Catherine Ruge ameuita mfumo mpya wa uongozi wa CHADEMA kuwa ni mfumo dume "patriarchy"

Maoni ya Catherine Ruge huenda yamesababishwa na hasira ya matokeo ya uchaguzi, maana ameshindwa kutetea nafasi yake ya Katibu wa Bawacha,
This is obvious, she's salty kwa kuangushwa na outsider. Alichagua upande wa Mbowe nao ukashindwa meaning hana tena path ya kuwa top bureaucrat kwenye chama.

She chose her path, let her deal with it.
 
Catherine aligombea kama KM wa Bawacha, but kura hazikutosha,

Anyways, CDM won, People wins...

Tusubir Kazi
 
Mbona Rose Mayemba, Salima Kasunzu wamechaguliwa ujumbe kamati kuu?. Au hujui kamati kuu ndio the most powerful committee ya chama.

Hao wawili walifanyiwa figisu nyingi sana wasishinde Rose Mayemba hadi sasa uchaguzi wake hauhitimishwa, yote hayo ilikuwa ili kumuangusha Msigwa. Rose Mayemba anaonekana ni jembe sana, mkweli, mpenda haki. Atafika mbali.

Salma Kasanzu form yake ilifichwa hapo Mlimani city asiweze kufanyiwa usaili.

View: https://youtu.be/pfMrZF7ISCc?si=OQFyOVZBlHeIEjhJ
 
ACT chama tanzu cha ccm na ni ngumu mwanamke kuwa kiongozi wa juu cdm kwa sababu mateso wanayopata kutoka kwa vyombo vya dola
 
H
Hahaha Team Lisu kwao wakishinda ndio haki, wakishindwa ni figisu. Demokrasia haitimii kwa wewe tu kushinda, kushindwa nayo ni demokrasia.
 


Kwa sasa wasubiri kwanza nchi ikae sawa.

Mafisadi wanatumia nguvu ya Pesa kuua utaifa na uzalendo kwa kusingizia cha haki sawa wakati hakuna usawa wa kisiasa .
Yaani hakuna haki katika chaguzi halafu wanaleta habari za kusadikika . Wazalendo wapo Bize kurudisha heshima ya chama .

Huyo manamama aitwe kwenye kamati ya maadili maana hao ndio wanaotututoa kwenye reli kwa pesa walizopewa.
Sisi tunataka tume huru na kuachana na mambo ya kuuzana na kutekana huku Wahusika wakiwa ndani ya Chadema kwa kutoa taarifa kwa Machawa wa CCM kwa fedha . Yaani Mayuda wasaliti kwa rushwa ya fedha wapo Chadema hawa kwanza wanatakiwa wafukuzwe uanachama maana ndio wanaouza watu na watu kutekwa halafu wanasema wanataka maridhiano .

Yaani mtu mtu akuibie halafu wewe ndio umuombe murudhiane badala ya kurudisha mali yako kwanza na kuomba Msamaha .


Pesa walizokuwa zimeshindwa kufanya kazi .

Hapo kinachotakiwa kufanyika kwa sasa ni Kundi la Tundu Lisu kuacha kuwajibu hao wala rushwa . Pesa zinawapa kiburi . Watawapotezea dira. Kinachotakiwa ni Wanachama kufanya mapokezi makubwa ya kuwapokea viongozi wa kitaifa lakini pia kumuaga Mbowe kwa heshima kubwa .

Lakini pia hao akina Ruge na wenzake wakiendelea hivyo basi wanachama ndio watakao wajibu maana hata kwenye nafasi za ubunge kura zitapigwa na wala rushwa hawatapata .

Uchaguzi hua ukiisha aliyeshinda anaheshimiwa na kupongezwa sio huo ujinga wa kina Ruge . Samia asiwape kiburi kwa pesa muda wake utaisha kufumba na kufumbua . Yeye sio Mungu zaidi amejenga mfumo wa kishetani wa rushwa na uovu mwingi wa kupenda fedha kwa njia haramu . Leo hii mauaji ya watu kwa sababu za kishirikina yameongezeka sana kwa sababu ya kuwa na viongozi na watu wa dini wanaohubiri pesa tu badala ya utu na haki na kuthamini binadamu badala ya ubinafsi .

Ruge amechagua fungu la kukosa. Akae kwa kutulia Chadema ya Lisu ndiyo itakayoingia madarakani hata kama sio mwaka huu lakini katiba mpya na Tume huru itapatikana kipindi cha Lisu na CCM itaangshwa na Lisu halina ubishi . CCM iko mwisho kabisa na hakuna wa kuiokoa maana hata Mungu wamemkashifu kama watengenezaji wa Meli ya Titanic waliosema meli ile hata Mungu hawezi kuizamisha .

CCM wamesema hata Mungu ampende asipende ushindi kwao ni lazima .
Kwa hiyo Ruge aende huko kwa wa atu wasiomjua Hata Mungu kwa sababu ya kujilimbikizia mali wanakisahau kua hazitaweza kuwaokoa wakati wa kisasi cha Mungu ukifika .
 
ACT chama tanzu cha ccm na ni ngumu mwanamke kuwa kiongozi wa juu cdm kwa sababu mateso wanayopata kutoka kwa vyombo vya dola


Kuna watu wapumbavu sana . Yaani mtu kama ni mpinzani kutojiingiza kwenye siasa za CCM ni usalitikubwa sana .
CCM ina mambo ya ajabu sana na yanayohatarisha sana amani ya nchi . Ni bahati tu angalau Nyerere alijenga majeshi imara sana na yenye nidhamu kubwa sana ndio maana wanawaficha CCM uovu wao kama chama tawala lakini CCM ina siasa hatari sana .

