TANZIA Captain John Komba afariki Dunia

TANZIA Captain John Komba afariki Dunia

​
Taarifa zilizonukuliwa na vyombo vya habari ni kuwa Kapt. John Komba amefariki kutokana na shinikizo la damu (i.e Immediate cause), lakini kwa wale waliofuatilia kwa makini mwenendo hadi mauti ya mwanamuziki, kipenzi cha watanzania, kada na mwanachama mwaminifu wa CCM marehemu Komba waatakubaliana nami kuwa chanzo cha hilo li presha kilikuwa ni kuzidiwa kwa madeni, madeni yaliyopelekea kupigwa mnada nyumba zake na mali zake mbali mbali.

Labda alikua kipenzi chako wewe... do NOT generalize
 
You got me wrong my brother! Polisi wanachofanya ni ukatili na unyama wa hali ya juu na Premier Pinda kuagiza wananchi tupigwe ni kauli inayokinzana na utawala wa sheria(ni kauli ambayo inaweza sikika kwenye nchi ambayo haina utawala wa sheria tu) and to set the record straight nilipambana against Pinda kwa kauli yake, Mauaji ya Albino yananisikitisha na kunihuzunisha kuliko! jaribu kupitia comments zangu kwenye threads zilizotoa habari za mauji ya Albino utajua ukweli, Tafuta comments zangu kuhusu mauaji ya Mwangosi huwa sikai upande wa madhalimu yanayomwaga damu ya watu wasio na hatia ili kulinda madaraka yao ambayo watayaacha na kurudi mavumbini(maana HAKIka wote tutakufa na Mungu atatuhukumu kwa matendo yetu bila kuangalia huyu alikuwa kiongozi au muongozwa)!, Hapo mwisho umeniweka kwenye kundi la watawala wa sasa which is absolutely wrong! I'm also a victim of on going brutality but not letting my condition of being oppressed affect my position of humanity na kufurahia kifo cha mtu

umeandika vema ila hapo mwisho kwenye red ukaharibu kama vile komba alivoimba vema ila mwisho wa maisha yake akaharibu kwa kumtukana mzee tunayemheshimu sana Warioba.

just to remind you....uvumilivu nao una mwisho wake pia. we are now tired of turning the other chick, Alisema warioba afe na ma ccm yaliyokuwa bungeni yakacheka na kumpigia makofi. Mtu anayekutamkia hadharani kuwa ufe ni kuwa keshajenga nia ya kukuondoa na akikupatia nafas hata sumu atakulisha. sasa Mungu katupigania wanyonge tusiokuwa na virungu vya polisi, kamtuliza dhalimu kabla hajatutuliza.....

tuna kila haki ya kushangilia. Mbona Idd Amin alipokufa tulishangilia? na ni vile alikimbia nia yetu ilikuwa kummalizia pale pale mtukula. kwa nini kwa idd amin iwe sawa lakin kwa huyu dhalimu isiwe?!!!
 
Umesema sahihi kabisa CCM wana matatizo kibao. Hoja yangu kubwa je tuna mbadala? Kwa upande wangu naona hatuna mbadala.

ni haki yaki yako. this is a democratic country japokuwa mafedhuli mnaikandamiza demokrasia.

lakin mwisho wa siku mafisadi mtaondoka tu....no way!!
 
​Swali ninalojiuliza hadi sasa ni kuwa “Wako wapi Marafiki wa Lowasa” kumsaidia huyu komba hadi adhalilike kiasi kile? Kwanini afe kwa kuzidiwa na madeni wakati rafiki yake mkuu anagawa rushw kla kukicha? Kwa nini ilishindikana kumsaidia wakati tunajua fika kuwa pesa alizokopa alizipeleka kujengea shule, kununulia vitabu, kukarabati ofisi za shule? N.k
.....
..
Nawapongeza sana Uongozi wa CCM kuendelea kumuweka kwenye "mabano EL" hasa kipindi hiki cha kujipanga na kutangaza nia.

Wenu.

