Pre GE2025 Catherine Ruge: Rais Samia anahofia mageuzi yataiondoa CCM Madarakani

Pre GE2025 Catherine Ruge: Rais Samia anahofia mageuzi yataiondoa CCM Madarakani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
23 November 2024
BREAKING NEWS :FIRE: CHADEMA KANDA YA NYASA

KIJIJI KIZIMA KILIVYOJITOKEZA KUMLAKI FREEMAN MBOWE


View: https://m.youtube.com/watch?v=4i7z4Uk6Il4
Katika ziara yake mikoa ya Songwe na Mbeya viongozi wa kitaifa na kikanda wakiongozwa mheshimiwa mwenyekiti wa CHADEMA mheshimiwa Freeman Mbowe wapokewa na umma wa wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi wa TAMISEMI 2024 ambapo CHADEMA wamebisha hodi na kufanya mikutano zaidi ya kumi kuelekea tarehe 27 November 2024 siku ya jumatano ambapo uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 utafanyika nchi nzima

Video hii ikionesha wananchi wa Ndanto wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya kanda ya Nyasa CHADEMA walivyoupokea msafara wa chama walicho na matumaini nacho kwa ukubwa kabisa kuwavusha kutoka uongozi wa chama dola kongwe kichovu cha CCM
 
25 November 2024
Iringa, Tanzania

Ole Sosopi - Serikali ya Mtaa wako Ndiyo Ikulu Yao, Chagueni Wenyeviti wa mitaa wa CHADEMA


View: https://m.youtube.com/watch?v=_U7XID9XQ2I
CCM Inafanya uhuni ikiwemo kupora uchaguzi na kisha, CCM Inadhani Shida Zenu ni Kanga na T-Shirt

Ole Sosopi kwa ajili hiyo wakataane wenyeviti wa mtaa wa CCM kwa kuchagua wa CHADEMA maana serikali hii ya mtaa, kitongoji na kijiji huhitaji nauli kuifuata Ikulu hii ya mtaa, vijiji na kitongoji tofauti na wizara au ikulu iliyopo Dodoma na Dar es Salaam ..
 
25 November 2024
Kata Luchelele
Nyamagana, Mwanza
Tanzania

Ezekia Dibogo Wenje alivyonguruma mkutano wa CHADEMA kata ya Luchelele akiwanadi wagombea TAMISEMI 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=a-yoX9aoFb4
Hakuna kujitoa, nyani haachiwi shamba la mahindi TAMISEMI 2024..

Ezekia Dibogo Wenje awataka watanzania wa kata ya Luchelele Nyamagama Mwanza Tanzania kuwa wagombea wa CHADEMA hawatawatoza hela kwa ajili ya mihuri, CHADEMA inasimamia haki na matumizi mazuri ya kodi za wananchi, mfano.... msafara wa magari 200 kwa kiongozi wa CCM kama rais ni kawaida, hayo ni matumizi mabaya ya fedha ...
 
22 November 2024
Bukoba, Tanzania

Wagombea wetu wakishinda 2024 halafu wakafanana na hulka za CCM kuuza mihuri, tutawaengua


View: https://m.youtube.com/watch?v=Qom1wYuArls
Chief Adronicus Kalumuna wa CHADEMA amesema hilo ndilo agano letu, tutawapima kila baada ya miezi 3 na wananchi watashirikishwa kupima utendaji wa wajumbe, wenyeviti wa mitaa na vijiji ili kuona wanatekeleza ahadi zetu kikamilifu kwa raia wote ...
 
Back
Top Bottom