​
Taarifa zilizonukuliwa na vyombo vya habari ni kuwa Kapt. John Komba amefariki kutokana na shinikizo la damu (i.e Immediate cause), lakini kwa wale waliofuatilia kwa makini mwenendo hadi mauti ya mwanamuziki, kipenzi cha watanzania, kada na mwanachama mwaminifu wa CCM marehemu Komba waatakubaliana nami kuwa chanzo cha hilo li presha kilikuwa ni kuzidiwa kwa madeni, madeni yaliyopelekea kupigwa mnada nyumba zake na mali zake mbali mbali.
You got me wrong my brother! Polisi wanachofanya ni ukatili na unyama wa hali ya juu na Premier Pinda kuagiza wananchi tupigwe ni kauli inayokinzana na utawala wa sheria(ni kauli ambayo inaweza sikika kwenye nchi ambayo haina utawala wa sheria tu) and to set the record straight nilipambana against Pinda kwa kauli yake, Mauaji ya Albino yananisikitisha na kunihuzunisha kuliko! jaribu kupitia comments zangu kwenye threads zilizotoa habari za mauji ya Albino utajua ukweli, Tafuta comments zangu kuhusu mauaji ya Mwangosi huwa sikai upande wa madhalimu yanayomwaga damu ya watu wasio na hatia ili kulinda madaraka yao ambayo watayaacha na kurudi mavumbini(maana HAKIka wote tutakufa na Mungu atatuhukumu kwa matendo yetu bila kuangalia huyu alikuwa kiongozi au muongozwa)!, Hapo mwisho umeniweka kwenye kundi la watawala wa sasa which is absolutely wrong! I'm also a victim of on going brutality but not letting my condition of being oppressed affect my position of humanity na kufurahia kifo cha mtu
Umesema sahihi kabisa CCM wana matatizo kibao. Hoja yangu kubwa je tuna mbadala? Kwa upande wangu naona hatuna mbadala.
Sasa unataka kutuaminisha nini au ndio mwendelezo wa unafiki wa Kitanzania!​Swali ninalojiuliza hadi sasa ni kuwa Wako wapi Marafiki wa Lowasa kumsaidia huyu komba hadi adhalilike kiasi kile? Kwanini afe kwa kuzidiwa na madeni wakati rafiki yake mkuu anagawa rushw kla kukicha? Kwa nini ilishindikana kumsaidia wakati tunajua fika kuwa pesa alizokopa alizipeleka kujengea shule, kununulia vitabu, kukarabati ofisi za shule? N.k
.....
..
Nawapongeza sana Uongozi wa CCM kuendelea kumuweka kwenye "mabano EL" hasa kipindi hiki cha kujipanga na kutangaza nia.
Wenu.
Tume ya katiba,
Mwanachama mtiifu wa ADC
RIP Komba taifa litakukumbuka,
WanaCCM wenzako watakulilia,
Wapiga kura wako watakosa utumishi wako.
Natamani wajitokeze wasanii wakutungie nyimbo kama ulivyofanya wakati wa Mwl Nyerere.
vyombo vya habari vimesema marehemu komba,ameacha mjane mmoja na watoto 11,je wote ni mama mmoja?
kama hakujiombea mwenyewe wakati akiwa hai duniani ndo imekula kwake hiyo. tupoteze mda wetu kumwombea dhulumati ambaye alitumia mda wake kuzini na vitoto vyetu, kutukana wazee wetu, kutuibia mali zetu, kusimamia tukidhalilishwa na vyombo vya dola na kutunanga, kupanga kuingia msituni ili kutuua, kuzuia utaratibu wananchi waliouchagua wa kuwaongoza nk nkSasa unataka kutuaminisha nini au ndio mwendelezo wa unafiki wa Kitanzania!
Kapt. Komba ameisaidia sana ccm na hilo linajulikana, EL yuko kwenye list ya waliokuwa wanategemea mwendelezo wa msaada wa Komba kama wengine walivyokwisha kufaidika.
Sasa hao waliokwisha faidika walimsaidia vipi kumaliza hayo madeni mpaka usiwalaumu na umlaumu mfaidika mtarajiwa!?
Kweli chama yake wangelikuwa waungwana kwenye issue kama ya Tegeta escrow naye akajipatia angalau tubilioni tuwili si angelimaliza au hata kupunguza kwa kiasi kikubwa hilo deni la crdb?
Cha msingi hapa sio kutumia msiba wa mtu kuendeleza propaganda bali sote tuiombee roho yake ipate amani bila kujali kuwa alikuwa 'mpinzani' wa rasimu ya Mzee Warioba.
wanandugu,
Awali ya yote nitoe pole zangu za dhati kabisa kwa Familia, Ndugu, Jamaa, Wapenzi, na Marafiki wote Wa Marehemu Kaptain John Komba. Kimsingi Komba ni Jirani yangu kabisa hapa Dar es salaam, Familia yake hasa mke wake na watoto ni Watu wazuri mno.Wanaongea na vizuri sana watoto wote wakike na wakiume hasa wale wanaoishi maeneo ya Goba ni Marafiki zangu wakubwa. Mke wake ni mfano wa akina Mama wenye Heshima mno.Ni mama Wa mfano wa kuigwa..
Baada ya utangulizi huu ngoja nirudi kwenye Mada, Mimi binafsi nilianza kumjua Marehemu Komba Vizuri sana Baada ya kutunga Nyimbo nyingi na Nzuri za kuomboleza kifo cha Hayati Mwalimu JK Nyerere, Hazikuwa nyimbo nzuri tu ila zilitungwa haraka sana na kusambazwa maredioni haraka sana kiasi kwamba kila mtu alishangaa.
