CCM, gesi haiondoki Mtwara piga ua

Nakubaliana na wewe, lakini watu wenye kuangalia hapa watasistiza corporate social responsibility. Mfano, inaweza kuwepo clause kwenye contract wanazoingia wenye makampuni kufanya yafuatayo.
  1. Kuweka idadi ya ajira (za chini na kati kipaumbele kwa wakazi wa Mtwara na Lindi -laziima kusimamia. Hii inaendana na merits. Kama hakuna wasomi wa kufill such positions ndo imekula kwao, itabidi watafute mikoa jirani (obviously Dar comes first)
  2. Kuandaa mikataba na vikundi uzalishaji mali (mfano mayai, mboga mboga na hata mchele). Bidhaa zote hizo zitokee maeneo hayo. Endapo wananchi hawana uwezo wa kuzalisha bidhaa bora, makampini na serikali wawajengee uwezo na kuweka wataalam kuwasaidia kuzalisha kwa kiwango/ubora na wingi unaohotajika. Kama kwa sasa hawapo, lazima kuwepo na short, medium and long term strategies kuwaendeleza hao watu kuchukua nafasi kama local producers and suppliers of such materials
  3. Huduma za jamii -maji, umeme, afya, elimu na barabara ziendelezwe na kujenga fursa za kuuchumi kwa watu kujikwamua


Sidhani kama sahihi kumpa mtu first priority ambaye hayuko tayari hata kulipia huo umeme. Nadhani kwa principle za biashara bidhaa huwa zinakwenda katika sehemu yenye soko.
 
Tatizo la Mtwara na Lindi linachangiwa na aina ya viongozi wa kisiasa tulionao. Kwa ujumla kwa Lindi na Mtwara tatizo lipo kwa Membe,Hawa Ghasia,Mkuchika,Anna Abdalah na Mkapa. Hivi kama kweli wote hawa wangesimama kidete kusimamia gesi isondoke Mtwara isingewezekana? Nawaomba wananchi wote wa Lindi/Mtwara kuwaadabisha jamaa hawa kwa kutowachagua katika uchaguzi ujao kwani hawana uzalendo.
 

thank u so much

thank you a lot GREAT THINKER
 

Kimsingi naunga mkono hoja yako ya gesi kutosafirishwa kutoka Mtwala kwenda Bagamoyo (hapa mkwele anatumia gia ya kwamba wanataka kusupply gesi Kenya kupitia Tanga), Kenya wamegundua gesi ya kutosha na wanajipanga vilivyo katika uchorongaji (exploration), Sera, uzalishaji na mwisho usambazaji. sisi tunakurupuka kila jambo na tuliaza vizuri katika utafiti na uchorongaji enzi za Mwalimu, alivyokufa tu eeh..... malizia!. Uganda pia wako fiti kuliko maelezo katika gesi and oil, EA Tanzania ndiyo ***** tu katika kila jambo.

Lakini hapo kwenye bold/blue ... unamshukuru mkapa kwa kukuachia barabara. Wembe ni ule ule... wakwele watamkumbukaje Kiwet?! Ila kazidi, Barabara, mipango ya reli, Badari, uwanja wa ndege,...eh!? Nami nikiwa Rais wa KG nitawajengea wanananchi wa eneo langu bomba la mafuta kutoka Dar. Eh.. ndo mpango kwenu kwanza wengine acha wasange meno, watajipanga nao baadaye! Chukua chako mapema!
 
