihi wa kiuongozi wa kujitoa na kutangaza hadharani sababu ni nini.
Hitimisho ni kuwa lawama za uongozi mbovu sio za MtuPori pekee bali viongozi hao wote.
 
Kama ni hivyo basi ni mbinu za kum shake kisaikolojia ili awe na adabu na mteuzi. Una panda cheo hadi Kamishna wa TRA una enjoy ukuu ghafla unapigwa mtama hadi kuwa RAS bila kutegemea na unanyong'onyea kisha unapewa madaraka yasiyo hojiwa na inakubidi ujikunyate kwa mteuzi kuwa ni mwokozi wako.
Haya mawazo wengi tunashindwa kuyaandika asante kwa kutusaidia
 
"Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda" - 2 Timotheo 4:7

Mungu akubariki Ustadh, the last of the dying breed, able to speak truth to power without fear. Kapumzike
Nimetoka kusikia wimbo huu kanisani nusu saa iliyopita.

Asante sana mkuu kwa kunionesha mstari wake.

Asante sana Assad kwa kuvipiga vita vilivyo vizuri, kuumaliza mwendo na kuilinda imani. Ubarikiwe sana.

Nchi yetu inakoelekea ni Mungu tu atunusuru. Tuishike mioyo.
 
Back
Top Bottom