Pre GE2025 Catherine Ruge: Rais Samia anahofia mageuzi yataiondoa CCM Madarakani

Pre GE2025 Catherine Ruge: Rais Samia anahofia mageuzi yataiondoa CCM Madarakani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
8 July 2024
‘Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) - 'Samia Anahofia Mageuzi Yataiondoa CCM Madarakani’


Catherine Ruge, Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), amesema kwamba sababu kubwa ya kufeli kwa mchakato wa kuleta mageuzi ya kisiasa nchini, kama vile upatikanaji wa Katiba Mpya, ni hofu aliyonayo Rais Samia Suluhu Hassan kwamba endapo mageuzi hayo yatatokea, chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM), kinaweza kuondoka madarakani.
 
Exclusive kwa kirefu : Kuna sababu zaidi ya 1,000 za kwanini safari hii 2025 CCM inang'oka kutoka madarakani.

Katibu mkuu wa BAWACHA afafanua sababu moja hadi nyingine ni ......
 
July 2024
Nkasi, mkoani Rukwa
Tanzania

Wananchi kwa mamia wajitokeza mkutano wa mbunge Aida Kenani
kumsikiliza mbunge wao kamanda Aida Kenani wa CHADEMA jimbo la Nkasi Kaskazini alipotembelea kata ya Mkinga

SIKUBIPU KUGOMBEA NA VIATU HIVI VINANITOSHA_KATA YA MKINGA


azumgumzia mambo mazito ya wananchi wananchi wa Rukwa wanaopakana na ziwa Tanganyika na maendeleo ya watu ..

Wananchi kwa mamia wanyoosha mikono juu na kupaza mayowe kumuunga mkono hoja za mbunge wao waliomchagua 2020

Mbunge asisitiza yeye bungeni hakuzungumzii mambo ambayo hawajamtuma maana wao ndiyo wamemuajiri na kumtuma maoni yao yasikike bungeni..

Mfano wananchi waliokata leseni Nkasi waishio pembezoni mwa ziwa Tanganyika hawakukata leseni za maandazi, bali leseni za uvuvi na ndiyo maisha yao ....

Wananchi kunyanyaswa kwa kuvua katika mabwawa pia haikubaliki, acheni kuwakataza ....
 
July 2024
Kirando, Nkasi
Rukwa Tanzania

MBUNGE AIDA KENANI ANAENDELEA NA ZIARA YA KIKAZI NA KUPOKELEWA KWA SHANGWE

Kirando ni kata ya Wilaya ya Nkasi katika Mkoa wa Rukwa, Tanzania, inayopakana na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa upande ....
 
July 2024
Nkasi, Rukwa
Tanzania

UMMMA WA WANANCHI WA NKASI MKUTANO WA MBUNGE WAO AIDA KENANI

Kunja kunja ngumi za nguvu za umma...piiii-pooz! Pawa. Turudie tena piiiiii pooz pawa (people's power) PAWA!!!! ....

Naamini sauti hii ya wana Nkasi imesikika, sasa tuingie moja kwa moja kuhusu masuala yanayogusa maisha yenu wananchi ....

Ndugu wananchi wa Chala | Isale | Isunta | Itete | Kabwe ... nimesimama hapa nikiwa na maumivu makubwa mbunge wenu, kazi ya mbunge ni kusikiliza maoni yenu, kauli yenu ikawa moja mkanituma niende kumwambia rais kupitia bungeni

... nikatoa angalizo wananchi hawakushirikishwa wakati katiba ya nchi inatamka kuwa raia yaani wananchi ndiyo wenye mamlaka ya mwisho juu ya hatima ya nchi yao ...

Kama serikali na wizara bungeni hataki kusikiliza maoni ya raia mimi nitarudi kwa matajiri wangu ambao ndiyo walioniajiri yaani wananchi wa Nkasi ya Kaskazini kuwashitaki ....
 
