Pre GE2025 Catherine Ruge: Rais Samia anahofia mageuzi yataiondoa CCM Madarakani

Pre GE2025 Catherine Ruge: Rais Samia anahofia mageuzi yataiondoa CCM Madarakani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
11 July 2024
Dar es Salaam, Tanzania

HATIMAYE MAANDAMANO YAFIKA MBELE YA OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CCM MTAA WA LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM

View: https://m.youtube.com/watch?v=zbVwwGgSC6Y

Huku sauti zikizizima kuwa wanataka haki na soko lao, wafanyabishara wa Kariakoo wameonesha imani yao ndogo iliyobaki kwa chama dola kongwe CCM....

Itapofika kifu yao ya imani, je watahamisha imani yao kwa chama gani au hasira zao watazitumia vipi chaguzi za 2024 na 2025 dhidi ya utawala wa CCM na wizara ya nchi ofisi ya Rais OR-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI

Bilioni 228 zilitolewa kwa vizimba 3500 kurekebisha Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam lakini wafanyabiashara wanazungushwa imebidi leo wapige kambi mbele ya Ofisi hiyo maarufu ya mikakati ya kisiasa ya CCM kufikisha kilio chao.

Mkuu wa wilaya ya Ilala ameshindwa kupata jibu la moja kwa moja kuhusu kadhia ya kunyimwa vizimba katika soko kuu la Kariakoo ....
 
15 July 2024
Kamsaba,
Jimbo la Momba.

Pamewaka!! CHADEMA WAIVURUGA CCM KAMSAMBA // WANACCM 100 WAHAMIA CHADEMA // WAFUNGUKA BAADA YA KUHAMIA

View: https://m.youtube.com/watch?v=ZTDtjKXVT-o

hotuba nzito za CHADEMA zashawaishi wanaCCM na wananchi.

Wasisitiza nchi kuwa na vijana na raia jeuri wanaoweza kuhoji badala ya kugaragara chini bali tuwahoji viongozi wa serikali

Leo kuna Kamsamba wanaCCM 100 kwa niaba ya wenzao wamejitokeza mbele ya makamu mwenyekiti wa kanda Nyasa CHADEMA..

Dhuluma za stakabadhi ghalani kwa zao la ufuta ni jambo la makosa makubwa wanalofanya serikali ya CCM kwa wananchi wa Kamsamba Momba ... huo ni ubabaishaji mkubwa wananchi walipwe kwa wakati badala ya kupewa risiti kwa mali kauli wakati wananchi wanataka fedha mkononi..

Serikali ya CCM imechoka hivyo inahitaji kupumzishwa mfano mahindi WFP wanataka kununua kwa bei ya Tshs. 1,000 lakini serikali hii ya CCM inataka wakulima wa mahindi walipwe Tshs. 500 kwa kilo ya mahindi.... chama dola kongwe cha kijani kimeshindwa kuwatetea ..

Halafu kwa kuwa 2024 na 2025 CCM wanakuja hapa na kibaba cha chumvi kutaka muwapigie kwa mapipa ya Pombe na T-Shirt, muwakatae hawa CCM.

Wazee wetu wamechoka kwa maji ya kutoka kutekwa mbali leo hii wanamuahidi katika umri huu kuwaletea maji, walikuwa wapi miaka yote hii 60 toka huyu mzee wetu akiwa kijana ... muwakatae hawa CCM kwa ahadi zao hewa miaka nenda rudi ..

Wana wa Kamsamba hivi kwanini mtembee na jini la CCM katika mfumo wa kadi ndani ya mfuko wako, leo tumechelewa kuwahii kufika ktk mkutano huu kutokana na barabara mbovu ikabidi gari yetu kutumia njia ya ngombe kufika hapa Kamsamba ...
 
Mambo magumu CCM, mbinu zote za kuomba kura kwa staili mpya wazitumia

1721052344252.png
 
17 Julai 2024
Tarime, Tanzania

BAWACHA TARIME VIJIJINI WAKIWASHA , VERONICA SANDO AKABIDHI MIKOBA KWA M/KITI MPYA LOYCE MANYATA

View: https://m.youtube.com/watch?v=Y4EiCGGa-qw

BAWACHA yajipanga kushiriki moja kwa moja katika uchaguzi wa 2024 na 2025 kuchukua uongozi wa vitongoji, udiwani na kuacha kutegemea viti vingi maalum ....
 
Julai 2024
Rungwe, Mbeya
Tanzania

SUGU AREJESHA MATUMAINI ........ MKUTANO WA HADHARA JIMBO LA RUNGWE KATA YA NDANTO MKOANI MBEYA

View: https://m.youtube.com/watch?v=s3rp3nMpmAg

Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa kamanda Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akiwa katika mkutano mkubwa kata ya Ndanto Rungwe mkoani Mbeya ...

Ndanto ni kata ya Wilaya ya Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 17,984....