Tume ya katiba,

Mwanachama mtiifu wa ADC
Sasa unataka kutuaminisha nini au ndio mwendelezo wa unafiki wa Kitanzania!
Kapt. Komba ameisaidia sana ccm na hilo linajulikana, EL yuko kwenye list ya waliokuwa wanategemea mwendelezo wa msaada wa Komba kama wengine walivyokwisha kufaidika.
Sasa hao waliokwisha faidika walimsaidia vipi kumaliza hayo madeni mpaka usiwalaumu na umlaumu mfaidika mtarajiwa!?
Kweli chama yake wangelikuwa waungwana kwenye issue kama ya Tegeta escrow naye akajipatia angalau tubilioni tuwili si angelimaliza au hata kupunguza kwa kiasi kikubwa hilo deni la crdb?
Cha msingi hapa sio kutumia msiba wa mtu kuendeleza propaganda bali sote tuiombee roho yake ipate amani bila kujali kuwa alikuwa 'mpinzani' wa rasimu ya Mzee Warioba.

RIP Komba taifa litakukumbuka,
WanaCCM wenzako watakulilia,
Wapiga kura wako watakosa utumishi wako.

Natamani wajitokeze wasanii wakutungie nyimbo kama ulivyofanya wakati wa Mwl Nyerere.
 
RIP Komba taifa litakukumbuka,
WanaCCM wenzako watakulilia,
Wapiga kura wako watakosa utumishi wako.

Natamani wajitokeze wasanii wakutungie nyimbo kama ulivyofanya wakati wa Mwl Nyerere.

Itakuwa kweli hajaandaaga wimbo wake..........kha haaaaaaaa!!!!!!
 
wanandugu,

Awali ya yote nitoe pole zangu za dhati kabisa kwa Familia, Ndugu, Jamaa, Wapenzi, na Marafiki wote Wa Marehemu Kaptain John Komba. Kimsingi Komba ni Jirani yangu kabisa hapa Dar es salaam, Familia yake hasa mke wake na watoto ni Watu wazuri mno.Wanaongea na vizuri sana watoto wote wakike na wakiume hasa wale wanaoishi maeneo ya Goba ni Marafiki zangu wakubwa. Mke wake ni mfano wa akina Mama wenye Heshima mno.Ni mama Wa mfano wa kuigwa..
Baada ya utangulizi huu ngoja nirudi kwenye Mada, Mimi binafsi nilianza kumjua Marehemu Komba Vizuri sana Baada ya kutunga Nyimbo nyingi na Nzuri za kuomboleza kifo cha Hayati Mwalimu JK Nyerere, Hazikuwa nyimbo nzuri tu ila zilitungwa haraka sana na kusambazwa maredioni haraka sana kiasi kwamba kila mtu alishangaa.
Kuna huu utamaduni kuwa mtu akishafariki, Watu husahau mabaya yake na Kuona Kama Kuyazungumza matendo yake(Mabaya) au mambo aliyofanya akiwa hai ni kumsema vibaya marehemu huu utamaduni inabidi ufike mwisho sasa.Hapa Tuache Unafiki.
Mbona Kama ni mabaya tulizungumza ya Iddi Amini kwani Hakuwa na Mazuri aliyofanya kwa watu wa uganda?? Leo Nitajadili Matendo ya Marehemu Komba Enzi za uhai wake Ambayo Yalikuwa ni Mazuri mno Kwa Chama Chake(CCM) lakini yakiumiza umma wa Watanzania.

Marehemu Captain John Komba akichangia Bungeni wakati wa Bunge Maalumu la Katiba alidai, Serikali Tatu zikipitishwa ataingia msituni kudai Serikali mbili.Wabunge wa CCM na baadhi ya wabunge wengine ambao miongoni mwao kuna viongozi wa Dini,Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Wanasheria,Waziri mkuu na Mawaziri akiwepo waziri wa Ulinzi ambaye anaongoza wizara inayosimamia Majeshi na vikosi vyote pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani hawakutoa kauli yoyote ya kukemea kauli hiyo na wamekubaliana na msimamo huo wa Captain Komba Kwa maana alikuwa akisaidia Mkakati wa CCM kupitisha Rasimu ya Serikali 2 kwa Njia yeyote.Maana yake ilikuwa ni nini? kama ni halali kuingia Msituni kudai serikali mbili basi ni halali kuidai Tanganyika na Zanzibar yenye mamlaka kamili kupitia msituni au kwa gharama yoyote, Ndio Funzo alilokuwa anatufundisha Tuliokuwa tunataka serikali 3.

