CAG Prof. Assad astaafu, Charles Kichere ateuliwa kuwa CAG mpya

CAG Prof. Assad astaafu, Charles Kichere ateuliwa kuwa CAG mpya

Ila ajabu huyu mteuliwa upya nae ana miaka 59..kwaio mwakani anakua elligible kustaafu hivyo kama ataficha vizuri mambo flani ya mtoto wa dada atakua extended au anaweza pigwa chini akaletwa mwingine ila huyu ataendelea kula maisha maxuri ya pensheni...
 
Atastaafia pazuri mzee baba.
 
Atastaafia pazuri mzee baba.
Ila hadi sasa hivi ni 5 - 0 hatutasikia habari zozote zile za kuhusu ufisadi ama ubadhirifu ni mwendo wa mapambio kwenda mbele ila jamaa ana roho mbaya hatari Assad kesho ndo tarehe yake ya kustaafu hivyo jamaa ametaka jamaa akakabidhi mikoba siku ya kesho..daah
 
Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Prof.Mussa Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano kwenye nafasi hiyo. Lakini Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (ambayo ndio sheria mama) haelezi hicho kinachoitwa "kipindi cha miaka mitano"
_
Katiba inaeleza kuwa CAG atakoma utumishi wake atakapotimiza umri wa miaka 60. Yani akifikisha umri wa miaka 60 anapumzika bila kujalisha ametumikia nafasi hiyo kwa muda gani. Iwe miezi miwili, miaka nane, au miaka kumi.

Ndio maana maCAG wote waliotangulia wameongoza ofisi hiyo kwa vipindi tofauti. Mzee Mohamed Aboud aliongoza kwa miaka 27 tangu 1969 hadi 1996. Thomas Kiama akaongoza kwa miaka 9 tangu 1996 hadi 2005. Ludovick Utouh akaongoza kwa miaka 8 tangu 2006 hadi 2014. Sasa hii kauli ya kusema Assad amemaliza kipindi chake cha "miaka mitano" imetoka wapi?

Matakwa ya kikatiba ni umri wa miaka 60, unless aondolewe kwa kushindwa kutimiza majukumu yake. Na ikitokea hivyo Katiba imeweka utaratibu wa kumuondoa kwa kuunda tume.

Lakini taarifa ya Ikulu inaeleza Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano. Je hiki kipindi cha miaka mitano Ikulu wamekitoa wapi? Kwenye sheria ipi? Kama ipo sheria hiyo ipo ni batili maana inapingana na katiba.

Na kwa kawaida unapotokea mgogoro kati ya sheria na katiba, basi Katiba ndiyo inayoshika hatamu (When a state law conflicts with a Constitution, then constitution prevails because constitution rules supreme above all state laws).
_
Prof.Assad amezaliwa tar.06 October mwaka 1961. Kwa sasa ana umri wa miaka 58. Atafikisha umri wa miaka 60 October 06 mwaka 2021. Hivyo kwa mujibu wa KATIBA alipaswa kustaafu nafasi yake ya CAG akifikisha umri huo, na si kwa hiki kinachoitwa "miaka mitano". I stand to be corrected.!View attachment 1252811
Sasa nime elewa (shukrani mkuu), kama ni hivyo basi mkulu amesigina katiba labda tuhakikishiwe vinginevyo. Hapa umejibu hoja kwa hoja.
Apparently kuna kifungu kingine kinatembea huko (Katiba inazidi kuvunjwa, Profesa Assad hakustahili kustaafishwa kwa mujibu wa katiba ibara ya 144) nacho kinaongelea kuwa CAG atakuwa na fixed term ya miaka 5 na anaweza kuchaguliwa tena kwa miaka 5. Na hapo hapo eti akifikisha 65 lazima aachie ngazi. Bahati mbaya bado sijapata tarehe za "vifungu hivi vya katiba". Kama ni hivyo basiJPM yuko ndani ya sheria.
 
Ila hadi sasa hivi ni 5 - 0 hatutasikia habari zozote zile za kuhusu ufisadi ama ubadhirifu ni mwendo wa mapambio kwenda mbele ila jamaa ana roho mbaya hatari Assad kesho ndo tarehe yake ya kustaafu hivyo jamaa ametaka jamaa akakabidhi mikoba siku ya kesho..daah
Utazisikia wapi tena mzee baba maana mteuliwa ameshanyooshwa kwanza kabla ya kurudishwa mjini hapa,ni full adabu sasa.

Kuna sehemu nimeona Assad amesema hana habari na kutenguliwa na yuko zake safarini kikazi.
 