July 2024

CHADEMA INASEMA SIASA NI MAISHA, TUNACHUKUA DOLA

Kanda ya Nyasa CHADEMA yaelezea jinsi viongozi wa serikali walivyokamata misaada ya CHADEMA iliyolegwa kupelekwa kwa wananchi
 
RUNGWE, MBEYA
TANZANIA,

UPEPO WA KISIASA WAGEUKA, TANGA LA JAHAZI LA CHADEMA YAKOLEZA MBIO KUELEKEA USHINDI
 
8 July 2024
‘Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) - 'Samia Anahofia Mageuzi Yataiondoa CCM Madarakani’


Catherine Ruge, Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), amesema kwamba sababu kubwa ya kufeli kwa mchakato wa kuleta mageuzi ya kisiasa nchini, kama vile upatikanaji wa Katiba Mpya, ni hofu aliyonayo Rais Samia Suluhu Hassan kwamba endapo mageuzi hayo yatatokea, chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM), kinaweza kuondoka madarakani.
Waondoke!
 
July 2024

WANACHAMA 193 WAPYA WAPOKELEWA KWA KIAPO MKINGA

Wananchi wameamua mkoani Rukwa kwenda na CHADEMA kuelekea ..... ushindi wa ....
 
Tume Huru ya Uchaguzi sheria mpya za teuzi za Makamishna yapitishwa na rais huku akishuhudiwa na viongozi wa vyama vya upinzani pamoja na bunge la taifa pia bunge la seneti.

Hali hivyo ya usikivu wa serikali imetokana na nini, tujiunge na waandishi wa gazeti la Taifa Leo :

Presha ya Gen Z yazaa matunda, Ruto akitia saini mswada wa IEBC​

Na KEVIN CHERUIYOT, BENSON MATHEKAJuly 9th, 2024 2 min read

NADCO-2.gif

Rais William Ruto akiwa na nakala ya mswada alioutia saini kupisha uteuzi wa makamishna wapya wa IEBC

RAIS William Ruto atia saini Mswada wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (uliorekebishwa) wa 2024 kuwa sheria.

Dkt Ruto alitia saini mswada huo Jumanne katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi mbele ya viongozi wa upinzani Raila Odinga (Orange Democratic Movement), Kalonzo Musyoka (Wiper Party), Naibu Rais Rigathi Gachagua na viongozi wa Bunge la Kitaifa na Seneti.
Hatua hiyo sasa inapisha rasmi uteuzi wa jopo la uteuzi litakaloajiri makamishna wapya wa tume ya uchaguzi.

NADCO-300x180.gif

Msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed mnamo Jumatatu alisema mswada wa IEBC ulikuwa wa kwanza kushughulikiwa na Bunge kulingana na mapendekezo ya ripoti ya Kamati ya Mdahalo wa Kitaifa (Nadco).

Ripoti hiyo ni zao la kamati ya pande mbili, iliyojumuisha viongozi kutoka mrengo wa Kenya Kwanza wa Rais Ruto na Azimio la Umoja One Kenya Coalition wa Bw Odinga.


Soma kwa kina kusainiwa kwa sheria ya marekebisho ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC SOURCE : Presha ya Gen Z yazaa matunda, Ruto akitia saini mswada wa IEBC
 
09 July 2024

Hotuba ya Rais Ruto na kiongozi wa Azimio Raila Odinga baada ya kupitishwa kwa mswada wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo - IEBC

 
09 July 2024

MAKALLA - "UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA NI UCHAGUZI MUHIMU SANA"

 
HOFU YA GEN-Z YAWAKUMBA WATAWALA AFRICA
Wachambuzi wa siasa wanasema mengi yamebadilika tangu vijana wa Kenya waanze maandamano ya kupinga utawala mbaya na ufisadi.

wanasiasa sasa kote Africa wanajitahidi kuanza kukubali utawala bora sasa na wa haki kwa kasi kubwa kuliko kwa hofu ya nchi zao kukumbwa na wimbi la vijana wa GEN-Z walioamua kuchukua hatima ya maisha yao mikononi mwao badala ya kusubiri hisani kutoka kwa watawala wa kizazi kilichopita wasiojua mahitaji ya vijana ...
 
8 July 2024
‘Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) - 'Samia Anahofia Mageuzi Yataiondoa CCM Madarakani’


Catherine Ruge, Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), amesema kwamba sababu kubwa ya kufeli kwa mchakato wa kuleta mageuzi ya kisiasa nchini, kama vile upatikanaji wa Katiba Mpya, ni hofu aliyonayo Rais Samia Suluhu Hassan kwamba endapo mageuzi hayo yatatokea, chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM), kinaweza kuondoka madarakani.
Uko sahihi
Si mageuzi ya kisiasa tu na maendeleo yatakuja kwa kasi pia
 
Back
Top Bottom