Pre GE2025 CAST VOTE: Kati ya Freeman Mbowe, Tundu Lissu na John Heche nani anafaa kuiongoza CHADEMA kuelekea 2029?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Kati ya Freeman Mbowe, Tundu Lissu na John Heche nani anafaa kuiongoza CHADEMA kuelekea 2029.

  • 1. Freeman Aikael Mbowe

    Votes: 23 17.8%
  • 2. Tundu Antipus Lissu

    Votes: 57 44.2%
  • 3. John Wegesa Heche

    Votes: 49 38.0%

  • Total voters
    129
  • Poll closed .
Kwa hyo wewe unamtaka mtu anaeisema ccm na syo kuiondoa ccm kwq kuwasemea wananchi?
 
Heche atapelekea CDM ikubalike kanda ya ziwa,magharbi na kati. He is ok up stairs si mwoga
 
Kwani demokrasia inamtaka akae madarakani miaka mingapi kwenye uongozi wa juu?

Au chama chao hakina ukomo wa kuongoza hadi mtu afie madarakani kwa uzee kama ilivyokuwa kwa Mugabe, na ilivyo kwa Paul Kagame au mu7 wa Ug?
 
Lissu anapaswa kuwa Waziri Mkuu wa Rais fulani lakini kwa nafasi ya Urais HAPANA. Lissu hawezi kuwa Rais. Lissu ni mtu tu wa kutumwa na kutekeleza. Nina ushahidi wa kauli zake nyingi kabla hajapigwa risasi na baada ya kupigwa risasi.

Urais unahitaji mtu mwenye utulivu wa akili, busara na asiye na ghadhabu. Kwenye uongozi tofauti ya Lissu na Magufuli ni ndogo sana.

Kama CHADEMA inaweza kutoa kiongozi mzuri basi ni Mbowe anazo qualities zote. Lakini ni mfanyabiashara. Atatumia fursa zote kujitajirisha kama anavyofanya na fedha na raslimali za chama. Wakishindwa basi John Mnyika
 
Sasa pigakura
 
CHADEMA waonyeshe mfano halisi wa Demokrasia wanayo washawishi kuwa ndio Inayofaa.

Haya ya kujificha kwenye "Katiba yetu" 'inaruhusu' haileti taswira nzuri. Je ndio maana wanadai Katiba mpya ili wajisimike miaka 20 ya uongozi bila ya kupingwa?

Kuna ajenda iliyojificha katika kudai Katiba mpya?

Mbowe asamehe tu hela zake.
 
Tk
 
Mbowe kwasasa hana jipya ndani ya chadema, tunahitaji muongoza dira mpya... Tundu Lissu... Afu makamu wake awe Heche!! Haloo
 
Mbowe kwasasa hana jipya ndani ya chadema, tunahitaji muongoza dira mpya... Tundu Lissu... Afu makamu wake awe Heche!! Haloo
Pigakura sasa
 
Sioni kama ni tatizo Mbowe akiwa m/kiti wa Chadema for life. Tatizo letu kama taifa ccm.
 
Angalau Lissu anaeleweka alisomea nini huenda akatusaidia kwenye mikataba na kesi mbalimbali dhidi ya beberu. Hao wengine wawili hua nahisi ni mishen town wanafanikiwa kwa kuujua tu mji na kona zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…