Kuna huu utamaduni kuwa mtu akishafariki, Watu husahau mabaya yake na Kuona Kama Kuyazungumza matendo yake(Mabaya) au mambo aliyofanya akiwa hai ni kumsema vibaya marehemu huu utamaduni inabidi ufike mwisho sasa.Hapa Tuache Unafiki.
Mbona Kama ni mabaya tulizungumza ya Iddi Amini kwani Hakuwa na Mazuri aliyofanya kwa watu wa uganda?? Leo Nitajadili Matendo ya Marehemu Komba Enzi za uhai wake Ambayo Yalikuwa ni Mazuri mno Kwa Chama Chake(CCM) lakini yakiumiza umma wa Watanzania.
Marehemu Captain John Komba akichangia Bungeni wakati wa Bunge Maalumu la Katiba alidai, Serikali Tatu zikipitishwa ataingia msituni kudai Serikali mbili.Wabunge wa CCM na baadhi ya wabunge wengine ambao miongoni mwao kuna viongozi wa Dini,Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Wanasheria,Waziri mkuu na Mawaziri akiwepo waziri wa Ulinzi ambaye anaongoza wizara inayosimamia Majeshi na vikosi vyote pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani hawakutoa kauli yoyote ya kukemea kauli hiyo na wamekubaliana na msimamo huo wa Captain Komba Kwa maana alikuwa akisaidia Mkakati wa CCM kupitisha Rasimu ya Serikali 2 kwa Njia yeyote.Maana yake ilikuwa ni nini? kama ni halali kuingia Msituni kudai serikali mbili basi ni halali kuidai Tanganyika na Zanzibar yenye mamlaka kamili kupitia msituni au kwa gharama yoyote, Ndio Funzo alilokuwa anatufundisha Tuliokuwa tunataka serikali 3.
Kumshambulia Dr.Salim Ahmed Salim, Mzee Butiku, Mzee Warioba Kisa tu wako na mtizamo na Muundo wa Serikali 3 ni kumdhalilisha Mwl.Nyerere.Huwezi kumtukana Dr.Salim Ahmed Salim na Mzee Butiku (Viongozi wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere) halafu uwe unamuenzi na kumuheshimu Mwalimu Nyerere(Hapa nawaasa Wanasiasa wetu wajifunze kujadili inssues(HOJA) sio watu.Marehemu michango yake mingi alijikita Kujadili watu.
Kuishambulia CHADEMA Kwenye Suala La Migogoro ya ELIMU
Akichangia bungeni June 2013, Marehemu Capt Komba alisema CHADEMA ni chama kinachochangia kushuka kwa elimu kwa sababu kimekuwa kikienda vyuoni na kuhamasisha migomo na mandamano na kufanya wanafunzi washindwe kusoma kwa utulivu.Alieenda mbali zaidi kwa kuwaita CHADEMA kuwa wana kisebusebu na kiroho pabo na ndiyo maana jimboni kwake Mbinga na Nyasa CHADEMA wamekataliwa.
Hapa kwa mtu makini unaelewa nini? Huu ulikuwa ni muendelezo wa kuacha ku deal na genuine causes za matatizo ka kutafuta scapegoats(Yaan Kutafuta mtu au Kundi la kubebesha lawama). Something was very wrong somewhere!
Kimsingi Wanafunzi wakiandamana lazima kuna sababu, na sababu nyingi zinasababishwa na serikali ya CCM, Mfano Kuchelewa kulipa pesa za mikopo, Mazingira mabovu ya kusomea na Kadhalika, Sasa Marehemu badala ya kushungulika na Chanzo cha tatizo akaishambulia Chadema, Aliendeleza Ukada wake.
Nitaendelea Baadaye…….
hakika nyimbo zake zilikuwa nguvu fulani ktk media au ktk kampaign namaanisha HAMASISHA / chuki sio mahali pale
kama hakujiombea mwenyewe wakati akiwa hai duniani ndo imekula kwake hiyo. tupoteze mda wetu kumwombea dhulumati ambaye alitumia mda wake kuzini na vitoto vyetu, kutukana wazee wetu, kutuibia mali zetu, kusimamia tukidhalilishwa na vyombo vya dola na kutunanga, kupanga kuingia msituni ili kutuua, kuzuia utaratibu wananchi waliouchagua wa kuwaongoza nk nk
no way, roho yake haiwezi kupata amani kamwe, bali vurugu na mateso makuu huko kuzimu.
Eee Mungu Mkuu mlipie huyu dhalimu kadri alivotutendea sisi binaadam wenzie ambao nasi ni viumbe na waja wako.
power corrupts, absolute power corrupts absolutely.Nashukuru kwa maoni yako. Personally, nilianza kumjua John Komba wakati wa vita ya Kagera mwaka 1978. Kwa tuliokuwepo then, naomba tumkumbuke kwa uwezo wake wa kuhamasisha katika mambo ya kitaifa kama alivyokuwa akifanya wakati ule. taifa zima tulikuwa pamoja kumtoa nduli Amin. Alitunga nyimbo zilizowahamasisha watu na askari sawia. Kwa hilo, nitamkumbuka.
Nafikiri baadaye aliharibika kwa kushawishika kulitumikia tumbo lake, akatumia kipaji chake alichopewa na muumba kushiriki kuwakandamiza wanyonge na kutumikia mfumo wa kifisadi. Polepole, watu wameacha kumheshimu na hawataweza kumuenzi kwa yale mema aliyofanya, kwa sababu ya msimamo wake kutetea maovu siku zake za mwisho.
Lakini binadamu ndivyo tulivyo. Baya moja linafuta mema kumi. Buriani John damian Komba.
Nape mbona hasemi akamsalimia baba yake wa kambo mzee Nnauye