CANVAS Business Model

CANVAS Business Model

Nina MBA na CPA.

Business models za vitabuni kwa africa ni ngumu sana na wengi wanafeli. Ila watu kama sisi tunazidigest, getting back to the basics and skeletons kisha nitakucoach fanya ABCD.....

Biashara siol lazima uwe mchawi au uende kwa mganga, biashara ni sayansi
Mkuu samahani, hivi ni mtu yoyote anayezingatia kanuni za biashara anaweza kuwa mfanya biashara au ni mtu maalum aliejaliwa Karama ya biashara ndie anapaswa kuwa mfanya biashara?
 
Nina MBA na CPA.

Business models za vitabuni kwa africa ni ngumu sana na wengi wanafeli. Ila watu kama sisi tunazidigest, getting back to the basics and skeletons kisha nitakucoach fanya ABCD.....

Biashara siol lazima uwe mchawi au uende kwa mganga, biashara ni sayansi
Sasa wanasayansi wa biashara kama nyie ndio mnahitajika kwa wingi. Sikufichi nina degree ya biashara ila kuifanyia kazi hata theluthi ya knowledge siwezi. Kama ni biashara tunafanya basics tu kuuza na kununua tu ila kuna mambo mengi mno kwenye biashara. Biashara zetu nyingi hata kuzipima kwenye mizani huwezi
 
Canvas Business Model ni aina gani ya biashara Wakuu?....
Ni strategic tool tu ambayo inatumika kuisummarize biashara kwa ufupi kuelezea activities zake, resources zinazohitajika, revenue collections, customer identification etc. Ni famous tool kwaajili ya wepesi wake wa kueleweka when it comes to how you do business.
 
Niliapia sitokuja kuongelea kitu chochote serious humu JF zaidi ya pombe na ngono ila ngoja leo nikushauri kitu sababu nimeona sana mabandiko yako na sijui kwanini yananiangukia

Nimefanya kazi za kuallocate funds kwenye startups kutoka kwenye foundations kadhaa nje na ndani ya nchi. Wengi ni wanasiasa kama wewe(usiishie kusoma hapo, vuta pumzi tuendelee). Wanalenga kutoa first impression kwa maneno mataam lakini biashara zao ni zero. Startups nyingi zinakufa hata kama walipewa funds sababu executives na founders ni wanasiasa tu, wanajua theory ya biashara na maneno mazito ya kutongoza investors ila hawajui kuendesha biashara kutokana, kutumia data, takwimu na saikolojia ili kufanya biashara iwe profitable zaidi.

Siku hizi nikisikia neno startup nataka hadi kutapika. Cheki kuna waghana flani walipata hadi usd 86 million wanajiita DASH ila kampuni limekufa, nenda kwa jirani zako JUMIA wako wapi sasahivi? Startups za hapa Tanzania ndo sitozitaja sababu founders lengo lao ni kupata funds wakanunue brevis wajenge nyumba then wafunge biashara.

Sasa mimi nakuomba kitu kimoja tu. Takwimu za biashara zako katika makundi haya.

1)Zitakazonifanya NIWEKEZE kwenye biashara yako
2)Zitakazonifanya NISIWEKEZE kwenye biashara yako.

Hapo kwenye takwimu nataka zote ambazo unatumia kwenye biashara yako kama vile customer follow ups, leads to client ratio, stock turnover, na statistics zote (kama una utimamu wa biashara utajua namaanisha zipi)
lkn pia ambatanisha financial statements za toka mwaka ulioanza kufanya business hadi mwaka huu.

Nitumie PM na kama nitapenda ninachokiona nina 15million hapa cash imekaa inasubiri kufanyiwa starehe tu, nitawekeza nusu kwenye biashara yako. Ukiona risk kunitumia nambie nikupe calendar yangu uchague siku tuonane ofisini kwangu, nitakua na cash ww uje na hizo data.