Tuyapigwa hels yetu mchana kweupe na tutakuwa tuna ambiwa hati safi kila mahali maana ukimwangalia tu ni mtu wa kujipendekeza
 
Apparently kuna kifungu kingine kinatembea huko (Katiba inazidi kuvunjwa, Profesa Assad hakustahili kustaafishwa kwa mujibu wa katiba ibara ya 144) nacho kinaongelea kuwa CAG atakuwa na fixed term ya miaka 5 na anaweza kuchaguliwa tena kwa miaka 5. Na hapo hapo eti akifikisha 65 lazima aachie ngazi. Bahati mbaya bado sijapata tarehe za "vifungu hivi vya katiba". Kama ni hivyo basiJPM yuko ndani ya sheria.
Public Audit Act 2008 - imeweka wazi juu ya hichi kitu, ni miaka mitano upon renewal! Msome
 
Hivi huyo kichere sio msukuma kweli?
Kila dalili inaonyesha hata ni wa Chato ili sasa hazina ihamie Ikulu ya home badala ya Dodoma. Katika miaka minne ya awamu hii huyu CAG mpya ameteuliwa na kutenguliwa mara kadha dalili kuwa ni homeboy. Tumekwisha!
 
Naona yule jamaa wa kule Dodoma atakuwa anafurahia sana hii habari.
Duu ukweli au uongo embu Wana Jamvi dadavueni
IMG-20191103-WA0022.jpeg
 
Ila ajabu huyu mteuliwa upya nae ana miaka 59..kwaio mwakani anakua elligible kustaafu hivyo kama ataficha vizuri mambo flani ya mtoto wa dada atakua extended au anaweza pigwa chini akaletwa mwingine ila huyu ataendelea kula maisha maxuri ya pensheni...
Naona somo la hisabati kwako lilikuwa noma!
2019 - 1970 = 49 Hesabu ya kutoa na kukopa tu ndugu yangu imekushinda na kuambulia zero. Ingalikuwaje kama ingalikuwa ya differentiation tuliyokuwa tunafundishwa darasa la kumi?

Prof Asad ndiye yuko 59. Hivyo second tenure of office ya miaka 5 kwake haingewezekana kwani mwakani angekuwa 60, umri ambao lazima astaafu kwa mujibu wa sheria. Kichere yeye ataweza kupiga terms zote 2 kabla ya kufika umri wa kustaafu kwa lazima. Atakuwa 59 at the end of his second tenure!
 
CHADEMA wataangua Vilio kumlilia Prof. Assad
Why CHADEMA? Kwa sababu unajua wamemsifia prof Assad kwa kusimamia vizuri taaluma yake,, na pia wanapiga kelele kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali za nchi huku ukikaa kumshangilia anayewanyima haki kama vile wewe siyo raia wa Tanzania, sad!
 
Ninachojua Rais Magufuli hajawahi kuwa serious na vita anayopigana na siku akiwa serious anaweza kuwa Rais bora.
Alichofanikiwa ni kutumia kodi zetu kutengeneza wafuasi ya dini yake mpya ya kusifia kila kitu na hapa anaenda kufanikiwa, ni dhahiri kila siku bajeti ya kutengeneza waimba mapambio inaongezeka wakati ile ya kuondoa umasikini kwa raia wa kawaida ikipungua.
Hivi unaweza kuwa na Rais mwenye uchungu wa nchi( sio anayependa kusifiwa hata kwenye ujinga) akakuaminisha kuwa huyu hafai kuwa boss wenu kwenye swala nyeti la kukusanya mapato halafu baada ya muda anakuambia huyu ndio boss wenu kwenye kuchunguza matumizi ya hela yenu.
Ikumbukwe Rais Magufuli hakulazimishwa kumtengua huyu mtu, alituambia mwenyewe huyu hatoshi....Sasa kama Rais yupo serious na vita anayopigana katika Watanzania wote huyu alituambia kashindwa kapata wapi ujuzi haraka kuwazid waliobaki?
Kwakuwa hajavunja katiba kumteua huyu mtu basi tunaendelea kunyamaza kama tulivyonyamaza baada ya kutujazia makada kwenye nafas za utendaji.
Kitu tunatakiwa kufanya kwa sasa ni kumuacha Rais Magufuli afanye atakavyo hata akitaka kuongeza muda wa kubaki madarakani muacheni nchi itamshinda ataanza kupigana na CCM wenzake na hapo ndio atajizika mwenyewe.
 
Back
Top Bottom