Kumshambulia Dr.Salim Ahmed Salim, Mzee Butiku, Mzee Warioba Kisa tu wako na mtizamo na Muundo wa Serikali 3 ni kumdhalilisha Mwl.Nyerere.Huwezi kumtukana Dr.Salim Ahmed Salim na Mzee Butiku (Viongozi wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere) halafu uwe unamuenzi na kumuheshimu Mwalimu Nyerere(Hapa nawaasa Wanasiasa wetu wajifunze kujadili inssues(HOJA) sio watu.Marehemu michango yake mingi alijikita Kujadili watu.

Kuishambulia CHADEMA Kwenye Suala La Migogoro ya ELIMU
Akichangia bungeni June 2013, Marehemu Capt Komba alisema CHADEMA ni chama kinachochangia kushuka kwa elimu kwa sababu kimekuwa kikienda vyuoni na kuhamasisha migomo na mandamano na kufanya wanafunzi washindwe kusoma kwa utulivu.Alieenda mbali zaidi kwa kuwaita CHADEMA kuwa wana kisebusebu na kiroho pabo na ndiyo maana jimboni kwake Mbinga na Nyasa CHADEMA wamekataliwa.
Hapa kwa mtu makini unaelewa nini? Huu ulikuwa ni muendelezo wa kuacha ku deal na genuine causes za matatizo ka kutafuta scapegoats(Yaan Kutafuta mtu au Kundi la kubebesha lawama). Something was very wrong somewhere!
Kimsingi Wanafunzi wakiandamana lazima kuna sababu, na sababu nyingi zinasababishwa na serikali ya CCM, Mfano Kuchelewa kulipa pesa za mikopo, Mazingira mabovu ya kusomea na Kadhalika, Sasa Marehemu badala ya kushungulika na Chanzo cha tatizo akaishambulia Chadema, Aliendeleza Ukada wake.

Nitaendelea Baadaye…….
 
Last edited by a moderator:
Sasa unataka kutuaminisha nini au ndio mwendelezo wa unafiki wa Kitanzania!
Kapt. Komba ameisaidia sana ccm na hilo linajulikana, EL yuko kwenye list ya waliokuwa wanategemea mwendelezo wa msaada wa Komba kama wengine walivyokwisha kufaidika.
Sasa hao waliokwisha faidika walimsaidia vipi kumaliza hayo madeni mpaka usiwalaumu na umlaumu mfaidika mtarajiwa!?
Kweli chama yake wangelikuwa waungwana kwenye issue kama ya Tegeta escrow naye akajipatia angalau tubilioni tuwili si angelimaliza au hata kupunguza kwa kiasi kikubwa hilo deni la crdb?
Cha msingi hapa sio kutumia msiba wa mtu kuendeleza propaganda bali sote tuiombee roho yake ipate amani bila kujali kuwa alikuwa 'mpinzani' wa rasimu ya Mzee Warioba.

kama hakujiombea mwenyewe wakati akiwa hai duniani ndo imekula kwake hiyo. tupoteze mda wetu kumwombea dhulumati ambaye alitumia mda wake kuzini na vitoto vyetu, kutukana wazee wetu, kutuibia mali zetu, kusimamia tukidhalilishwa na vyombo vya dola na kutunanga, kupanga kuingia msituni ili kutuua, kuzuia utaratibu wananchi waliouchagua wa kuwaongoza nk nk

no way, roho yake haiwezi kupata amani kamwe, bali vurugu na mateso makuu huko kuzimu.

