hili suala lataka tafakuri na uangalifu wa hali ya juu vinginevyo tutakula wa chuya.
Kumpata mkuu wa serikali na nchi wa dhahabu ambaye ana uwezo wa kukidhi angalau 60% ya mahitaji na matarajio ya wananchii siyo jambo la mchezo, ni ngumu. US, UK wana haha na kuyumba kwelikweli kumpata kiongozi wa ndoto yao, Urusi waliyumba kwa decades kadhaa kabla ya kuibuka kwa Putin.
Kuna baadhi ya nchi hazijawahi kuwapata kabisa.
mara nyingi viongozi wa dhahabu wakiwa madarakani upingwa sana. Wakiwa kwenye vyama vya upinzani uwekewa vikwazo sana. Siyo kwamba nchi inakuwa haina watu wenye sifa ila kumpata mwenye sifa ambaye yupo katika mazingira ya kuweza kuchaguliwa kuwa mkuu wa serikali ndio changamoto. Kiongozi wa dhahabu ni mtu mwenye vision na mikakati, sahihi, mwenye nia njema kwa jamii, anayeweza kuishinda nafsi yake na anayeweza kufanya reform muhimu zinazoweza kuifanya vision yake iwe kweli.
Katika mazingira yetu ya sasa ndani na nje ya mfumo ni vigumu kwa mtu kuweza kusema pasipo kupepesa macho wala mashaka kuwa fulani ana uwezo wa kukibeba kijiti kwa mafanikio na watu wengi wakakubaliana naye. tunachoweza kufanya ni kubahatisha tu. ni mtazamo wangu na naweza kukosolewa. tukumbuke kuwa nyerere alipotaka kung'atuka mwaka 1980 ilisumbua sana kumpata mbadala wake hadi akaghairi, mwinyi alipokuwa anaondoka ilikuwa tabu zaidi kupata mbadala wake.
Viongozi hawa ni baadhi tu ya mifano ya viongozi wa dhahabu ambao mataifa yao yanawakumbuka vizavi na vizazi ingawa nao pia walikuwa na mapungufu yao (queen Victoria, Margaret thatcher, Winston Churchill, Yasser Arafat, Sheikh Rashid ibn Saeed Al Maktoum, Anthony Charles Lynton Blair, Angela Merkel, Kambarage, Ho Chi Minh, Nguyễn Văn Linh, Deng Xiaoping, Mao Zedong, Franklin D. Roosevelt, Abraham Lincoln, Lee Kuan Yew, Suharto n.k) siku mungu akinijaria msukumo na muda nitabainisha vigezo vya viongozi hawa kutambulika kuwa ni wa kipekee.