BUBE
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 845
- 254
Nakubaliana na wewe, lakini watu wenye kuangalia hapa watasistiza corporate social responsibility. Mfano, inaweza kuwepo clause kwenye contract wanazoingia wenye makampuni kufanya yafuatayo.
- Kuweka idadi ya ajira (za chini na kati kipaumbele kwa wakazi wa Mtwara na Lindi -laziima kusimamia. Hii inaendana na merits. Kama hakuna wasomi wa kufill such positions ndo imekula kwao, itabidi watafute mikoa jirani (obviously Dar comes first)
- Kuandaa mikataba na vikundi uzalishaji mali (mfano mayai, mboga mboga na hata mchele). Bidhaa zote hizo zitokee maeneo hayo. Endapo wananchi hawana uwezo wa kuzalisha bidhaa bora, makampini na serikali wawajengee uwezo na kuweka wataalam kuwasaidia kuzalisha kwa kiwango/ubora na wingi unaohotajika. Kama kwa sasa hawapo, lazima kuwepo na short, medium and long term strategies kuwaendeleza hao watu kuchukua nafasi kama local producers and suppliers of such materials
- Huduma za jamii -maji, umeme, afya, elimu na barabara ziendelezwe na kujenga fursa za kuuchumi kwa watu kujikwamua
Sidhani kama sahihi kumpa mtu first priority ambaye hayuko tayari hata kulipia huo umeme. Nadhani kwa principle za biashara bidhaa huwa zinakwenda katika sehemu yenye soko.