Eee Mungu Mkuu mlipie huyu dhalimu kadri alivotutendea sisi binaadam wenzie ambao nasi ni viumbe na waja wako.
 
wanandugu,

Awali ya yote nitoe pole zangu za dhati kabisa kwa Familia, Ndugu, Jamaa, Wapenzi, na Marafiki wote Wa Marehemu Kaptain John Komba. Kimsingi Komba ni Jirani yangu kabisa hapa Dar es salaam, Familia yake hasa mke wake na watoto ni Watu wazuri mno.Wanaongea na vizuri sana watoto wote wakike na wakiume hasa wale wanaoishi maeneo ya Goba ni Marafiki zangu wakubwa. Mke wake ni mfano wa akina Mama wenye Heshima mno.Ni mama Wa mfano wa kuigwa..
Baada ya utangulizi huu ngoja nirudi kwenye Mada, Mimi binafsi nilianza kumjua Marehemu Komba Vizuri sana Baada ya kutunga Nyimbo nyingi na Nzuri za kuomboleza kifo cha Hayati Mwalimu JK Nyerere, Hazikuwa nyimbo nzuri tu ila zilitungwa haraka sana na kusambazwa maredioni haraka sana kiasi kwamba kila mtu alishangaa.
Kuna huu utamaduni kuwa mtu akishafariki, Watu husahau mabaya yake na Kuona Kama Kuyazungumza matendo yake(Mabaya) au mambo aliyofanya akiwa hai ni kumsema vibaya marehemu huu utamaduni inabidi ufike mwisho sasa.Hapa Tuache Unafiki.
Mbona Kama ni mabaya tulizungumza ya Iddi Amini kwani Hakuwa na Mazuri aliyofanya kwa watu wa uganda?? Leo Nitajadili Matendo ya Marehemu Komba Enzi za uhai wake Ambayo Yalikuwa ni Mazuri mno Kwa Chama Chake(CCM) lakini yakiumiza umma wa Watanzania.

Marehemu Captain John Komba akichangia Bungeni wakati wa Bunge Maalumu la Katiba alidai, Serikali Tatu zikipitishwa ataingia msituni kudai Serikali mbili.Wabunge wa CCM na baadhi ya wabunge wengine ambao miongoni mwao kuna viongozi wa Dini,Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Wanasheria,Waziri mkuu na Mawaziri akiwepo waziri wa Ulinzi ambaye anaongoza wizara inayosimamia Majeshi na vikosi vyote pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani hawakutoa kauli yoyote ya kukemea kauli hiyo na wamekubaliana na msimamo huo wa Captain Komba Kwa maana alikuwa akisaidia Mkakati wa CCM kupitisha Rasimu ya Serikali 2 kwa Njia yeyote.Maana yake ilikuwa ni nini? kama ni halali kuingia Msituni kudai serikali mbili basi ni halali kuidai Tanganyika na Zanzibar yenye mamlaka kamili kupitia msituni au kwa gharama yoyote, Ndio Funzo alilokuwa anatufundisha Tuliokuwa tunataka serikali 3.

Kumshambulia Dr.Salim Ahmed Salim, Mzee Butiku, Mzee Warioba Kisa tu wako na mtizamo na Muundo wa Serikali 3 ni kumdhalilisha Mwl.Nyerere.Huwezi kumtukana Dr.Salim Ahmed Salim na Mzee Butiku (Viongozi wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere) halafu uwe unamuenzi na kumuheshimu Mwalimu Nyerere(Hapa nawaasa Wanasiasa wetu wajifunze kujadili inssues(HOJA) sio watu.Marehemu michango yake mingi alijikita Kujadili watu.

Kuishambulia CHADEMA Kwenye Suala La Migogoro ya ELIMU
Akichangia bungeni June 2013, Marehemu Capt Komba alisema CHADEMA ni chama kinachochangia kushuka kwa elimu kwa sababu kimekuwa kikienda vyuoni na kuhamasisha migomo na mandamano na kufanya wanafunzi washindwe kusoma kwa utulivu.Alieenda mbali zaidi kwa kuwaita CHADEMA kuwa wana kisebusebu na kiroho pabo na ndiyo maana jimboni kwake Mbinga na Nyasa CHADEMA wamekataliwa.
Hapa kwa mtu makini unaelewa nini? Huu ulikuwa ni muendelezo wa kuacha ku deal na genuine causes za matatizo ka kutafuta scapegoats(Yaan Kutafuta mtu au Kundi la kubebesha lawama). Something was very wrong somewhere!
Kimsingi Wanafunzi wakiandamana lazima kuna sababu, na sababu nyingi zinasababishwa na serikali ya CCM, Mfano Kuchelewa kulipa pesa za mikopo, Mazingira mabovu ya kusomea na Kadhalika, Sasa Marehemu badala ya kushungulika na Chanzo cha tatizo akaishambulia Chadema, Aliendeleza Ukada wake.

