Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Prof.Mussa Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano kwenye nafasi hiyo. Lakini Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (ambayo ndio sheria mama) haelezi hicho kinachoitwa "kipindi cha miaka mitano"
_
Katiba inaeleza kuwa CAG atakoma utumishi wake atakapotimiza umri wa miaka 60. Yani akifikisha umri wa miaka 60 anapumzika bila kujalisha ametumikia nafasi hiyo kwa muda gani. Iwe miezi miwili, miaka nane, au miaka kumi.
Ndio maana maCAG wote waliotangulia wameongoza ofisi hiyo kwa vipindi tofauti. Mzee Mohamed Aboud aliongoza kwa miaka 27 tangu 1969 hadi 1996. Thomas Kiama akaongoza kwa miaka 9 tangu 1996 hadi 2005. Ludovick Utouh akaongoza kwa miaka 8 tangu 2006 hadi 2014. Sasa hii kauli ya kusema Assad amemaliza kipindi chake cha "miaka mitano" imetoka wapi?
Matakwa ya kikatiba ni umri wa miaka 60, unless aondolewe kwa kushindwa kutimiza majukumu yake. Na ikitokea hivyo Katiba imeweka utaratibu wa kumuondoa kwa kuunda tume.
Lakini taarifa ya Ikulu inaeleza Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano. Je hiki kipindi cha miaka mitano Ikulu wamekitoa wapi? Kwenye sheria ipi? Kama ipo sheria hiyo ipo ni batili maana inapingana na katiba.
Na kwa kawaida unapotokea mgogoro kati ya sheria na katiba, basi Katiba ndiyo inayoshika hatamu (When a state law conflicts with a Constitution, then constitution prevails because constitution rules supreme above all state laws).
_
Prof.Assad amezaliwa tar.06 October mwaka 1961. Kwa sasa ana umri wa miaka 58. Atafikisha umri wa miaka 60 October 06 mwaka 2021. Hivyo kwa mujibu wa KATIBA alipaswa kustaafu nafasi yake ya CAG akifikisha umri huo, na si kwa hiki kinachoitwa "miaka mitano". I stand to be corrected.!
View attachment 1252811