CAG: TSh. milioni 140 ambazo Wizara ya Maliasili na Utalii iliilipa kampuni ya Wasafi hazikuwa na Mkataba uliosainiwa

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza kuwa Sh140 milioni ambazo Wizara ya Maliasili na Utalii iliilipa kampuni ya Wasafi hazikuwa na mkataba wowote uliosainiwa.

Wizara hiyo ililipa fedha hizo kwa ajili ya wasanii ambao wangetangaza utalii wa ndani katika mikoa sita nchini Tanzania.

Akizungumza leo Alhamisi Aprili 8, 2021 katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma CAG, Charles Kichere amesema, "Wizara ililipa Sh140 milioni kwa kampuni ya Wasafi kwaajili ya wasanii ambao wangetangaza utalii wa ndani katika mikoa sita, hata hivyo hakukuwa na mkataba wowote uliosainiwa baina ya wizara na kampuni ya Wasafi na kushindwa kuhakiki wigo na huduma iliyotolewa na kampuni ya Wasafi."

Social -mwananchi update
 

Attachments

  • Screenshot_20210408-154616.jpg
    49.2 KB · Views: 2
  • globalpublishers-___CNZ46h0DOzj___-.jpg
    95.6 KB · Views: 2


"Katika mahojiano na waziri (Dk. Hamis Kigwangalla), alikiri kampuni ya Wasafi iliomba zabuni ya kutangaza tamasha la utalii, na kutoa maagizo ya kutolewa malipo hayo. Kwa maoni yangu, Sh.140 mil walicholipwa, hakiendani na sheria ya matumizi ya umma." - Charles Kichere, CAG.
 
Mara paap , jiwe kaamka , spatii picha jins mkutano wa waandishi wa habar utakavyotawanyika πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜€πŸ˜€ na CAG kutokomea kusikojulikana πŸ™„, mana si Kwa spana hz wanazompiga, lakni jiwe si alimwajibisha kigwangala Kwa kumtimua uwazir
 
Waziri mwenye dhamana bila shaka alikuwa ni Hamis Kigwangala. Ni vyema akachukuliwa hatua pamoja na hao wahuni wenzake ili wazirejeshe hizo fedha za serikali.

Wakileta ujuaji, wafilisiwe tu mali zao. Muda wa kucheka na nyani umekwisha.
 
Kigwangwala huko haja ndefu inagonga chupi inarudi ndani.
 
Kigwa hajawahi kufukuzwa uwaziri.
 
Mjomba CAG ukifika kwenye NEC utanishtua mi nasinzia kidogo.
 
Kwani kupoteza uwaziri nayo ni adhabu,mbona wengine wanasota jela kwa kesi za utakatishaji fedha,kushirikiana na magege ya kiharifu,ubadhirifu wa mali ya umma na tuhuma kibao za kubambikiziwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…