CAG: TSh. milioni 140 ambazo Wizara ya Maliasili na Utalii iliilipa kampuni ya Wasafi hazikuwa na Mkataba uliosainiwa

CAG: TSh. milioni 140 ambazo Wizara ya Maliasili na Utalii iliilipa kampuni ya Wasafi hazikuwa na Mkataba uliosainiwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza kuwa Sh140 milioni ambazo Wizara ya Maliasili na Utalii iliilipa kampuni ya Wasafi hazikuwa na mkataba wowote uliosainiwa.

Wizara hiyo ililipa fedha hizo kwa ajili ya wasanii ambao wangetangaza utalii wa ndani katika mikoa sita nchini Tanzania.

Akizungumza leo Alhamisi Aprili 8, 2021 katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma CAG, Charles Kichere amesema, “Wizara ililipa Sh140 milioni kwa kampuni ya Wasafi kwaajili ya wasanii ambao wangetangaza utalii wa ndani katika mikoa sita, hata hivyo hakukuwa na mkataba wowote uliosainiwa baina ya wizara na kampuni ya Wasafi na kushindwa kuhakiki wigo na huduma iliyotolewa na kampuni ya Wasafi.”

Amesema kiasi hicho cha fedha kilicholipwa kwa Wasafi hakiendani na sheria za matumizi ya fedha za umma.

Amebainisha upungufu uliobainika katika uanzishwaji wa tamasha la Urithi haukuwa na nyaraka zilizowasilishwa kwa ajili ya ukaguzi kuhusu matumizi hayo pamoja na Sh487 milioni zilipelekwa kwenye taasisi saba na kwamba hakukuwa na nyaraka zilizowasilishwa kudhibitisha matumizi hayo.

“Matumizi ya Sh585 milioni yaliyolipwa na mhasibu wa mfuko wa tozo ya maendeleo ya utalii hayakuwa na nyaraka toshelezi na kushindwa kudhibitisha uhalali wa malipo hayo,” amesema

Chanzo: Mwananchi Online
 
Wewe una wekeza wasanii kwenye usanii mazao yake si yanajulikana usanii
 
Ndomana bwana yule hv karibuni aligeuka mshauri kwa mama yetu....
By the way haya ya upigaji hayotoisha kinachotakiwa ni mfumo imara na adhabu kali kwa wabadhilifu ili iwe fundisho na kukoma kwa mambo ya kuchezea pesa za uma kizembe namna hyo
 
Uyu muhuni Ela zote alikua anapeleka kwa waganga.
IMG_20210404_182550.jpg
 
Huyu jamaa alikuwa wpi kipindi cha marehemu JPM? Mbona anataka kutuchonganisha na mwenda zake .
 
WAKATI WA KAMPENI JAMAA ALIGAWA BODA BODA ZENYE THAMANI YA SHS MIL 200 JIMBONI KWAKE.SO UNADHANI HIZO PESA JAMAA ALIZIPATA WAPI MZEE BABA?
 
Back
Top Bottom