Nitaendelea Baadaye…….

Nashukuru kwa maoni yako. Personally, nilianza kumjua John Komba wakati wa vita ya Kagera mwaka 1978. Kwa tuliokuwepo then, naomba tumkumbuke kwa uwezo wake wa kuhamasisha katika mambo ya kitaifa kama alivyokuwa akifanya wakati ule. taifa zima tulikuwa pamoja kumtoa nduli Amin. Alitunga nyimbo zilizowahamasisha watu na askari sawia. Kwa hilo, nitamkumbuka.

Nafikiri baadaye aliharibika kwa kushawishika kulitumikia tumbo lake, akatumia kipaji chake alichopewa na muumba kushiriki kuwakandamiza wanyonge na kutumikia mfumo wa kifisadi. Polepole, watu wameacha kumheshimu na hawataweza kumuenzi kwa yale mema aliyofanya, kwa sababu ya msimamo wake kutetea maovu siku zake za mwisho.

Lakini binadamu ndivyo tulivyo. Baya moja linafuta mema kumi. Buriani John damian Komba.
 
Last edited by a moderator:
Dar es Salaam. Msiba wa Mbunge wa Mbinga
Magharibi, Kapteni John Komba jana uligeuka
uwanja wa siasa, baada ya makada wa CCM
wanaotajwa kugombea urais pamoja na wapambe
wao kupigana vikumbo na kurushiana vijembe,
ikiwa na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Ilikuwa kama walijipanga kwani kila mgombea
aliyekuwa anafika katika msiba huo alionekana
kuwa na wapambe waliompokea, kumpeleka kutoa
pole kwa wafiwa na kumuonyesha eneo la kukaa.
Ukiacha kauli mbalimbali walizotoa kumwelezea
marehemu Komba (61), wapambe wa wagombea
hao walionekana mara kwa mara kuwa karibu nao
wakizungumza, hali iliyoonyesha kuwa kila kundi
lilitaka mgombea wao kuonyesha uwepo wake.
Waliohudhuria
Wanaotajwa kuutaka urais ambao walihudhuria
msiba wa mbunge huyo uliotokea juzi jioni ni
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja,
Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi,
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, wote
kutoka CCM, pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema,
Dk Willibroad Slaa.
Wapiga picha na Membe
Membe ndiyo alikuwa wa kwanza kufika nyumbani
kwa marehemu eneo la Mbezi Tangi Bovu na baada
ya muda aliwasili Rais Jakaya Kikwete na kukaa
naye.
Mara baada ya Rais Kikwete kuondoka, Membe
alilakiwa na kundi kubwa la makada wa CCM ambao
mbali na kumsalimia walimvuta pembeni na kuomba
kupiga naye picha huku wakisika wakisema kuwa
“Tunataka kupiga picha na mheshimiwa rais”.
Watu hao ambao walikuwa wakiongozwa na
Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage ambaye
hata hivyo hakupiga picha na waziri huyo, walisema
kuwa kama mambo yakienda vyema, Membe
anaweza kuwa rais na hata alipokuwa akiondoka
walimsindikiza hadi kwenye gari lake.
Vijana na Nchimbi, Ngeleja
Ukiacha Dk Nchimbi ambaye alikuwa akizongwa
zaidi na vijana wa CCM, kivutio kingine kilikuwa
kwa Ngeleja ambaye mara kwa mara alikuwa
akizungukwa na vijana waliokuwa wakimuuliza
maswali mbalimbali, hasa kuhusu sakata la Akaunti
ya Tegeta Escrow.
Ngeleja pamoja na aliyekuwa Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka walipata mgawo wa fedha kutoka katika
