Waswahili tabu sana, mtu yuko Buza kwa Mama Kibonge na anashindia chai ya rangi na kitumbua kimoja halafu anajifanya kufahamu uwezo wa Iran kijeshi kuliko intelijensia zote za nchi za magharibi zinavyofahamu [emoji23][emoji23][emoji23]
Swala la Iran limewekwa kiporo kwa sasa na litashughulikiwa kikamilifu mwaka 2025 ie baada ya uchaguzi wa Marekani kumalizika mwakani.
Mazingira yenye kuhalalisha Iran kushughulikiwa tayari yameshaandaliwa hivyo ni swala la muda tu na ratiba ndio sasa inaandaliwa na David Cameron hakuongea kwa bahati mbaya.
Iran ameandaliwa mtego bila ya yeye kufahamu na kajiingiza mzima mzima. Iran bado ipo katika harakati zake za kutafuta kufikia uwezo wa kumiliki silaha za nuklia japo kwa sasa inasemekana wamefikia 60% ya urutubishwaji ikiwa ni pungufu ya uwezo wa kutengeneza silaha za nuklia kwa 25%.
Iran weighs the pros and cons of becoming a nuclear power. The consequences of the decision will be immense for its friends and foes.
www.gisreportsonline.com
Inasemekana ili kufikia uwezo huo Iran inaweza ikahitaji miaka 5 au zaidi na ndio maana sasa inasemekana wakati wa kuiwahi Iran umefika na hakutakuwa na kizuizi zaidi.
They say,
"strike while the iron is hot."