Good luck sweetheart.
Nimeenda hii. Naomba nikucheki kwa personal issues. Hii ya siasa na executions kama inameki sensi hivi. Kunakuwaga na kigepu hapa katikati kinachofanya kampuni nyingi kuwa vilevile miaka 100 ijayo
 
Huu ni ukweli usiopingika, actually Startups ni kachimbo kapya ka watu kupigia hela lakini pia sio Founders wote. Kuna baadhi wako smart sana tu kwenye solutions zao, nimekutana nao baadhi, wana visions lakini bahati mbaya wanazokutana nazo baada ya kupata Investors, investors wanakuja kama kutake over na kuanza kurun biashara kama wanavyoona wao kwakuwa wanapower ya capital kitu ambacho kinapelekea mpaka founders visions zinakufa, ukifatilia cases nyingi ziko hivo mpka hata kwa Elon Musk alvoanzisha Paypal. Ila all in all kuna Real people who want to solve real problems na kuna wapigaji kwa mgongo wa Startups na NGOs.
🥴🤫
 
Nimeenda hii. Naomba nikucheki kwa personal issues. Hii ya siasa na executions kama inameki sensi hivi. Kunakuwaga na kigepu hapa katikati kinachofanya kampuni nyingi kuwa vilevile miaka 100 ijayo
Ni strategy tu, kampuni nyingi hazina strategies nzuri, mtu hajui miaka kumi ijayo Biashara yake itakuwa wapi?
Achilia mbali kumi hata miaka miwili hana goals wala haendi na kasi ya technology


NB: raha ya ngoma uingie ucheze


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heshima kwenu wakuu
Siku kadhaa nyuma niliweka andiko hapa lakutafuta mwekezaji kwenye biashara yangu, na nikapokea calls, SMS na Pms kadhaa zingine walitaka kujua nafanyaje fanyaje ili kuweza kuendeleza game na uzuri pia kuna wanaonifahamu physicaly so haikuwa ngumu kwao kuamini nilichoandika.

Mimi natumia CANVAS BUSINESS MODEL
Yenye vipengele 9, vipengele hivi kwa pamoja ndivyo vinavyobeba Biashara yako
1. Key Partners
Hawa ni watu ambao utashirikiana nao kufanikisha biashara yako mfano mimi naweza sema ni wauza malighafi, wakulima, nk

2. KEY ACTIVITIES
Hapa sasa biashara yako itakuwa inafanya nini? Mfano mimi nazalisha vipodozi.

3. KEY RESOURCES
Hapa ni vifaa gani au resources gani zitahitajika ili ufanikishe mfano mimi ni cash, machines, nk

4. VALUE PREPOSITION
Hapa sasa ni utofauti wako wewe na washindani wako, yaani utafanya nini ambacho kitaleta wateja kwako kutoka kwa washindani wako waje kwako.

5. CUSTOMER RELATIONSHIP
Hapa sasa ni mbinu gani utakazozitumia kuhakikisha unakuwa na mahusiano yasiyokoma na wateja wako, yaani wateja wasisahau uwepo wako kila watakapopata huduma.

6. CHANNELS
Utatumia channels gani kuwafikia tupo kwenye dunia ya tiktok ya IG ya websites nk so utatumia channel ipi (hapa uwe makini sana sana usije tumia whatsapp akati ni Biashara ya utalii)

7. CUSTOMER SEGMENT
Hapa sasa unamjua mteja wako ni nani mfano unauza madaftali ya watoto wa vidudu mtumiaji ni mtoto ila mteja wako ni mzazi (hapa nimuhimu sana kumjua mteja wako hapa ndipo utajua kipato cha mteja wako nk)

8. COST STRUCTURE
hapa sasa ndo utajua mwenendo mzima wa biashara yako na utatumia kiasi gani kuzalisha pisi ngapi,au kodi,mishahara nk

9.REVENUE STREAM
hapa ndo utajua sasa namna yakutengeneza pesa, yaani pesa itamzaaje mwenzake

LAKINI YOTE KWA YOTE
ZINGATIA FEEDBACK

Ni kipengele muhimu sana kwenye biashara yoyote ile,
Kuna aina mbili za feedback.