Kwa mfano akiwa Rais Mkristo wanaingiza saa ana Udini na kusema kuwa Rais ni lazima awe Mkatoliki k wa sababu tu wanajua wakatoliki wanaushawishikubwa ndani na nje ya nchi lakini pia wanauwezo wa kuchambua mambo bila kukurupuka . Watawadanganya watu kuwa sasa ni zamu ya wakristo matokeo yake wa ataleta mtu wa kakundi fulani . Hata hivyo wakristo kutokana na migawanyiko yao ya madhehebu inakua kuwa ni ngumu kuwashika akili na kuwaaminisha mambo ya kijinga. Akiwa raisi Muislam wanaibuka watu ndani ya CCM na kuunda vikundi vya kuhamasisha kuwa sasa ni zamu yetu na wa anatumia fedha nyingi kueneza propaganda za kumsaliti mwenzetu kwa sababu wenzetu zamu yao wanatubagua . Matokeo yake ni kujenga chuki kwa wale wanaopinga mambo ya kidini . Hali hii kwa wa afia dini inaleta chuki mpaka kuuana kwa sababu wanaona wasio penda hayo maujinga kuwa ni wasaliti na wasiokuwa na dini.

Tumeondoka kwenye kuwapata watu wenye uwezo wa kuongoza nchi bali waliowekwa na kakundi ka watu wachache wasiojali moja wa kitaifa zaidi ya matumbo yao .
Wengine wakishapewa pesa za kwenda Israel na Maka basi wanafanya maovu mengi wakiaminishwa kuwa wakifika kwenye hizo hija wanasamehewa dhambi zao zote .

CCM ina siasa za kishamba sana
 
Hivi wale wanawake wawili Rose na Kasanzu walioteuliwa kuingia kamati kuu ni nafasi gani zile?
 
Uongozi unatakiwa kutolewa kwa merit, hata kama mwanamke, awe na merit, sasa tutajuaje kakosa uongozi hata baada ya kuwa na merit, na si kwa kukosa merit?

Tumeona hata wanaume wamenyukana na wengine kushindwa.

Kina Mbowe, Wenje, Odero, wameshindwa, wale si wanawake.

Sasa tutajuaje wanawake wameshindwa kwa sababu ya patriarchy na si kwa sababu ya kushindwa kwa kukosa merit tu?

Analalamika hakuna mwanamke pale juu, kwani kuna mwanamke gani kagombea nafasi za mwenyekiti na makamu mwenyekiti? Alitaka wanawake wapewe nafasi hizo tu bila kugombea?
 
H

Hahaha Team Lisu kwao wakishinda ndio haki, wakishindwa ni figisu. Demokrasia haitimii kwa wewe tu kushinda, kushindwa nayo ni demokrasia.
Nina uhakika hujamsikiliza au hata kufuatlia story yake, uchaguzi wa Njombe, Kanda ya Nyasa.

Hana mpinzani Njombe, lakini hata kura ya kupigiwa yeye kama mgombea pekee ndio au hapana ulivurugwa na watu walioletwa kufanya fujo.
 
Wanawake ni wa kuwasamehe tu maana akili zao wanazijua wenyewe......mwanamke sio wa kumjibu ni wa kumuangalia hasa kwenye mambo ya kipuuzi......wao wenyewe akili zao hawazielewi.......
 
Kabla ilikua, Mbowe, Lissu,yule sheikh wa zenj, Mnyika, Kigaila na Mwalimu....Mfumo huo Catherine hakuuona?
 
Unapokuwa mstari wa mbele unawekaje hizi vitu? Baada ya kusonga mbele utaanza kurudi nyuma kusaidiana.
 
Aende kule akapewe
 
Uaneni tuu huko ,CCM ndio chama kimbilio hao matapeli watawazungusha kichwa Hadi mpate moto with zero results
 

..katika meza kuu kuna nafasi 3, yaani Katibu Mkuu, na Manaibu wake wawili, ambao wanateuliwa na mwenyekiti na kuthibitishwa na baraza kuu. Naamini Catherine Ruge alitamani kuwepo na uwakilishi wa wanawake ktk nafasi hizo.
 
Ujinga mtup
u
 
..katika meza kuu kuna nafasi 3, yaani Katibu Mkuu, na Manaibu wake wawili, ambao wanateuliwa na mwenyekiti na kuthibitishwa na baraza kuu. Naamini Catherine Ruge alitamani kuwepo na uwakilishi wa wanawake ktk nafasi hizo.
Sasa Catherine Ruge kasimama upande wa Mbowe, upande ambao umeshindwa on merit. Kwa nini anaona kashindwa kwa sababu ya patriarchy na si kwa sababu alikuwa upande usio sahihi?

Hata Mbowe kashindwa, lakini, hakushindwa kwa sababu ya patriarchy.

Kwa nini wanawake wakishindwa wanakuwa wepesi kutaja patriarchy hata kama wameshindwa on merit?

Hapa mtu ambaye angekuwa na nafasi ya kusikilizwa zaidi kwenye hoja ya patriarchy angekuwa mwanamke ambaye akisimama upande wa Lissu, halafu akataka hizo nafasi, halafau akakosa.

Huyo angeweza kutuonesha kuwa, kukataliwa kwake hakutokani na tofauti za kisiasa, kunatokana na patriarchy.

Sasa huyu Catherine Ruge tunajua ana tofauti za kifalsafa na Lissu, Catherine alikuwa upande wa Mbowe, kama kakataliwa na Lissu kwa sababu za kifalsafa kwa nini anataja mambo ya patriarchy?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…