Carlinhos, Kiungo fundi na bora kabisa kutoka Angola atua nchini kujiunga na Yanga

Protect

Senior Member
Joined
Apr 4, 2020
Posts
103
Reaction score
362


Carlos Stenio Fernandes Guimares"Carlinhos", amewasili nchini Tanzania mchana wa Leo tayari kabisa kwa kuanza kuitumikia timu yake mpya ya Yanga

Carlinhos ambaye anacheza nafasi ya Kiungo mshambuliaji, anasemekana atakuwa ni kiungo bora kabisa ambaye amewahi kucheza kwenye ardhi hii ya Tanzania

Carlinhos anatokea kwenye timu ya Interclub ya nchini Angola, ujio wake Yanga na wachezaji wengine waliosajiliwa msimu huu unawapa washabiki na wanachama wa Yanga imani kubwa kuwa msimu ujao utakuwa wa furaha kwao
 
Level ya club bingwa Africa iyo team imepata mafanikio gan?? Mbona anaonekana kama sibomana mweupe
Kweni mchezaji mzuri awezi patikana timu ya kawaida?
 
Labda angekuwa anatoka timu ya Recreativo do LIBOLO angalau tungesema ina record afrika
 
Nyie Utopolo kwa mijisifa

Hiyo club INTERCLUB ipo nafasi ya 8 kati ya 16, ikiwa na point 32 nyuma ya kinara Luanda yenye point 54.

Kwa hiyo acheni kujipa matumaini makubwa kupitiliza subirini uwanjani
 
Yaaani wana mbwembwe hawa watu, ila ligi ikianza wakiona ni magarasa wanakimbilia kulaumu TFF na marefa
Inaelekea Yanga ni timu pekee kulalamikia TFF na marefa...tehteh...upo wakati msemaji wa klabu Fulani nchini alikuwa anakwenda kwenye mikutano ya waandishi wa habari akiwa amebeba tv tena basi ya chogo kuwaonyesha waandishi wa habari alichodai ni uonevu wanaofanyiwa Simba na marefa..
 
Nyie Utopolo kwa mijisifa

Hiyo club INTERCLUB ipo nafasi ya 8 kati ya 16, ikiwa na point 32 nyuma ya kinara Luanda yenye point 54.

Kwa hiyo acheni kujipa matumaini makubwa kupitiliza subirini uwanjani

Picha la Kutisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…