Carlinhos, Kiungo fundi na bora kabisa kutoka Angola atua nchini kujiunga na Yanga

Carlinhos, Kiungo fundi na bora kabisa kutoka Angola atua nchini kujiunga na Yanga

View attachment 1547788

Carlos Stenio Fernandes Guimares"Carlinhos", amewasili nchini Tanzania mchana wa Leo tayari kabisa kwa kuanza kuitumikia timu yake mpya ya Yanga

Carlinhos ambaye anacheza nafasi ya Kiungo mshambuliaji, anasemekana atakuwa ni kiungo bora kabisa ambaye amewahi kucheza kwenye ardhi hii ya Tanzania

Carlinhos anatokea kwenye timu ya Interclub ya nchini Angola, ujio wake Yanga na wachezaji wengine waliosajiliwa msimu huu unawapa washabiki na wanachama wa Yanga imani kubwa kuwa msimu ujao utakuwa wa furaha kwao
Mbona anafanana na yule mcheza show wa Awilo Longomba
 
Kweli jamani hata kama hela hutafuti wewe huwezi kuitumia rafu kiasi hiki

Wananchi wanachanga hela kwa ajili ya kununua wachezaji halafu kamati ya yanga inawatumia kama nauli ndugu zao walioshindwa kumudu maisha huko nchi za watu halafu wakifika huku wanadanganya mashabiki kua ni mastraiker?
 
Kumbe huna habari ooh, basi wenzio wameanzisha kituo cha kulelea wazee pale msimbazi
Aaaahh,Simba ni timu ya wahenga + wazee + kununua mechi +kubebwa na Tff,lakini mwishoni mwa msimu wahenga watuziba midomo kwa kuibuka top scores,Okwi + Boko - Kagere.Kushabikia Simba na Yanga ni Raha Sana ,kupigana vijembe,kukatishana tamaa,mchezaji mzuri kuitwa bomu,timu yangu pendwa kupambwa na media ,kulishana matango Poli ni Jambo la kawaida, viongozi kuwahadaaa mashabiki ni kawaida tu,kazi ni kwako shabiki kutumia akili yako ipasavyo kudadavua mbovu na mbichi.
 
View attachment 1547788

Carlos Stenio Fernandes Guimares"Carlinhos", amewasili nchini Tanzania mchana wa Leo tayari kabisa kwa kuanza kuitumikia timu yake mpya ya Yanga

Carlinhos ambaye anacheza nafasi ya Kiungo mshambuliaji, anasemekana atakuwa ni kiungo bora kabisa ambaye amewahi kucheza kwenye ardhi hii ya Tanzania

Carlinhos anatokea kwenye timu ya Interclub ya nchini Angola, ujio wake Yanga na wachezaji wengine waliosajiliwa msimu huu unawapa washabiki na wanachama wa Yanga imani kubwa kuwa msimu ujao utakuwa wa furaha kwao
Ni kweli huyo ni bonge la mchezaji,lakini yanga watujibu mambo yafuatayo:
1.je hao wachezaji wote wamesajiliwa kwa matakwa ya kocha yupi,maana mpaka sasa hawana kocha mkuu
2.lugha ni moja ya changamoto kubwa sana kwenye ufundishaji,.kakati wao ni upi?
3.yanga ni klabu ambayo haina fedha,huyo kocha na hao wachezaji nani atawalipa huko mbeleni?
4.kila kitu kinafanywa na gsm,je wana back up plan,in case gsm wakijitoa ghafla?
5.muundo mzima wa klabu ya yanga hauelewi kabisa,hatujui chain of comand ya yanga ikoje,sasa kwa hali hii, urugu ikitokea miongoni mwa viongozi,nani atamrekebisha mwenzie?
 
Utopolo October 18 watachapana bakora kocha wao watamfukuza kwa kipigo cha aibu watakachopata
 
Kwa tunavyozifahamu timu za Angola ambazo zilimsajili hadi Rivaldo zisingeweza kumwacha huyo mchezaji kama angekuwa mzuri
 
Maneno maneno tu.....
Hamna hata ka clip kakuokoteza??

Yanga mnafeli sn🤔🤔

Soka la kisasa Karne hii ushahidi wa ubora wa mchezaji ni video tu
 
Aaaahh,Simba ni timu ya wahenga + wazee + kununua mechi +kubebwa na Tff,lakini mwishoni mwa msimu wahenga watuziba midomo kwa kuibuka top scores,Okwi + Boko - Kagere.Kushabikia Simba na Yanga ni Raha Sana ,kupigana vijembe,kukatishana tamaa,mchezaji mzuri kuitwa bomu,timu yangu pendwa kupambwa na media ,kulishana matango Poli ni Jambo la kawaida, viongozi kuwahadaaa mashabiki ni kawaida tu,kazi ni kwako shabiki kutumia akili yako ipasavyo kudadavua mbovu na mbichi.
Ndo maana hasa ya utani wa jadi mkuu. Washabiki wengi hawajui hili, wanabaki kuchukiana tu badala ya kutaniana
 
Back
Top Bottom