wanandugu,
Awali ya yote nitoe pole zangu za dhati kabisa kwa Familia, Ndugu, Jamaa, Wapenzi, na Marafiki wote Wa Marehemu Kaptain John Komba. Kimsingi Komba ni Jirani yangu kabisa hapa Dar es salaam, Familia yake hasa mke wake na watoto ni Watu wazuri mno.Wanaongea na vizuri sana watoto wote wakike na wakiume hasa wale wanaoishi maeneo ya Goba ni Marafiki zangu wakubwa. Mke wake ni mfano wa akina Mama wenye Heshima mno.Ni mama Wa mfano wa kuigwa..
Baada ya utangulizi huu ngoja nirudi kwenye Mada, Mimi binafsi nilianza kumjua Marehemu Komba Vizuri sana Baada ya kutunga Nyimbo nyingi na Nzuri za kuomboleza kifo cha Hayati Mwalimu JK Nyerere, Hazikuwa nyimbo nzuri tu ila zilitungwa haraka sana na kusambazwa maredioni haraka sana kiasi kwamba kila mtu alishangaa.
Kuna huu utamaduni kuwa mtu akishafariki, Watu husahau mabaya yake na Kuona Kama Kuyazungumza matendo yake(Mabaya) au mambo aliyofanya akiwa hai ni kumsema vibaya marehemu huu utamaduni inabidi ufike mwisho sasa.Hapa Tuache Unafiki.
Mbona Kama ni mabaya tulizungumza ya Iddi Amini kwani Hakuwa na Mazuri aliyofanya kwa watu wa uganda?? Leo Nitajadili Matendo ya Marehemu Komba Enzi za uhai wake Ambayo Yalikuwa ni Mazuri mno Kwa Chama Chake(CCM) lakini yakiumiza umma wa Watanzania.
Marehemu Captain John Komba akichangia Bungeni wakati wa Bunge Maalumu la Katiba alidai, Serikali Tatu zikipitishwa ataingia msituni kudai Serikali mbili.Wabunge wa CCM na baadhi ya wabunge wengine ambao miongoni mwao kuna viongozi wa Dini,Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Wanasheria,Waziri mkuu na Mawaziri akiwepo waziri wa Ulinzi ambaye anaongoza wizara inayosimamia Majeshi na vikosi vyote pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani hawakutoa kauli yoyote ya kukemea kauli hiyo na wamekubaliana na msimamo huo wa Captain Komba Kwa maana alikuwa akisaidia Mkakati wa CCM kupitisha Rasimu ya Serikali 2 kwa Njia yeyote.Maana yake ilikuwa ni nini? kama ni halali kuingia Msituni kudai serikali mbili basi ni halali kuidai Tanganyika na Zanzibar yenye mamlaka kamili kupitia msituni au kwa gharama yoyote, Ndio Funzo alilokuwa anatufundisha Tuliokuwa tunataka serikali 3.
Kumshambulia Dr.Salim Ahmed Salim, Mzee Butiku, Mzee Warioba Kisa tu wako na mtizamo na Muundo wa Serikali 3 ni kumdhalilisha Mwl.Nyerere.Huwezi kumtukana Dr.Salim Ahmed Salim na Mzee Butiku (Viongozi wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere) halafu uwe unamuenzi na kumuheshimu Mwalimu Nyerere(Hapa nawaasa Wanasiasa wetu wajifunze kujadili inssues(HOJA) sio watu.Marehemu michango yake mingi alijikita Kujadili watu.
Kuishambulia CHADEMA Kwenye Suala La Migogoro ya ELIMU
Akichangia bungeni June 2013, Marehemu Capt Komba alisema CHADEMA ni chama kinachochangia kushuka kwa elimu kwa sababu kimekuwa kikienda vyuoni na kuhamasisha migomo na mandamano na kufanya wanafunzi washindwe kusoma kwa utulivu.Alieenda mbali zaidi kwa kuwaita CHADEMA kuwa wana kisebusebu na kiroho pabo na ndiyo maana jimboni kwake Mbinga na Nyasa CHADEMA wamekataliwa.
Hapa kwa mtu makini unaelewa nini? Huu ulikuwa ni muendelezo wa kuacha ku deal na genuine causes za matatizo ka kutafuta scapegoats(Yaan Kutafuta mtu au Kundi la kubebesha lawama). Something was very wrong somewhere!
Kimsingi Wanafunzi wakiandamana lazima kuna sababu, na sababu nyingi zinasababishwa na serikali ya CCM, Mfano Kuchelewa kulipa pesa za mikopo, Mazingira mabovu ya kusomea na Kadhalika, Sasa Marehemu badala ya kushungulika na Chanzo cha tatizo akaishambulia Chadema, Aliendeleza Ukada wake.
Nitaendelea Baadaye…….