CC YA CCM: Hata kama tozo zimejenga vituo vya afya 234 na shule za Sekondari 214 bado wananchi wana hoja, zitazamwe upya

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029

CCM yatoa maelekezo kwa Serikali kuhusu tozo,Asante CCM kwa kulituliza Taifa,​

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) imeielekeza Serikali kuchukua ushauri wa wananchi kuhusu tozo sambamba na kujielekeza katika kubana matumizi ya serikali na kutanua wigo wa kodi.

CCM yatoa maelekezo kwa Serikali kuhusu tozo

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi Septemba 8, 2022 jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumzia maazimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichokaa jana Septemba 8, 2022 kikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

CCM imeingilia kati tozo siku chache baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba pamoja na mawaziri wenzake kujitokeza kuzungumzia tozo wakati kukiwa na malalamiko ya wananchi na wadau wengine kuhusu tozo hizo.

Shaka amesema Kamati Kuu imewapongeza Rais Samia na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwa kazi nzuri wanayoifanya na pia kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi.

Amesema Kamati Kuu inatambua mafanikio yaliyofikiwa kutokana na mapato ya tozo kama vile ujenzi wa vituo vya afya 234 pamoja na sekondari 214. Hata hivyo, imeielekeza Serikali kutazama hali halisi na kuchukua maoni ya wananchi kuhusu tozo za miamala ya kielektroniki.

"Kamati Kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa umeielekeza Serikali kutazama hali halisi na kuchukua hatua stahiki kuhusu maoni na ushauri wa wananchi kuhusu tozo.

"Kamati Kuu ya CCM imeielekeza Serikali kufikiria na kujielekeza katika kubana matumizi ya Serikali lakini pia kuendelea kujenga mazingira rafiki na wezeshi ili kujenga uchumi imara unaozalisha kwa lengo la kutanua wigo wa kodi pamoja na kubuni vyanzo vipya vya kodi ili kuwa na viwango na mfumo rafiki wa kodi kwa kila mmoja," amesema Shaka.

Shaka amewataka wasaidizi wa Rais Samia washuke chini kwa wananchi ili kusikiliza shida zao sambamba na kujua hali halisi ya maisha yao. "Tunafuatilia mwenendo na uwajibikaji wa wateule wote wa Rais. Chama ndiyo mwenye mali, kwa hiyo lazima tuimamie serikali," amesema Shaka wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini hapa.
 
CCM chama cha wanyonge na walalahoi kamwe wasingekubali Wananchi waendelee kulalamika,

VIVA CCM VIVA

VIVA SAMIA VIVA

VIVA KINANA VIVA

VIVA CHOGOLO VIVA

VIVA SHAKA VIVA

VIVA......... VIVA
 
Natamani nione hii orodha ya hivi vituo vipya vya afya na hizo sekondari mpya zilizojengwa na tozo mwenye kujua aorodheshe hapa
 
Waliopitisha hizo tozo wakiongozwa na m/kiti ndo hao hao wa waliokaa kikao na kujifanya wanakuja na maamuzi. Hapo wameshaona wamekusanya mpunga wa kutosha halafu wanatuigizia eti chama kimewaagiza. Wizi mtupu!
 
Hivi kuchukua pssa zako mwenyewe ulizoziifadhi bank baada ya kukatwa kodi za mapato, ni taxable transaction? Aione: Mwigulu

Idea haikua mbaya, lazima tuchangie maendeleo ya nchi yetu. Ndiyo maana tuna panda miti ili si kwamba itufaidishe in our life time, but also the coming generations
 
Natamani nione hii orodha ya hivi vituo vipya vya afya na hizo sekondari mpya zilizojengwa na tozo mwenye kujua aorodheshe hapa
Mkopo wa fedha wa shilingi Trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) na kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya Korona nchini Tanzania ndio ulitumika kwenye ujenzi wa madarasa.

Kwani si mwaka jana tu walitangaza wenyewe na sasa wanataka kutufanya tumesahau!
 
