CCM fikirieni namna ya kumuenzi Marehemu Kapteni John Komba

CCM fikirieni namna ya kumuenzi Marehemu Kapteni John Komba

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
3,192
Reaction score
7,112
Nimefikiria jinsi alivyotumika kuking'arisha chama kwa utunzi na nyimbo zake hasa katika nyakati ngumu za uchaguzi.
Huyu nilianza kumshuhudia tangu enzi za Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Hata baada ya kufariki bado nyimbo zake zimetumika katika mikusanyiko ya chama na kwenye kampeni.
Inawezekana kuna sehemu alikengeuka lakini bado haiondoi mchango wake mkubwa ktk chama.

Kama aliacha watoto na kama wapo waliopata elemu ya juu basi chama kiangalie namna ya kumuenzi.

Wengine sisi tukiwa wadogo tuliipenda ccm sababu tu ya nyimbo alizoimba Komba.
Kuna watoto wengi tu wa viongozi wa zamani ambao chama na serikali kimewakumbuka , lakini ukipima michango yao kwa chama wengi hawafikii hata robo ya mchango wa John Komba.

Ninaamini Mama yetu akikumbushwa hili atalipokea kwa mikono miwili. Hata Dr Nchimbi akikumbushwa hili atalichukuwa haraka
 
Back
Top Bottom