CC YA CCM: Hata kama tozo zimejenga vituo vya afya 234 na shule za Sekondari 214 bado wananchi wana hoja, zitazamwe upya

Natamani nione hii orodha ya hivi vituo vipya vya afya na hizo sekondari mpya zilizojengwa na tozo mwenye kujua aorodheshe hapa
Hata Mimi naitaka, aisee watuwekee na mahali Kama ni kata flani n.k

Then tutaanza trace kimoja kimoja Kama ni kituo Cha afya na shule hivyo hivyo,

Nchi kubwa hii Rais anaweza kuwa anapelekewa makaratasi tu kumbe huko chini ,hamna kinachoendanda na anachoambiwa, Sasa tupe data sisi tutavitafua,

Kama ni shule tutauliza imejengwa lini ? Kama ni kipindi Cha Serikali ya tono ,tunakiondoa, Kama ni serikali ya 6 kinabaki mpaka idadi itimie
 
Kweli Watanzania hatuna jema
 
Mkuu vituo vingine wamejengea matumboni mwao, ukiona tumbo kubwa limefunikwa shati la kijani jua ni zahanati/kituo Cha afya hicho kinapita.

Ccm imefika sehemu masikio yameziba na mbaya zaidi macho nayo yalishakufa siku nyingi. Tukichelewa Hawa watu wanatumaliza tunaona.

Inaumiza Sana.
 
Hakuna atakayekupatia hiyo orodha ya majina ya sekondari,primary schools au hospitali.Watakutajia idadi na kiasi cha mabilioni hewa lakini vilipo hapa Tanzania,hilo sahau ni siri ya nchi.
Natamani nione hii orodha ya hivi vituo vipya vya afya na hizo sekondari mpya zilizojengwa na tozo mwenye kujua aorodheshe hapa
 
Hakuna atakayekupatia hiyo orodha ya majina ya sekondari,primary schools au hospitali.Watakutajia idadi na kiasi cha mabilioni hewa lakini vilipo hapa Tanzania,hilo sahau ni siri ya nchi.
😂😂🤣 Sio kweli bhana, Serikali itatuwekea nasi tuvitembelee, Ili kupongeza inapobidi
 
Pamoja na hayo .hii mitandao ya simu ipunguze makato na kuacha mbambamba zilizo na msingi.eti hawa voda wanasema wamepata hasara??? Wanapataje hasara wakati wanajikusanyia mabilion ya pesa kwenye makato na bundle.
 
Natamani nione hii orodha ya hivi vituo vipya vya afya na hizo sekondari mpya zilizojengwa na tozo mwenye kujua aorodheshe hapa
Infinsi .pamoja na hayo zimeleta ahuen katika bei za mafuta
 
😂😂🤣 Sio kweli bhana, Serikali itatuwekea nasi tuvitembelee, Ili kupongeza inapobidi
Hatukutakiwa kuomba orodha,kama miradi ni halali na imelenga wananchi wenye nchi taarifa kama hizo siyo za kuombea bali zilitakiwa ziwe zinapatikana kwa njia za wazi.Sasa hapa Tanganyika si walifuta mtandaoni kila kitu kilichohusu Rasimu ya Katiba ya Wananchi wa Tanzania iliyoandikwa na Tume ya Jaji Warioba?
Hata hii habari haitolewi kwa Wananchi ili kuwafumba macho.
 
Kweli mkuu umeongea maneno kuntu
 
Naona waziri wa tozo saiz kiti hakikaliki, ANAPUYANGA Kila Mahali akijipa hata KAZI zisomhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…