Huyu Catherene Ruge kati wa wanawake wenye nguvu na ushawishi CHADEMA, alikuwemo ktk 10....
Shida yake ni kushindwa kutumia akili ktk kufanya maamuzi badala yake yeye na wenzake kina Wenje, Boni Yai, yule mwenyekiti mpya wa BAWACHA, Yericko Nyerere, Ntobi nk wakakubali kulipwa mapesa ya rushwa yaliyobeba laana ya damu za watanzania wana CHADEMA waliouwawa na Abdul na mama yake Bi Samia Suluhu Hassan...
Hawa kina Catherine wakauza utu na heshima yao huko. Laiti wangekuwa wavumilivu, wakaitetea na kusimama upande wa HAKI bila shaka, kwa uadilifu wao huo hizi nafasi zingekuwa zao tu bila shaka...
Lakini walichagua uchafu, rushwa na ufisadi. Ni nani huyo atawatetea na kuwapa heshima? Wameuza heshima na utu wao. Ni sharti walipie gharama ya matendo yao...
Kwa sasa wasubiri kwanza nchi ikae sawa.
Mafisadi wanatumia nguvu ya Pesa kuua utaifa na uzalendo kwa kusingizia cha haki sawa wakati hakuna usawa wa kisiasa .
Yaani hakuna haki katika chaguzi halafu wanaleta habari za kusadikika . Wazalendo wapo Bize kurudisha heshima ya chama .
Huyo manamama aitwe kwenye kamati ya maadili maana hao ndio wanaotututoa kwenye reli kwa pesa walizopewa.
Sisi tunataka tume huru na kuachana na mambo ya kuuzana na kutekana huku Wahusika wakiwa ndani ya Chadema kwa kutoa taarifa kwa Machawa wa CCM kwa fedha . Yaani Mayuda wasaliti kwa rushwa ya fedha wapo Chadema hawa kwanza wanatakiwa wafukuzwe uanachama maana ndio wanaouza watu na watu kutekwa halafu wanasema wanataka maridhiano .
Yaani mtu mtu akuibie halafu wewe ndio umuombe murudhiane badala ya kurudisha mali yako kwanza na kuomba Msamaha .
Pesa walizokuwa zimeshindwa kufanya kazi .
Hapo kinachotakiwa kufanyika kwa sasa ni Kundi la Tundu Lisu kuacha kuwajibu hao wala rushwa . Pesa zinawapa kiburi . Watawapotezea dira. Kinachotakiwa ni Wanachama kufanya mapokezi makubwa ya kuwapokea viongozi wa kitaifa lakini pia kumuaga Mbowe kwa heshima kubwa .
Lakini pia hao akina Ruge na wenzake wakiendelea hivyo basi wanachama ndio watakao wajibu maana hata kwenye nafasi za ubunge kura zitapigwa na wala rushwa hawatapata .
Uchaguzi hua ukiisha aliyeshinda anaheshimiwa na kupongezwa sio huo ujinga wa kina Ruge . Samia asiwape kiburi kwa pesa muda wake utaisha kufumba na kufumbua . Yeye sio Mungu zaidi amejenga mfumo wa kishetani wa rushwa na uovu mwingi wa kupenda fedha kwa njia haramu . Leo hii mauaji ya watu kwa sababu za kishirikina yameongezeka sana kwa sababu ya kuwa na viongozi na watu wa dini wanaohubiri pesa tu badala ya utu na haki na kuthamini binadamu badala ya ubinafsi .
Ruge amechagua fungu la kukosa. Akae kwa kutulia Chadema ya Lisu ndiyo itakayoingia madarakani hata kama sio mwaka huu lakini katiba mpya na Tume huru itapatikana kipindi cha Lisu na CCM itaangshwa na Lisu halina ubishi . CCM iko mwisho kabisa na hakuna wa kuiokoa maana hata Mungu wamemkashifu kama watengenezaji wa Meli ya Titanic waliosema meli ile hata Mungu hawezi kuizamisha .
CCM wamesema hata Mungu ampende asipende ushindi kwao ni lazima .
Kwa hiyo Ruge aende huko kwa wa atu wasiomjua Hata Mungu kwa sababu ya kujilimbikizia mali wanakisahau kua hazitaweza kuwaokoa wakati wa kisasi cha Mungu ukifika .