CAG: Uwanja wa Ndege Chato ni mradi usio na faida

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,494
Reaction score
96,074
Tulisema tukaitwa wapinzani tuna wivu.

Sasa wenye mamlaka wa kusema wamesema.

--
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema gharama za ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita zilizidi bajeti iliyotengwa kwa sababu ulifanyika bila upembuzi yakinifu.

CAG alisema kutofanyika kwa upembuzi yakinifu kunaongeza hatari kwa Serikali kuwekeza katika mradi usio na tija na uwezekano wa kuwapo gharama zisizodhibitiwa na ongezeko la muda katika utekelezaji wake.

“Mpatio yangu yalibaini Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) hawakufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuanz aujenzi,” amesema Kichere.

CAG Kichere amesema Sh3.62 bilioni za mradi huo zilitolewa kwenye miradi mingine kwa matarajio kwamba zingerejeshwa baada ya Hazina kutoa fedha zake, jambo ambalo halikutekelezwa kwa wakati hivyo kusimamisha miradi mingine iiliyopangwa.
 
Tulisema tukaitwa wapinzani tuna wivu.

Sasa wenye mamlaka wa kusema wamesema.

.https://www.instagram.com/p/CcUyVOhtBIe/?igshid=YmMyMTA2M2Y=
Hivi uwanja wa ndege wa Chato unatofauti gani na Uwanja wa Ndege wa Musoma unaojengwa? Au wa Mtwara? Hizo faida anazotaka CAG ni zipi? Zionekane baada ya mda fani? Maana nina hakika ata ujenzi wa terminal 3 Mwaimu Nyerere bado hatujaanza kupata faida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo uwanja wa Chato ulikuwa na umuhimu gani kujengwa chato wakati kuna uwanja wa Mwanza na pale Bukoba?
 
Tulisema tukaitwa wapinzani tuna wivu.

Sasa wenye mamlaka wa kusema wamesema.

.https://www.instagram.com/p/CcUyVOhtBIe/?igshid=YmMyMTA2M2Y=
Hata mobutu seseseko kuku wa zebanga alijenga uwanja MKUBWA wa ndege kijijini kwao lakini baada ya kifo chake kiwanja hicho kimekuwa uwanja wa kuchungia mbuzi.....
Afrika siasa Ni ngumu kuliko fizikia..
 
Tofauti ni kuwa viwanja vya Musoma na Mtwara vimejengwa miji mikuu ya mikoa sehemu ambazo kuna watu na biashara nyingi wakati uwanja wa Chato umejengwa kijijini kwenye watu wachache ni biashara chache!
 
Una tofauti kubwa ndugu yangu. Ukitaka kujua jaribu kufikiri uwanja wenye hadhi ya Chato ujengwe chalinze au Mwanga. Ungeona ni sawa?
 
Kulikuwa na uharaka gani wa kujenga uwanja Chato wa runway ya kimataifa bila idhini ya bunge?? Hivyo viwanja vingine viko kwenye mpango kazi wa TAA

Mkuu Mpinzire hebu shirikisha ubongo wako japo kwa dakika 5
 
Badala ya kulilia legasi ni vema ukatueleza ni lini tutapata faida na itatokana na nini
 
Sio sgr tuu tukianza kuongelea miradi tanzania hii ni mingi ikiwemo chato. Kukosa mlengo kama taifa na dira kuu ni chanzo cha yote aya.

Nilitaka sahau mzizi wa yote aya ni CCM. Pamoja na kuhusisha vyeo vya kiutendaji pamoja na siasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…