Carlos Stenio Fernandes Guimares"Carlinhos", amewasili nchini Tanzania mchana wa Leo tayari kabisa kwa kuanza kuitumikia timu yake mpya ya Yanga
Carlinhos ambaye anacheza nafasi ya Kiungo mshambuliaji, anasemekana atakuwa ni kiungo bora kabisa ambaye amewahi kucheza kwenye ardhi hii ya Tanzania
Carlinhos anatokea kwenye timu ya Interclub ya nchini Angola, ujio wake Yanga na wachezaji wengine waliosajiliwa msimu huu unawapa washabiki na wanachama wa Yanga imani kubwa kuwa msimu ujao utakuwa wa furaha kwao