Pre GE2025 Catherine Ruge: Rais Samia anahofia mageuzi yataiondoa CCM Madarakani

Pre GE2025 Catherine Ruge: Rais Samia anahofia mageuzi yataiondoa CCM Madarakani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
20 November 2024
Tunduma, Tanzania

CHADEMA YAZINDUA KAMPENI KWA KISHIDO ZA TAMISEMI 2024 TUNDUMA


View: https://m.youtube.com/watch?v=HmROGEzDpv0
CHADEMA wafanya mkutano mkubwa Tunduma mkoa wa Songwe, mkutano huo uliofungua kampeni katika mojawapo wa majimbo katika kanda ya CHADEMA Nyasa umehudhuriwa na umati mkubwa ....

Halmashauri ya Mji Tunduma upo umbali wa km 30 kutoka makao makuu ya Mkoa wa Songwe, Halmashauri inapakana na wilaya ya Ileje upande wa Mashariki, Jamhuri ya Zambia na wilaya ya Momba kwa upande wa magharibi pia wilaya ya Mbozi kwa upande wa Kaskazini.
 
Lamadi, Busega
Tanzania

TUNDU LISSU AFIKA LAMADI NA KUPOKEWA KWA KISHINDO KUELEKEA UCHAGUZI TAMISEMI 2024 SIMIYU


View: https://m.youtube.com/watch?v=ayTwWByfxeI

Mji wa Lamadi umepakana na Ziwa Viktoria upande wa Magharibi, Pori la Akiba Kijereshi na Kata za Lutubiga na Mkula upande wa Mashariki, Wilaya ya Bunda upande wa Kaskazini na Kata ya Kalemela upande wa Kusini. Mji wa Lamadi ufikika kwa barabara za kitaifa ambazo ni Barabara ya Mwanza - Musoma, pamoja na Barabara ya Shinyanga, Bariadi - Lamadi.

Mitaa yake ni Itongo, Makanisani, Majengo, Msekula Road, Mwalukonge, Kisesa na vijiji vitatu ambavyo ni Lukungu, Mwabayanda na Kalago (Mwabulugu Lakeshore).

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 44,146 [2]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 22,062 waishio humo.[3].

Wakazi walio wengi ni wa makabila ya Wasukuma, Wajita, Wakurya, Wazanaki na Waha.
 
8 July 2024
‘Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) - 'Samia Anahofia Mageuzi Yataiondoa CCM Madarakani’


Catherine Ruge, Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), amesema kwamba sababu kubwa ya kufeli kwa mchakato wa kuleta mageuzi ya kisiasa nchini, kama vile upatikanaji wa Katiba Mpya, ni hofu aliyonayo Rais Samia Suluhu Hassan kwamba endapo mageuzi hayo yatatokea, chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM), kinaweza kuondoka madarakani.
Nani ambae hahofii?
 
8 July 2024
‘Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) - 'Samia Anahofia Mageuzi Yataiondoa CCM Madarakani’


Catherine Ruge, Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), amesema kwamba sababu kubwa ya kufeli kwa mchakato wa kuleta mageuzi ya kisiasa nchini, kama vile upatikanaji wa Katiba Mpya, ni hofu aliyonayo Rais Samia Suluhu Hassan kwamba endapo mageuzi hayo yatatokea, chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM), kinaweza kuondoka madarakani.
Hakuna ubishi kwenye hil8
 
Lamadi, Busega
Tanzania

TUNDU LISSU AFIKA LAMADI NA KUPOKEWA KWA KISHINDO KUELEKEA UCHAGUZI TAMISEMI 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=ayTwWByfxeI

Mji wa Lamadi umepakana na Ziwa Viktoria upande wa Magharibi, Pori la Akiba Kijereshi na Kata za Lutubiga na Mkula upande wa Mashariki, Wilaya ya Bunda upande wa Kaskazini na Kata ya Kalemela upande wa Kusini. Mji wa Lamadi ufikika kwa barabara za kitaifa ambazo ni Barabara ya Mwanza - Musoma, pamoja na Barabara ya Shinyanga, Bariadi - Lamadi.

Mitaa yake ni Itongo, Makanisani, Majengo, Msekula Road, Mwalukonge, Kisesa na vijiji vitatu ambavyo ni Lukungu, Mwabayanda na Kalago (Mwabulugu Lakeshore).

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 44,146 [2]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 22,062 waishio humo.[3].