akaunti hiyo na tayari wamehojiwa na Kamati Ndogo
ya Maadili ya CCM, huku Ngeleja akisubiri kesho
kuhojiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma ambayo tayari imeshamuhoji Profesa
Tibaijuka.
“Kwa sasa siwezi kusema chochote. Chama kilitupa
adhabu (ya kuanza kampeni za urais mapema),
ninaiheshimu adhabu hiyo na ninasubiri tamko la
chama na hapo ndiyo nitakuwa na mengi ya
kusema,” aliwajibu Ngeleja.
Mwigulu na wanahabari
Kiongozi mwingine aliyekuwa kivutio ni Mwigulu
Nchemba kwani kila baada ya muda aliitwa na
makada wa chama hicho katika makundi na
kuonekana wakizungumza mambo mbalimbali.
Nchemba ambaye hivi karibuni ziara zake za
mikoani zilisitishwa na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana kwa maelezo kuwa hazikuwa
na baraka za chama hicho na zililenga kujitangaza,
ndiye kiongozi aliyeongoza kwa kuzungumza na
vyombo vya habari katika msiba huo.
Katika muda wa saa tano aliokaa katika eneo hilo
alizungumza na vyombo vya habari zaidi ya mara
tano, ikiwa ni mara nyingi kuliko kiongozi yeyote
aliyefika katika msiba huo.
Lowassa azima muziki
Kati ya viongozi waliokuwa kivutio zaidi ukiacha Dk
Slaa, ni Lowassa ambaye alifika katika msiba huo
saa 7:30 mchana ikiwa ni nusu saa baada ya
walinzi wake kufika.
Mara baada ya kufika aliwapa pole wafiwa na
kwenda kukaa eneo lililotengwa kwa ajili ya
viongozi wa Serikali karibu na Mbunge wa Kigoma
Mjini, Peter Serukamba na Ngeleja, na mara kadhaa
alifuatwa na makada wa chama hicho na viongozi
mbalimbali na kuzungumza naye.
Wakati akizungumza na vyombo vya habari, muziki
uliokuwa ukipigwa iliamuliwa uzimwe na mmoja wa
waongozaji wa msiba huo kwa maelezo kuwa waziri
huyo wa zamani na mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama alikuwa akizungumza.
Dk Slaa na walinzi
Mara baada ya Lowassa kuondoka eneo hilo, muda
mfupi baadaye aliwasili Dk Slaa akiwa na walinzi
watano wenye miraba minne wakiwa wamevaa suti
nyeusi na miwani nyeusi.
Kuwasili kwa kiongozi huyo wa Chadema kuliibua
minong’ono ya hapa na pale kutokana na walinzi
waliokuwa wamemzunguka ambao hawakumpa mtu
yeyote nafasi ya kumsogelea.
Msafara wa magari manne ya Dk Slaa ambaye
anatajwa kuwa miongoni mwa wanaotajwa kuwania
urais ndani ya Ukawa, yalikuwa yamepambwa na
bendera za Chadema tofauti na viongozi wa CCM
waliofika eneo hilo. source gazetii la mwananchi
 
hakika nyimbo zake zilikuwa nguvu fulani ktk media au ktk kampaign namaanisha HAMASISHA / chuki sio mahali pale

Yah right ...................... you were carried away with CCM propaganda that's why you thought you were not alone!! Yes in did you were not alone ....................... that's PROPAGANDA AT ITS BEST!! Work up dude!!
 
Tarehe na siku ambayo kamati kuu ya CCM ilikaa kwa ajili ya kuwajadili wagombeo waliokuwa kifungoni Mh. Lowassa nae alikuwa na kikao chako cha Siri kilichohusisha wajumbe wapatao nane wa kamati kuu ambao hawakuweza kuhudhuria kikao cha kamati kuu.