Makubwa yaibuliwa mkutanoni ya kamata kamata inayowalenga makada na wapenzi wa CHADEMA inaendelea kwa CCM kutumia vyombo vya dola kujaribu kutisha raia kata ya Ndanto Rungwe walioamua kwenda na CHADEMA 2024 / 2025 ...
 
8 July 2024
‘Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) - 'Samia Anahofia Mageuzi Yataiondoa CCM Madarakani’

Catherine Ruge, Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), amesema kwamba sababu kubwa ya kufeli kwa mchakato wa kuleta mageuzi ya kisiasa nchini, kama vile upatikanaji wa Katiba Mpya, ni hofu aliyonayo Rais Samia Suluhu Hassan kwamba endapo mageuzi hayo yatatokea, chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM), kinaweza kuondoka madarakani.
Inaonesha hajuwi maana ya R nne za mama Samia.
 
SIna la kusema!
CCM wako mitaani kuandikisha wapiga kura!
Huenda kilichofanyika uchaguzi serikali za mitaa 2019 kinaenda kutokea tena!
 
SIna la kusema!
CCM wako mitaani kuandikisha wapiga kura!
Huenda kilichofanyika uchaguzi serikali za mitaa 2019 kinaenda kutokea tena!

Kabisa wanaenda kuvuruga uchaguzi wa 2024 huku wananadi 4R kwa hadaa kubwa.
 
Julai 2024
Mbinga Mjini, Ruvuma
Tanzania

CHADEMA MBINGA WAKITOA ELIMU YA UCHAGUZI VIJIJINI

View: https://m.youtube.com/watch?v=FfMHlS9TGuQ

Viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) jimbo la Mbinga mjini wakiongozwa na mwenezi wa chama hiko kamanda Wurso Aloyce, mwenyekiti wa BAWACHA kamanda Mariam Mapunda, katibu wa jimbo kamanda Amina Saidi, mwenyekiti wa chama wilaya kamanda Steven Mateso pamoja na mwanachama mwakilishi wa wadau mkoa wa Ruvuma kamanda Menrick Sanga.

Wamefanya ziara ya operesheni maalum katika kijiji cha Rudisha kilichopo kata ya Kilimani jimbo la Mbinga mjini, wamefika kijijini hapo na kutoa elimu ya uraia na elimu ya uchaguzi kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa mwaka huu 2024

Kata Kilimani wilaya ya Mbinga mjini ina vijiji vifuatavyo: Kilimani, Sepukila, Mhekela, Rudisha, Mkwaya na Njomlole.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 14,594. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,529 waishio humo.
 
Nyie. Chadema bwana🤣 Ila mnajijua wenyewe, nyie kuleni ruzuku tu Ila Kura msahau
 
8 July 2024
‘Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) - 'Samia Anahofia Mageuzi Yataiondoa CCM Madarakani’

Catherine Ruge, Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), amesema kwamba sababu kubwa ya kufeli kwa mchakato wa kuleta mageuzi ya kisiasa nchini, kama vile upatikanaji wa Katiba Mpya, ni hofu aliyonayo Rais Samia Suluhu Hassan kwamba endapo mageuzi hayo yatatokea, chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM), kinaweza kuondoka madarakani.
It is obvious
 
Julai 2024
Mbinga Mjini, Ruvuma
Tanzania

CHADEMA MBINGA WAKITOA ELIMU YA UCHAGUZI VIJIJINI

View: https://m.youtube.com/watch?v=FfMHlS9TGuQ

Viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) jimbo la Mbinga mjini wakiongozwa na mwenezi wa chama hiko kamanda Wurso Aloyce, mwenyekiti wa BAWACHA kamanda Mariam Mapunda, katibu wa jimbo kamanda Amina Saidi, mwenyekiti wa chama wilaya kamanda Steven Mateso pamoja na mwanachama mwakilishi wa wadau mkoa wa Ruvuma kamanda Menrick Sanga.

Wamefanya ziara ya operesheni maalum katika kijiji cha Rudisha kilichopo kata ya Kilimani jimbo la Mbinga mjini, wamefika kijijini hapo na kutoa elimu ya uraia na elimu ya uchaguzi kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa mwaka huu 2024

Kata Kilimani wilaya ya Mbinga mjini ina vijiji vifuatavyo: Kilimani, Sepukila, Mhekela, Rudisha, Mkwaya na Njomlole.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 14,594. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,529 waishio humo.

Wao wanawaza kupora na kutekana sisi tutimize wajuvu wetu wa kuelimisha umma na Mungu atatubariki
 
Shukrani kwa umakini, na kumradhi kwa Catherine Magige kwa usumbufu wa Google Typo predictions / Artificial Intelligence G6 smartphone

Moderator JamiiForums arekebishe kichwa cha habari.
Bwaga moyo
 
Back
Top Bottom