Wakazi walio wengi ni wa makabila ya Wasukuma, Wajita, Wakurya, Wazanaki na Waha.

Mwamna aliyebarikiwa Huyu
 
Hakika chama dola kongwe CCM kina wajumbe wa fomu za TAMISEMI , wakati CHADEMA ina nguvu wa watu nguvu ya umma
 
21 November 2024
Nyamongo, Tarime vijijini
Tanzania

KIVUMBI CHA LISSU TARIME VIJIJINI, AKUSANYA KIJIJ KIZIMA CHA NYAMONGO TAMISEMI 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=A0VRw7KI5Wc

Nyamongo inapatikana katika wilaya ya Tarime Vijijini ambapo wakaazi wake ni wakulima, wafugaji, wajasiriamali, wachimbaji wadogo wa madini na wafanyabiashara

Pia Nyamongo kuna Migodi mkubwa wa Dhahabu wa North Mara unaendeshwa na Kampuni ya Barrick Gold, kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.
 
21 November 2024
Tarime mjini, Tanzania

MJINI WOTE WA TARIME WAJITOKEZA KWA MAADAMANO MAKUBWA KUMPOKEA TUNDU LISSU


View: https://m.youtube.com/watch?v=t4DD3sqACSY

Mji wazizima kwa mayowe ya furaha, miluzi, ngoma ya litungu na vigelegele kuipokea CHADEMA ilipofungua kampeni ya uchaguzi wa TAMISEMI 2024

WanaTarime walimpokea mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA mheshimiwa Tundu Antipas Lissu huku wananchi wakiimba tumechoka na chama dola kongwe CCM ...

Wananchi full tabasamu wakiimba rais wao wa mioyoni bila kuchagizwa bali ni kukubali kwao kuwa rais wa CHADEMA ataleta matumaini mpya baada ya maisha ya wazazi wao kuchakazwa na sera mbaya za CCM huku pia kizazi cha vijana nacho kukumbana na changamoto kali wakiwaza watoto wao nao wapitie hayo na kuamua sasa basi kukichagua chama dola kongwe kuanzia ngazi ya mtaa, kitongoji, kijiji, 2024 ...

View: https://m.youtube.com/watch?v=GcAhr_wCBN0
 
21 November 2024
Mbozi, Tanzania

CHADEMA YAZINDUA KAMPENI ZA TAMISEMI 2024 KWA KUSHINDO


View: https://m.youtube.com/watch?v=lfl269gZ4X8

Mji mdogo wa Mlowo jimbo la Mbozi Tanzania mambo yalikuwa moto

Mbunge wa mioyoni Paschal Haonga na viongozi wa CHADEMA wakiwa Mlowo Songwe waongea na wanachama, wapenzi na wananchi kuelekea uchaguzi wa tarehe 27 November 2024

Mbozi kwa mujibu wa takwimu za sensa ya watu na makazi ya 2022 ina jumla ya watu 510,599, hii ikiwa sawa na asilimia 40 ya wakazi wote wa mkoa wa Songwe ambao kwa takwimu hizo ni 1,344,687 [1]

Miji wilayani ni Mlowo, penye viwanda vya kahawa vitatu vya GDM, Mbozi MCCO na LIMA (watu 37,000-50,000). Aidha Vwawa ndiko makao makuu ya wilaya ambapo idadi ya wakazi wake ni zaidi ya 60,000. Miji mingine miwili iko kando ya barabara kuu ya TANZAM kutoka Dar es Salaam kupitia Mbeya kwenda Zambia.

Reli ya TAZARA inapita vilevile wilayani na kuna vituo huko Vwawa na Tunduma.

Katika wilaya hii kuna kata 29 za Vwawa, Mlowo, Ihanda, Ukwile, Ipunga, Kilimampimbi, Isalalo, Msia, Ruanda, Mahenje, Nanyala, Iyula, Hezya na Nyimbili. Nyingine ni Ichenjezya, Ilolo, Hasanga, Igamba, Nambinzo, Itaka Halungu, Isansa, Itumpi, Shiwinga, Mlowo, Magamba, Mlangali na Bara.
Ramani: Mahali pa Mbozi (kijani cheusi) katika mkoa wa Mbeya kabla haujamegwa
 
21 November 2024
Ludewa, Njombe
Tanzania

ROSE MAYEMBA ATUA LUDEWA AWACHANA UKWELI WANANCHI "MMEONA UTOFAUTI WA KUONGOZWA NA CHADEMA NA CCM"


View: https://m.youtube.com/watch?v=Vc_UB2dzf38
Ludewa kuna matatizo ya huduma za kijamii ikiwemo matibabu, vituo vya afya, maabara na usafiri. Pamoja ya kuwa wilaya hiyo ina utajiri wa asili wa ardhi, ziwa Nyasa, Mito ya Maji na madini mkakati ambayo hayajawanufaisha wakaazi wa Ludewa na nchi kwa ujumla .

