PreGE2025 Catherine Ruge: Nimeenguliwa kwa SMS bila kujulishwa makosa yangu ambapo ni kinyume na Katiba ya CHADEMA

PreGE2025 Catherine Ruge: Nimeenguliwa kwa SMS bila kujulishwa makosa yangu ambapo ni kinyume na Katiba ya CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyu mama alionesha kufurahia sana sakata la akina Halima Mdee kipindi kile kwakua aliamini atabaki na nafasi kubwa ndani ya chama, naona mambo yanaanza kwenda ndivyo sivyo.

Tusishangae baada ya bunge kuvunjwa wenzake wakaja kuomba msamaha na wakapewa nafasi za kugombea yeye akakosa kwasababu ameshaanza kuonesha utovu wa nidhamu kwa Mwenyekiti.
Hawakujua kuwa covid19 ni project ya Mbowe.

Pia hawakujua kuwa Mbowe mchana hushinda CHADEMA usiku hulala Ikulu.

UKikaa chini ya mti uliooza mimizi kuna siku utakuanguakia.

Wote walioamini Mbowe ndio mtu salama, msafi na makini na wakajitoa kufa na kupona kwake kwa kujya au kwa kutokujua...wote wataangukiwa na mti huu...wanapotea kisiasa.


Kwa uxoefu wangu mtu muasi hajawahi kufanikiwa popote.

Nawahurumia kuwa wamechagua kuucheza muziki wa Mbowe na inaenda kula kwao moja kwa moja.

Je...Lissu na Heche watazinyamazia hila za Mbowe zinazoendelea kwa chini chini?

Je wakizianinika utafikiri hali itakuwaje?

Je team Mbowe inayojaribu kumwangusha Lissu kwa mara ya pili wataweza?


Je mnakumbuka kuwa Lisdu alisema kipindi cha kampeni kuwa chama kimetekwa anataka kukiokoa...tunaliona hili sasa?.

Kumbe Mbowe alishakidalalia chama ccm mapema sana
 
Catherine Ruge pia ameeleza kuwa ameenguliwa bila kupewa taarifa rasmi, akikiri kupata taarifa za kuenguliwa kwake kupitia ujumbe mfupi wa simu (sms)na Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika, bila ya kuelezwa makosa yake na sababu za kuenguliwa kwake ambapo pia ni kinyume na Katiba ya nchi ibara ya 13 (6)(a) ambayo imeweka misingi ya kusikilizwa.

Soma Pia: Tundu Lissu atengua uteuzi wa CPA Catherine Ruge

"Nimeshtushwa na uamuzi wa Mwenyekiti wa Chama Taifa ambaye pia ni Mwanasheria nguli kukiuka misingi ya Katiba ya Chama chetu na misingi ya haki za binadamu hasa haki ya kusikilizwa.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kanuni ya Chama toleo la mwaka 2019 kanuni ya 6.5 imeweka pia utaratibu wa kumchukulia hatua mwanachama na Kiongozi yeyote ndani ya chama, mathalani kanuni inaweka utaratibu wazi wa kufuatwa wakati wa kuchukua hatua za kinidhamu, mojawapo ni kuandikiwa mashtaka yako na kupewa nafasi ya kusikilizwa." Amesema Catherine Ruge.

View attachment 3294486
Hilo nalo jinga kweli yeye anaongozwa na katiba ya chama chake au katiba ya nchi hiyo ibara aliyo i quote ni ya katiba ya chama chake au katiba ya nchi huu ujinga huu
 
Uwe umejulishwa kwa sms, kwa mitandao ya kijamii, sisi hayatuhusu, kifo ni kifo tu hakina jinsia.
 
Back
Top Bottom