CC YA CCM: Hata kama tozo zimejenga vituo vya afya 234 na shule za Sekondari 214 bado wananchi wana hoja, zitazamwe upya

CC YA CCM: Hata kama tozo zimejenga vituo vya afya 234 na shule za Sekondari 214 bado wananchi wana hoja, zitazamwe upya

Natamani nione hii orodha ya hivi vituo vipya vya afya na hizo sekondari mpya zilizojengwa na tozo mwenye kujua aorodheshe hapa
Hata Mimi naitaka, aisee watuwekee na mahali Kama ni kata flani n.k

Then tutaanza trace kimoja kimoja Kama ni kituo Cha afya na shule hivyo hivyo,

Nchi kubwa hii Rais anaweza kuwa anapelekewa makaratasi tu kumbe huko chini ,hamna kinachoendanda na anachoambiwa, Sasa tupe data sisi tutavitafua,

Kama ni shule tutauliza imejengwa lini ? Kama ni kipindi Cha Serikali ya tono ,tunakiondoa, Kama ni serikali ya 6 kinabaki mpaka idadi itimie
 
Acheni blah blah!

Alieanzisha ni mwana ccm aliepitishwa na cc ya CCM kuwa hapo alipo;

Mngekuja na matamko haya;-

"Rasimu ya warioba irudi mezani SASA iwe katiba mpya"

"Mzee warioba ajumuishwe kwenye kikosi kazi cha mkandala mchakato wa katiba mpya ukamilike"
Kweli Watanzania hatuna jema
 
Kabla ya yote tunataka kujua hivyo vituo vya afya 234 vilipojengwa au vinapojengwa KWa kutaja na kata hivyo na shule,
Jedwali chini linaonesha mpaka 2021 to 2022 March ni vituo 34 tu vya afya vilisajiliwa, Sasa hivyo vituo 234 vimejengwa ndani ya miezi 6 ?
Mkuu vituo vingine wamejengea matumboni mwao, ukiona tumbo kubwa limefunikwa shati la kijani jua ni zahanati/kituo Cha afya hicho kinapita.

Ccm imefika sehemu masikio yameziba na mbaya zaidi macho nayo yalishakufa siku nyingi. Tukichelewa Hawa watu wanatumaliza tunaona.

Inaumiza Sana.
 
Hakuna atakayekupatia hiyo orodha ya majina ya sekondari,primary schools au hospitali.Watakutajia idadi na kiasi cha mabilioni hewa lakini vilipo hapa Tanzania,hilo sahau ni siri ya nchi.
Natamani nione hii orodha ya hivi vituo vipya vya afya na hizo sekondari mpya zilizojengwa na tozo mwenye kujua aorodheshe hapa
 
Hakuna atakayekupatia hiyo orodha ya majina ya sekondari,primary schools au hospitali.Watakutajia idadi na kiasi cha mabilioni hewa lakini vilipo hapa Tanzania,hilo sahau ni siri ya nchi.
😂😂🤣 Sio kweli bhana, Serikali itatuwekea nasi tuvitembelee, Ili kupongeza inapobidi
 
Pamoja na hayo .hii mitandao ya simu ipunguze makato na kuacha mbambamba zilizo na msingi.eti hawa voda wanasema wamepata hasara??? Wanapataje hasara wakati wanajikusanyia mabilion ya pesa kwenye makato na bundle.
 
Natamani nione hii orodha ya hivi vituo vipya vya afya na hizo sekondari mpya zilizojengwa na tozo mwenye kujua aorodheshe hapa
Infinsi .pamoja na hayo zimeleta ahuen katika bei za mafuta
 
😂😂🤣 Sio kweli bhana, Serikali itatuwekea nasi tuvitembelee, Ili kupongeza inapobidi
Hatukutakiwa kuomba orodha,kama miradi ni halali na imelenga wananchi wenye nchi taarifa kama hizo siyo za kuombea bali zilitakiwa ziwe zinapatikana kwa njia za wazi.Sasa hapa Tanganyika si walifuta mtandaoni kila kitu kilichohusu Rasimu ya Katiba ya Wananchi wa Tanzania iliyoandikwa na Tume ya Jaji Warioba?
Hata hii habari haitolewi kwa Wananchi ili kuwafumba macho.
 
Kweli mkuu umeongea maneno kuntu
 
CCM yatoa maelekezo kwa Serikali kuhusu tozo,Asante CCM kwa kulituliza Taifa,​

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) imeielekeza Serikali kuchukua ushauri wa wananchi kuhusu tozo sambamba na kujielekeza katika kubana matumizi ya serikali na kutanua wigo wa kodi.

CCM yatoa maelekezo kwa Serikali kuhusu tozo

View attachment 2350888

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) imeielekeza Serikali kuchukua ushauri wa wananchi kuhusu tozo sambamba na kujielekeza katika kubana matumizi ya serikali na kutanua wigo wa kodi.

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi Septemba 8, 2022 jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumzia maazimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichokaa jana Septemba 8, 2022 kikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

CCM imeingilia kati tozo siku chache baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba pamoja na mawaziri wenzake kujitokeza kuzungumzia tozo wakati kukiwa na malalamiko ya wananchi na wadau wengine kuhusu tozo hizo.

Shaka amesema Kamati Kuu imewapongeza Rais Samia na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwa kazi nzuri wanayoifanya na pia kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi.
View attachment 2350889
Amesema Kamati Kuu inatambua mafanikio yaliyofikiwa kutokana na mapato ya tozo kama vile ujenzi wa vituo vya afya 234 pamoja na sekondari 214. Hata hivyo, imeielekeza Serikali kutazama hali halisi na kuchukua maoni ya wananchi kuhusu tozo za miamala ya kielektroniki.

"Kamati Kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa umeielekeza Serikali kutazama hali halisi na kuchukua hatua stahiki kuhusu maoni na ushauri wa wananchi kuhusu tozo.

"Kamati Kuu ya CCM imeielekeza Serikali kufikiria na kujielekeza katika kubana matumizi ya Serikali lakini pia kuendelea kujenga mazingira rafiki na wezeshi ili kujenga uchumi imara unaozalisha kwa lengo la kutanua wigo wa kodi pamoja na kubuni vyanzo vipya vya kodi ili kuwa na viwango na mfumo rafiki wa kodi kwa kila mmoja," amesema Shaka.

Shaka amewataka wasaidizi wa Rais Samia washuke chini kwa wananchi ili kusikiliza shida zao sambamba na kujua hali halisi ya maisha yao. "Tunafuatilia mwenendo na uwajibikaji wa wateule wote wa Rais. Chama ndiyo mwenye mali, kwa hiyo lazima tuimamie serikali," amesema Shaka wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini hapa.
Naona waziri wa tozo saiz kiti hakikaliki, ANAPUYANGA Kila Mahali akijipa hata KAZI zisomhusu.
 
Back
Top Bottom