Moja Kati ya wajumbe waliohudhuria alikuwa Marehemu Capt. Komba. Wakati kikao cha kamati kuu kinaendelea ndipo wajumbe wa Kamati Kuu (CC) walibaini Lowassa anaendesha kikao cha Siri na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu. Mmoja Kati ya wajumbe wa kamati kuu alipewa jukumu la kuwapigia simu wajumbe wote ambao hawakuwepo kikaoni kuwauliza sababu ya kutokuwepo. Wajumbe wote waliopigiwa simu hawakuwa na majibu yaliyodhisha.

Taarifa zinadai kwamba Marehemu Komba alivyobanwa baada ya kupigiwa simu na mjumbe wa Kamati Kuu (CC) pressure ikapanda kitu kilichosababisha mauti kumfika.

Huyu jamaa ni hatari sanaa na ana mtandao mkubwa alisikika mjumbe mmoja wa kamati kuu!!

Kuna taarifa za kiusalama zaidi naogopa kuziweza kwa sasa nitarudi baadae kuwapa update kuhusu nini kinaendelea ili kumshughurikia lowassa. Na inasemekana Kamati kuu ilishindwa kufanya maamuzi ili kujua maamuzi yaliyofikiwa kwenye kikao cha Lowassa alichokuwa anafanya
 
Kuna kitu sijaelewa huu wimbo wa nape na wenzake wanasema mzee mwadilifu katutoka?yawni komba muadilifu?
 
kama hakujiombea mwenyewe wakati akiwa hai duniani ndo imekula kwake hiyo. tupoteze mda wetu kumwombea dhulumati ambaye alitumia mda wake kuzini na vitoto vyetu, kutukana wazee wetu, kutuibia mali zetu, kusimamia tukidhalilishwa na vyombo vya dola na kutunanga, kupanga kuingia msituni ili kutuua, kuzuia utaratibu wananchi waliouchagua wa kuwaongoza nk nk

no way, roho yake haiwezi kupata amani kamwe, bali vurugu na mateso makuu huko kuzimu.

Eee Mungu Mkuu mlipie huyu dhalimu kadri alivotutendea sisi binaadam wenzie ambao nasi ni viumbe na waja wako.

hili neno hili
 
Yaani huu wimbo wa nape unanichefua mpaka basi ...eti komba ni muadilifu..nape mavi nini
 
Nashukuru kwa maoni yako. Personally, nilianza kumjua John Komba wakati wa vita ya Kagera mwaka 1978. Kwa tuliokuwepo then, naomba tumkumbuke kwa uwezo wake wa kuhamasisha katika mambo ya kitaifa kama alivyokuwa akifanya wakati ule. taifa zima tulikuwa pamoja kumtoa nduli Amin. Alitunga nyimbo zilizowahamasisha watu na askari sawia. Kwa hilo, nitamkumbuka.

Nafikiri baadaye aliharibika kwa kushawishika kulitumikia tumbo lake, akatumia kipaji chake alichopewa na muumba kushiriki kuwakandamiza wanyonge na kutumikia mfumo wa kifisadi. Polepole, watu wameacha kumheshimu na hawataweza kumuenzi kwa yale mema aliyofanya, kwa sababu ya msimamo wake kutetea maovu siku zake za mwisho.

Lakini binadamu ndivyo tulivyo. Baya moja linafuta mema kumi. Buriani John damian Komba.
power corrupts, absolute power corrupts absolutely.

mwanzoni alikuwa Bin Adam, baaadaye Mungu akampa pesa na madaraka ili avitumie kuwasaidia Bin Adam wenzake, akamgeuka Mungu akaamua kuvitumia hivyo kugandamiza wanyonge, this is typical of mafisad na madhulumati wengi waliopo madarakani sasa. majitu yametudhulumu mpaka yamefikia hatua yanajitangaza yenyewe kuwa ni machatu yenye makengeneza yaliyo hodari kuona wapi zilipo mali za umma na kuzichota kiujanjajanja kwenda kuzifukia huko uswiz kwa wazungu matajiri. wakati huo mama zetu wanadhalilika kwa kuzalishwa kwa vibatari na mifuko ya rambo huko vijijini.

Mungu atatenda tu Inshaallah!!!
 
Back
Top Bottom