Kwa sasa nchi inapita kipindi kigumu kutokana na migogoro ya uwekezaji ktk sekta ya madini,(mafuta na gesi)ardhi,viwanda n.k.Tatizo kubwa likiwa manufaa kidogo wanayopata Wananchi toka kwa uwekezaji huo.Hofu iliyotanda ni kuwa vigogo wanatumia mikataba feki kujinufaisha na uwekezaji huo.Wananchi wa mikoa ya kusini hasa Mtwara wameanza kulalamikia hatua ya kusafirisha gesi toka huko na kuileta "TANZANIA" badala ya kui-process kule na kusafirisha tu umeme kuuleta "TANZANIA".maana wanahisi watapoteza fursa nyingi za kimaendeleo na hivyo kuendeleza mfumo wa kubaki kama eneo duni kimaendeleo.
Wanajamii naomba tujadili watu wa Mtwara tunapaswa kuungwa mkono kwa hofu yetu au kupingwa kama baadhi ya watu wanavyobeza uamuzi wetu wa kukataa kusafirisha gesi toka kwetu kuja "TANZANIA"?
 
kwa wana mtwara,gas ni ki2 ambacho mbali na manufaa ya moja kwa moja kamavile ushuru,ajira na hata kuendelea uwekezaji wa ndani,hata biashara.kwakweli ni ha2a mojawapo ya kuutapeli mji huo.na zaidi hata mbunge wao ndani ya kikao cha bunge ilisimama na kusaliti jimbo lao kwa kusema gas kuja dar ni muhimu na ni sahihi,huku mb wa kilwa mr,bungara akibishana nae kuwa sio sahihi.mimi nimekaa mtwara kwa miaka minne sasa maendeleo yake kwa kila mwaka hubadilika na ni kwa speed kubwa na influence kubwa ni vyuo vilivyopo,pamoja na gas ya mnazi bay(msimbati).MTWARA KWANZA NA VYAMA BAADAE KWA MASILAHI YA TAIFA.
 

Mabomba ya gesi yameshawasili. Mkwara wenu haujasaidia mkuu
 

Imekuwaje siku hizi ghafla unaifagilia CCM?
Sasa nimeamini ule usemi 'everybody has a price '
 
Gesi ya Mtwara ishafika Kinyerezi Dar. Bigshow na wenzake wana ntwara walicheza mdumange wa Tanga ndani ya Mdundiko wa Pwani wakaacha kucheza sindimba.
Ha ha ha haaaaa!
 
Gesi ya Mtwara ishafika Kinyerezi Dar. Bigshow na wenzake wana ntwara walicheza mdumange wa Tanga ndani ya Mdundiko wa Pwani wakaacha kucheza sindimba.
Ha ha ha haaaaa!

Bigshow mwenyewe kageuka CCM siku hizi
 
daaaah! inasikitisha huyu big show sasa ndie CCM kindakindaki.
 

mkuu tukiangalia hili swala kiuchumi kuna kitu kinaitwa opportunity cost, hiyo gesi mkiingangania huko mtwara italazimu serikali ianze upya tena kujenga viwandakwa fedha nyingi mno, hii gesi kwenda bagamoyo tukumbuke ya kwamba bagamoyo kutakua na bandari kubwa sana kitu kitachochangia bagamoyo uwe mji mkubwa na kuwa na biashara nyingi zinazohitaji umeme ili kulipatia taifa mapato ambayo huenda yakaja kuisaidia hata mtwara. remember chochote kilichomo ndani ya tz ni kwa manufaa ya watanzania wote
 
poleni wana mtwara yani mnalalamika wakati tayari mitambo ilishajengwa Dar... na waliishajaribu kusafirisha gesi wakafanikiwa sijui sasa mnalalamika nini ..... hata kama gesi ingebaki mtwara ndio mngeifanyia nini sasa? umeme wa gesi si kwa ajili yenu? kinachoangaliwa zaidi ni soko la hiyo gesi wala haina haja ya kulalama.
 
Wangesema Korosho haitoki Mtwara ningewaelewa kabisa lakin gas ya Mungu wanaizuiaje ?.Kibaya zaidi gas nyingi inavunwa kwenye bahari kuu sasa sijui bahari kuu nayo ni Mtwara ?Watu huko kusini wamejaa ujinga sana ndio maana walikuwa wakiliwa na Simba hadi karne ya 20.


Imekuwaje siku hizi ghafla unaifagilia CCM?
Sasa nimeamini ule usemi 'everybody has a price '
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…