Case Study: Kama kwenu hakuna wafanyabiashara, komaa na shule, Biashara iwe ni Plan B, Usiige wengine bila kufikiria hali ya kwenu

Pole sana, haina uhusiano wo wote hiyo hoja yako fanya biashara ukianguka inuka tena fanya biashara iko siku mambo yatakaa sawa na ukitaka mambo yaende vizuri anza mdogo mdogo kuliko uanze juu ukianguka hutarudia kamwe ila mdogo mdogo nzuri sana haijalishi kwenu kuna waliwahi kuwepo wafanya biashara au hawakuwepo
 
Acha kuishi kwa kukaririri biashara ni ww mwenyewe utakavo amua kufanya wala sio mambo ya kuangalia ukoo ma blaa blaa

Biashara ni nidhamu ya pesa ,juhudi zako na ubunifu wako
 
Yaan mtoa mada yupo sahihi...100% sasa nikiona mtu anapingana nae aisee namuonea huruma...jaman tembeeni muone...biashara ni kitu kingine...na sio mtaji...unaweza pewa hta billions of money ukashindwa zalisha buku kama faida..
 
Ni kwel biashara ipo ndani ya damu ya mtu lakini Hapana unaweza kujifunza pia
 
Nikiangalia ukoo wetu mpaka sasa hakuna anaefanya biashara, wengi ni vitengo tu serikalini na kuajiriwa

Siwezi sema hatuna damu ya biashara, ni maamuzi tu sababu babu na bibi yangu pande zote mbili, walifanya biashara zama hizo za giza na ndio zikasomesha wazee wangu ila sasa elimu na ajira, ziliwafanya wasideal na biashara

Mrengo ambao wengi tumefata, naamini biashara usipoianza hata wao watakaofata ni ngumu kufanya

Inapaswa ianze na mmoja
 
Tujifunze tujifunze tujifunze.
Jambo kubwa sana ni mazingira. Sisi waswahili hatupendi kilimo bali biashara. Sasa mambo yamebadirika waswahili nao wanalima.
Kila kitu lazima tujifunze, global world inatupendelea kizazi cha sasa hatuna excuse! Connection ipo kiganjani.
Ukitaka bidhaa kutoka China unakpata kupitia mawadiliano.
Waafrika tupo nyuma sana kwenye kila kitu, we have to leapfrog

Siku hizi hata elimu inageuzwa kuwa biashara.
Siku hizi walimu wanafungua shule na kufanya biashara ya elimu. Wafamasia, madaktari nk nao jugeuza elimu kuwa biashara.
Tuahamasishane kufanya kila kitu wanachofanya wenzetu.
Hao wachaga wakinga nk bado sana ukilinganisha ba wahindi warabu wachina nk.
Tufanye kila kitu, utandawazi unatusaidia.
 
Nakubaliana kabisa na hoja hii, nikiwa kama mtu niliyejaribu biashara na kuangukia pua na kuamua kubakia kwenye ajira mpaka mwisho😆😆.

Biashara, kuajiriwa, kuwa mama wa nyumbani, mishen town, etc huwa viko kwenye damu, kuna watu wanaweza kuchomoka kwenye hiyo family pattern na wakafanikiwa, lakini wachache.

Hapa chini kuna link inaelezea makabila ya africa yanayofanya vizuri kwenye biashara👇 inaweza kuwa haina maelezo ya kujitosheleza lakini ukifiatilia utagundua hii kitu inakaa ktk damu zaidi.
 
Siku huzi sifa ni kutokea maisha magumu yasiyo na moja wala mbili.

Siku hizi ukimwambia mtu anatokea maisha mazuri ni kama hafurahii hivi.

Siku hizi sifa ni struggle na kutoboa.

So, waliotokea maisha mzuri, wakashikwa mikono wakaendeleza mafanikio ya familia zao, dizain kama wakikaa mbele za watu nao wanatamani waseme wali hustle hadi kufika walipo kwakua hustle ni sifa.

Kila kitu kina mwanzo wake, kila familia ina yule kijana anaeukataaga unyonge na kuvunja miiko ya ukoo. Huwa hawaeleweki kirahisi na pengine huchelewa sana kufanya mambo common kama kuoa na kuwa na familia. Kuna muda huonekana wamepotea kabisa, ila wakitobia kila mtu huwaelewa sasa. Pigeni kazi tu Mungu wetu ni mmoja, zamu yako ikifika unatoboa japo haitakua rahisi kama mtu aliyetokea maisha bora anepata miongozo huku wewe ukichimba mwenyewe kila information.

CC: Kris Lukos
 
Ktk maisha tegemea bahati Zaidi,, mengineyo yatafata.


Wapo watu wamepiga Sana kitabu shuleni lakini leo wapo mitaani wanahangaika..
 
Umejichanganya. Umetoa ushauri kama unampa mtu maskini lkn unachanganya na utajiri. Hapo kusema Wameru na Waarusha hukimbilia boda boda sasa! Acha uongo. Usiwatumia watu unaowafahamu kufanya classification and characterisation ya whole population.
 
Umejichanganya. Umetoa ushauri kama unampa mtu maskini lkn unachanganya na utajiri. Hapo kusema Wameru na Waarusha hukimbilia boda boda sasa! Acha uongo. Usiwatumia watu unaowafahamu kufanya classification and characterisation ya whole population.
Sio wote lakini biashra ya boda boda ndio imezoeleka zaidi mjini Arusha kwa wakazi wake, nakumbuka nilifika hapo mpaka 2017 hakuna bajaji ila boda boda zimejaa

And yes, wapo wengine wana biashara zingine sio wote ni boda boda lakini ni biashara ya boda boda imejizolea umaarudu zaidi
 
Sio wote lakini biashra ya boda boda ndio imezoeleka zaidi mjini Arusha kwa wakazi wake, nakumbuka nilifika hapo mpaka 2017 hakuna bajaji ila boda boda zimejaa
Wenyeji wa mahali popote wanakuwa na madaraja yote ya watu kiuchumi na kijamii. Tofauti na watu wanaohamia kutoka mahali pengine kuleta mitaji, kufanya biashara. Wanaokuja wanakuwa layer ya juu. Hata ukienda Moshi na Wilaya zake waendesha boda boda wengi na hao hao unaosema wanapeana mitaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…