1. Feedback kutoka kwa wateja

2. Feedback kutoka kwa wazoefu wa biashara

Feedback kutoka kwa wateja zitakufanya ujue ni wapi unakosea kwenye bidhaa/huduma unayouza, wateja wanatarajia nini kutoka kwako, utaboreshaje huduma/bidhaa yako. Ndomana ni muhimu.

Feedback ya wazoefu wa biashara itakusaidia kukushape wew ambae unafanya biashara katika mipango yako, mbinu, uendeshaji, changamoto na utatuzi wake n.k. kuna muda unaweza kujiona uko sawa kwakila kitu kwasababu wew ndo muanzilishi wa biashara lakini kiuhalisia kuna vitu unakosea na kwasababu umejiwekea wewe ndo wewe huwezi kuskiliza thirdy party you will learn it in a hard way utachoma pesa mpaka uje kugundua kwamba ulikuwa unakosea sehmu ushaiva sana na hamu ya biashara huna tena so feedback from Outside is very important.

Jamani
Poleni kwa gazeti afu wale wajuaji wenzangu namie nilipokosea njooni msahihishe tu mimi sio mwalimu jamani just sharing kile ninachofanya mimi


Picha kwa udhamini sio kila Biashara ni startup
Salum Awadh


View attachment 2797417
Kwa sisi ma Transporter mbona kama vile haitusaidii
 
Sasa wanasayansi wa biashara kama nyie ndio mnahitajika kwa wingi. Sikufichi nina degree ya biashara ila kuifanyia kazi hata theluthi ya knowledge siwezi. Kama ni biashara tunafanya basics tu kuuza na kununua tu ila kuna mambo mengi mno kwenye biashara. Biashara zetu nyingi hata kuzipima kwenye mizani huwezi
Juzi juzi nimesikia umeingia kwenye udalali wa magari na viwanja. Unajiita corporate conglomerate agency pale lumumba.

Na umemtafuta mtu umempa hela akawa anakupigia kampeni eti kijana una kitu, utafika mbali 😀.

Hizi digrii zetu hizi michongoma kichizi.. Nimekaa NGO moja mwaka Jana mtaalamu nimemuweka nadharia moja ambayo anaiandikia proposal kila siku lakin kwenye graundi imemshinda na akatimuliwa wiki hiyohiyo.
 
Ni strategy tu, kampuni nyingi hazina strategies nzuri, mtu hajui miaka kumi ijayo Biashara yake itakuwa wapi?
Achilia mbali kumi hata miaka miwili mbili hana goals wala haendi na kasi ya technology


NB: raha ya ngoma uingie ucheze


Sent using Jamii Forums mobile app
I know this. Niko na kampuni moja hapa tumejibrand vya kutosha na wateja wamepatikana. Kiongozi wetu anasema brand yetu kubwa tuongeze Bei zetu. Bos wake kaja kapinga, anasema unaweza kuongeza Bei uliowapata ukawapoteza.

Task: how and which strategies to adopt, itakayohakikisha hawa uliokuwa nao utakuwa nao kesho na kesho?.

NB : Mimi sio mtaalam wa marketing
 
I know this. Niko na kampuni moja hapa tumejibrand vya kutosha na wateja wamepatikana. Kiongozi wetu anasema brand yetu kubwa tuongeze Bei zetu. Bos wake kaja kapinga, anasema unaweza kuongeza Bei uliowapata ukawapoteza.

Task: how and which strategies to adopt, itakayohakikisha hawa uliokuwa nao utakuwa nao kesho na kesho?.

NB : Mimi sio mtaalam wa marketing
Boss wake yupo sahihi na huyo kiongozi wako kilaza (sorry to say this)
kwa uzoefu wangu kidogo nilio nao mnatakiwa mfanye mambo mawili tu
1. Muangalie namna yakupunguza matumizi
2. Muongeze mauzo ambapo revenue itaongezeka na ikiongezeka means faida inaongezeka pia
Sasa namna yakuongeza mauzo ndo hapo mpambane


NB: BIASHARA SIO RAHISI
 
Back
Top Bottom