CCM, gesi haiondoki Mtwara piga ua

Kweli mkuu kule watu wanauza utu kwa buku
 
me wa kaskazini na nitakusapoti baadhi ya mambo.ni kweli kulikuwa hakuna umuhimu wa kusafirisha gesi kutoka kusini kuja dar kwa ajili ya kuzalisha umeme badala yake wangejenga mitambo huko huko lakini hapa kuna tatizo moja,watapata wapi 10 pasenti kutoka kwenye mikataba?naunga mkono kusafirisha gesi kuja dar na mikoa mingine kwa matumizi mengine kama ya nyumbani etc.so kazeni umeme uzalishwe huko huko mtwara!!
 
THE BIG SHOW, SHERRIF ARPAIO,

..mimi nadhani mngepigania umeme usambazwe wilaya zote ktk mikoa ya kusini.

..pia suala la ELIMU litafutiwe ufumbuzi ktk mikoa ya kusini.

..elimu ina matatizo sana maeneo ya kusini. kuna maeneo waalimu wanabakwa, kwingine kuna migogoro ya udini, halafu uchanganye na suala la utoro na wazazi kuozesha watoto wa kike.

..bila kutatua matatizo ktk sekta ya elimu wananchi wa kusini hawawezi kufaidika na uchimbaji wa gesi ktk maeneo yao.

..pia kuwe na mfumo mzuri zaidi wa manunuzi ya mazao kama Korosho na mengine yanayopatikana huko.

..Shiyanga, Geita, Tabora, wana migodi ya dhahabu lakini hali zao hazina tofauti na wakati hawana migodi hiyo. kwa msingi huo hoja ya wananchi wa kusini inapaswa kujumuisha mambo mengi sana na siyo kulazimisha tu "gesi haitatoka Mtwara."
 
Last edited by a moderator:

kwahiyo hayo mabomba ya gesi wanayoweka mtayalipua ama?
 



ushauri wako una uhalisia joka kuu

na tunachotaka wana mtwara ni mabadiliko ya kanda hii hasa hasa kutokana na rasimali zinazotoka huku,wilaya ya tandahimba ni ya pili kitaifa kwa kuingiza pato la kodi kila mwaka,,na hii nikutokana na ushuru wa zao la korosho,lakini ukiangalia hali za maisha ya watu wa eneo husika inatia hasira sana

enough is enough,kwa sasa imetosha
 
Jana tarehe 21/12/12 katika kikao cha rcc Mtwara mh, kanali mstaafu Joseph Simbakalia ameisoma live barua iliyoandikwa na vyama vya upinzani kwa ujumla kwamba kutakuwa na maandamano na anaombwa kuyapokea tarehe 27/12/12 kuhusu suala hil. Mbele ya mawaziri Hawa Ghasia na John Mkuchik, mkuu wa Mkoa ameuita mchakato huu ni upumbavu na amewahimiza wana Mtwara kwenda shule kwani elimu ndio itakao waokoa, alisema even if gesi ikibaki Mtwara what are u going to do with it kama ninyi ni shuleless na pia akasema mkikomaa sana gesi inaweza kuondokea juu kwa juu baharini huko huko na msipate kitu. Mheshimiwa alijitahidi kueleza fulsa zitazopatikana ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda kwa kuanza na kiwanda cha cement cha dangote.hata hivyo amesema waandamanaji wasijisumbue siku hiyp kwanza hatakuwapo.
 
kwahiyo hayo mabomba ya gesi wanayoweka mtayalipua ama?


ikibid tutachuku ushauri huu wako,,

na hata kwa sangoma tutaenda,tutawatumia hata kina zitto kwenda kigoma kuchukua utaalam huo,,

hata kutangaza uhuru wetu tutatangaza tuh
gesi kwanza,mtwara kwanza

siasa baadae
 
watu washaamka sasa,,pia washachoka kwa utumwa wao

wasubiri 2015

Le Big show heshima mbele kwanza, nashukuru kwa wewe na wananchi wenzako kwa kuonyesha concern kwenye issue ya gas ingawa nina wasiwasi kuna makosa ya kiufundi mnaweza kuyafanya halafu mkajikuta hata mkipewa forum ya kusikilizwa mnachotaka kifanyike mkajikuta mnaongea vitu ambavyo vikiwa implemented mkajikuta back to square one. viwanda vimejengwa na hamna ajira mlizotegemea.

Nchi hii ina tatizo kubwa la management ya natural resources and distribution of national cake, ni tatizo mtambuka, ku-break cycle yake inahitaji ulielewe vizuri tatizo in totality ili u-identify entry point ambayo hata kama haitakuwa na significant impact on breaking the cycle, at least iwe most beneficial to the impoverished community.

Ukiangalia issue ya gas kama zilivyokuwa kwenye natural resource nyingine kama madini ambayo exploitation yake ni capital intensive, watu wameshachukua 10% zao na kuziweka uswisi lakini kibaya zaidi ni kuwa kuna udhaifu mkubwa sana wa kumonitor cost anazo-inccur investor as upfront cost and operational cost throughout all phases of the project. hili tumeliona kwa pan african energy jinsi walivyoinflate cost zao na tutaliona tena kwenye hizo project zitakazofuata.

Nilichokuwa nashauri ni kutafuta washauri hata kwenye forum kama humu JF ambao wamefamiliarize na case kama hizi watupe ushauri, given mazingira, sheria na matatizo tulio nayo, where best can we start to break the cycle. tunaweza kufikiri kujenga viwanda ni strong approach, kumbe the best ni kudeal na gas policy. Manake given umasikini na illitracy level tuliyo nayo, ili hii gas imnufaishe mwananchi kule mtwara na kwingineko inahitaji more than honest government nothing short of saint government. Mimi si mtaalamu wa haya mambo (academically) lakini nina interest ya kuyasoma in future.
 

THE BIG SHOW,

..nadhani korosho ndiyo mkombozi wa wananchi wa kusini.

..kwanza, kilimo hicho kinahusisha wananchi wengi wa huko.

..pili, mapato ya korosho yanaingia moja kwa moja mifukoni mwa wananchi.

..mapato ya gesi yanakwenda serikalini kwanza, halafu ndiyo halmashauri za wananchi zipata gawio.

..mimi naunga mkono madai yenu kuhusu gesi, lakini wakati nadhani u have to go a step further.
 


tumeskia kuhusu hicho kikao,lakini jiulize watu wote ni wajinga hadi wafikie hatua ya kukaidi suala hilo kama lina manufaa??ukwe;i ni kwamba rasimu ya sheria ya gesi na vipaombeele vyake kwa ujumla haiko wazi,na hili suala limechukuliwa kisiasa zaid,gesi iko mtwara sherehe za uzinduzi wa bomba unafanyia dsm ikiwa na mantiki ipi??kama wanaona kuna fursa zipo kwanini wasiwaeleze wananchi wanasubiri hadi zomea zomea ifike kisha ndiyo waje kuwaplease raia??

Watu wa mtwara sio vihiyo kwa kiasi hiko,na sio kwamba wamekosa shule kwa kiwango cha chini kiasi hiko,kila kitu kiko wazi,wanasiasa wameingiza interest zao pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…