CCM chama cha wanyonge na walalahoi kamwe wasingekubali Wananchi waendelee kulalamika,

VIVA CCM VIVA

VIVA SAMIA VIVA

VIVA KINANA VIVA

VIVA CHOGOLO VIVA

VIVA SHAKA VIVA

VIVA......... VIVA
AIBU KUITWA MNYONGE NDANI YA NCHI HURU
 
Waliopitisha hizo tozo wakiongozwa na m/kiti ndo hao hao wa waliokaa kikao na kujifanya wanakuja na maamuzi. Hapo wameshaona wamekusanya mpunga wa kutosha halafu wanatuigizia eti chama kimewaagiza. Wizi mtupu!
Umewaheshimu sana hiyo sentensi ya mwisho. Siyo tu wizi bali us
 
CCM yatoa maelekezo kwa Serikali kuhusu tozo,Asante CCM kwa kulituliza Taifa,​

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) imeielekeza Serikali kuchukua ushauri wa wananchi kuhusu tozo sambamba na kujielekeza katika kubana matumizi ya serikali na kutanua wigo wa kodi.

CCM yatoa maelekezo kwa Serikali kuhusu tozo

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) imeielekeza Serikali kuchukua ushauri wa wananchi kuhusu tozo sambamba na kujielekeza katika kubana matumizi ya serikali na kutanua wigo wa kodi.

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi Septemba 8, 2022 jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumzia maazimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichokaa jana Septemba 8, 2022 kikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

CCM imeingilia kati tozo siku chache baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba pamoja na mawaziri wenzake kujitokeza kuzungumzia tozo wakati kukiwa na malalamiko ya wananchi na wadau wengine kuhusu tozo hizo.

Shaka amesema Kamati Kuu imewapongeza Rais Samia na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwa kazi nzuri wanayoifanya na pia kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi.

Amesema Kamati Kuu inatambua mafanikio yaliyofikiwa kutokana na mapato ya tozo kama vile ujenzi wa vituo vya afya 234 pamoja na sekondari 214. Hata hivyo, imeielekeza Serikali kutazama hali halisi na kuchukua maoni ya wananchi kuhusu tozo za miamala ya kielektroniki.

"Kamati Kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa umeielekeza Serikali kutazama hali halisi na kuchukua hatua stahiki kuhusu maoni na ushauri wa wananchi kuhusu tozo.

"Kamati Kuu ya CCM imeielekeza Serikali kufikiria na kujielekeza katika kubana matumizi ya Serikali lakini pia kuendelea kujenga mazingira rafiki na wezeshi ili kujenga uchumi imara unaozalisha kwa lengo la kutanua wigo wa kodi pamoja na kubuni vyanzo vipya vya kodi ili kuwa na viwango na mfumo rafiki wa kodi kwa kila mmoja," amesema Shaka.

Shaka amewataka wasaidizi wa Rais Samia washuke chini kwa wananchi ili kusikiliza shida zao sambamba na kujua hali halisi ya maisha yao. "Tunafuatilia mwenendo na uwajibikaji wa wateule wote wa Rais. Chama ndiyo mwenye mali, kwa hiyo lazima tuimamie serikali," amesema Shaka wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini hapa.
Kabla ya yote tunataka kujua hivyo vituo vya afya 234 vilipojengwa au vinapojengwa KWa kutaja na kata hivyo na shule,
Jedwali chini linaonesha mpaka 2021 to 2022 March ni vituo 34 tu vya afya vilisajiliwa, Sasa hivyo vituo 234 vimejengwa ndani ya miezi 6 ?
 
Attachments

  • downloadfile.png
    downloadfile.png
    69.7 KB · Views: 8
Hawa hawasikii hata uwaambie nini
Bundle limelalamikiwa miaka nenda rudi zaidi ya kupanda bei haijawahi kupungua
Kwenye hili nikuombe CCM ipitie na kuangalia hii,
 
Waziri Mkuu ana v8 la m450 plus gharama ya msafara anaekushangaa chumba cha milioni 11.
Kwann asianze kushangaa gharama za msururu wa msafara wake
 
Watanzania tulilogwa. Hivi mtu unatofautishaje chama na serikali katika mazingira ya hapa kwetu pamoja na mfumo wa kiutawala. Waliopitisha tozo ni wale wale, wanaojiomba kusikiliza wananchi ni wale wale, wanaolifanyia kazi lalamiko la wananchi ni wale wale. Yarabi Mola utuangalie na sisi wadanganyika jamani
 
Back
Top Bottom