Mfano Wilaya ya Ludewa iliyopo mkoa wa Njombe kuna wingi wa madini mkakati wa Liganga na Mchuchuma uchimbaji wa madini ya chuma na makaa ya mawe yanayopatikana katika vijiji vya Mundindi na Mkomango'mbe.
 
22 November 2024
Mwanza city, Tanzania

MAPOKEZI YA TUNDU LISSU JIJINI MWANZA KAMPENI ZA TAMISEMI 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=c0nXTs3xjfg
Mapokezi ya makamu mwenyekiti CHADEMA bara mheshimiwa Tundu Lissu na mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema - BAVICHA mwalimu John Pambalu balaa, yasimamisha mechi ya Simba SC na wenyeji Pamba FC kwa mùda, ili ...

Hakika chama kongwe kina wajumbe wa fomu za uteuzi wa uchafuzi huku CHADEMA ina umma wa watu waliowachqgua kama chama kinachowakilisha matumaini yao yaliyofelishwa kwa miaka 60 chini ya utawala wa CCM
 
22 November 2024
Dodoma City, Tanzania

Catherine Ruge, Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) - Wanawake mjitokeze kupiga kura TAMISEMI 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=ijx4Vp7SSQk

Katibu mkuu wa BAWACHA akiwa mjini Dodoma mtaa wa Maili Mbili kuwatia moyo wagombea wa mjini Dodoma na kusema ..
 
22 November 2024
Kata ya Itaka
Mbozi, Tanzania

Kijiji cha Itewe Kata ya Itaka Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe mwenyekiti Freeman Mbowe, Joseph Mbilinyi mwenyekiti kanda ya Nyasa wapita kusalimia wanakijiji na kuwaambia wamchague mgombea wa CHADEMA kijiji cha Itewe (video chini):


View: https://m.youtube.com/watch?v=GNWHAdF7aL0

Msafara wa Mwenyekiti wa Chama Taifa ulikuwa umeshafanya Mikutano ya kampeni katika Kata ya Itaka, Kijiji Cha Itewe na Kata ya Halungu Mjini.

Awali mkutano wa kwanza uliokuwa ufanyike katika mji wa Mlowo uliozuiliwa na Polisi pamoja na wenyeji wetu ambao ni Chama Cha ACT Wazalendo kutualika kushiriki kwenye mkutano wa pamoja ila Polisi walikataa na kutawanya wananchi Kwa mabomu ya machozi .

Kabla ya kuwakamata walifuatwa na gari ya Polisi ambayo ilikutana nao njiani na hivyo iligeuza na baada ya mwendo kidogo walikuwa njia imefungwa na gari za polisi ndipo walipofungua milango Kwa nguvu na kuanza kuwashambulia waliokuwa kwenye Magari hayo na kuwakamata Kwa nguvu. Video hii chini:

View: https://m.youtube.com/watch?v=juLQWMrkxLY
Jeshi la Polisi leo tarehe 22 Novemba, 2024 katika Pori la Halungu lililopo Wilaya ya Mbozi wamevamia Msafara na kumkamata Mwenyekiti wa Chama Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe pamoja na Viongozi mbalimbali aliokuwa ameambatana nao .
 
23 November 2024
Ndanto, Rungwe
Mbeya
Tanzania

MAPOKEZI YA FREEMAN MBOWE WILAYA YA RUNGWE TANZANIA 2024 TAMISEMI

View: https://m.youtube.com/watch?v=PeP4KmGBlJM

Ndanto ni kata ya Wilaya ya Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 17,984

Wakaazi wa kijiji cha Nzunda kilichopo Ndanto ni mfano wa kuigwa, ukiwa Nzunda kata ya Ndanto utaona mengi ya kufurahisha.

Kijiji hiki kipo katikati ya kijiji cha Swaya na Ntokela Tarafa ya Ukukwe Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.Kijiji hiki ni nyota inayowaka na kuangaza mafanikio makubwa ambayo ni mfano wa kuigwa nchi nzima.
 
Back
Top Bottom