SI KWELI Captain Ibrahim Traoré ajenga nyumba mpya za bure kwa wananchi wa Burkina Faso

SI KWELI Captain Ibrahim Traoré ajenga nyumba mpya za bure kwa wananchi wa Burkina Faso

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu
====
Nimekutana na hii video inasemakana ni nyumba za bure kwa wananchi wa taifa la Burkina Faso kuna ukweli wa taarifa hii?



1750669998807.png
 
Tunachokijua
Captain Ibrahim TRAORÉ ni Rais wa kijeshi chini Burkina Faso aliyefanya mapinduzi ya kumtoa Rais wa wa mpito wa wakati huo ambaye alikuwa ni mwanajeshi pia Paul-Henri Sandaogo Damiba September 2022. Aidha Captain Ibrahim anatajwa kuwa miongoni mwa marais wenye umri mdogo zaidi barani Afrika na duniani.

Zipo picha na video ambazo zilianza kusambaa mtandaoni tangu mwezi Mei, 2025, zikionesha majengo ya ghorofa ambayo yanadaiwa kuwa ni mradi unaotekelezwa na Rais wa Burkinafaso Kapteni Ibrahim Traoré kwa ajili ya kutoa huduma ya makazi bila malipo kwa raia wa nchi hiyo.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search ulibaini kuwa picha na video hizo zilichapishwa kutoka kwenye mradi wa Shirika la Kitaifa la Uboreshaji na Maendeleo ya Makazi (AADL) ulioko nchini Algeria. Hivyo picha hizo hazina uhusiano wowote na nchi ya Burkinafaso.

Pia ipo video iliyochapishwa katika mtandao wa Facebook wakati ujenzi wa majengo hayo ukiendelea, sehemu ya video inaonesha uwepo wa magari ambayo yana namba za usajili 'plate number' zinazofanana na zile ambazo hutumiwa nchini Algeria na si Burkinafaso. Vilevile mtumiaji mwingine wa mtandao wa huo alichapisha video Februari 1, 2025 ya majengo hayo akitaja kuwa mradi wa AADL, Koraichi Reghaiya eneo lililopo nchini Algeria.

Aidha Google Earth inabainisha muonekano wa eneo la Koraichi Reghaia lililopo nchini Algeria, ambapo ndipo majengo hayo yanapatikana.
screenshot-2025-06-24-141839-png.3381371
screenshot-2025-06-24-142357-png.3381372
Back
Top Bottom