SnowBall
JF-Expert Member
- Sep 13, 2011
- 3,052
- 2,842
- Thread starter
- #41
Umeandika vizuri sana...ninachogundua kwako ni kuwa sio kweli kwamba hatuoni..ila 'tunaona' lakini haitushughulishi sana kuchukua hatua kwa yele tuyaonayo..ryte?. Kwa sababu tukiamua kuona kwa macho ya ukweli tutakwazika na neno 'penzi' halitanoga...lolz...Labda tu nikuulize..Unaweza kuishi kwa kuujua ukweli unaouma?..au ni vizuri kutotaka kujua kwa sababu haitasaidia???
Kupenda tu kwenyewe ni 'myth'
Si kweli kwamba ukipenda mtu unakuwa blind, siamini hili
Ila kinachokuwepo ni kuwa, ukiwa mapenzini kuna kawaida ya kuyafumbia macho mapungufu ya mtu
Hata yale mapungufu yanayoudhi kabisa, unayavumilia kwa sababu tu, gharama ya kuvumilia mapungufu hayo unaona NAFUU kuliko gharama ya kumpoteza mtu huyo.
Kuvumilia kutokuwepo kwani inakuwa 'aghali' sana kuliko kuvumilia mapungufu yake.
Kama ujuavyo, ukiamua kufumbia macho na kuendelea naye, itafika mahali yule mtu unamzoea, hapo sasa gharama ya mapungufu inaanza kuwa unbearable. Ikizidi sana ndio watu huachana, unabaki kujiuliza, kwani hakuona mapungufu yake kabla hajakubali?
Kumbe ilikuwa kiwewe cha penzi bichi au changa