Uchaguzi 2020 CCM haifai, tatizo ni Upinzani hauna sifa za kutawala nchi. Inabidi tuvumilie tu

Tanzania ya 1961 ilikuwa ile yenye injinia 2, madaktari 2, n.k. Tanzania ya leo 2020 yenye graduate 500000 kwa mwaka unatuletea chama cha viongozi wa form 6!!!!!!!!!!!!!!!!! Rubbish!
Hivi uongozi ni madegree?
 
hata makuwadi wa wakoloni nao walikuwa wakimkatisha tamaa hivi hivi Mwalimu (RIP mzee wetu) - kwamba eti Watnganyika wasingekuwa na uwezo wa kujitawala.

wacha Tundu Lissu aendelee kupiga spana. sasa hivi serekali inafanya kazi kwa maagizo ya Tundu Lissu na bado hajakabidhiwa nchi, akipewa je?
 
Hivi uongozi ni madegree?
Tafuta visingizio vyote lakini leo hii hatuhitaji form 6 kuunda na kuongoza chama kinachotaka kutshika dola.
Btw. tunachotaka siyo kitu kinachoitwa 'uongozi.' Lengo siyo kuona mtu anayetoka jasho jukwani halafu tuseme huyo ndo kiongozi. For what? Kuna kitu ndani ya kiongozi tunachokitafuta; teknology knowledge, science knowledge, economic understanding, health knowledge and guidance, etc.
 
Upinzani Tz huko vzr , tatizo ni tume huru tu mtoa mada ni popoma
 
Wewe ni genious sana uitoe CCM nani mbadala ? Huo ndio mtihani kwa sisi watanzania
 
Mfahamishe huyo hajielewi
 
Ndio maana Mwl. Nyerere alisema, "I cannot let my country go to the dogs"!
 
UPUUZI MTUPU! Hiyo tathmini kwamba upinzani hauna sifa ya kutawala Nchi uliufanya lini na wapi? Na ulitumia vigezo gani kufikia hitimisho lako? Tuondolee UPUMBAVU wako hapa!

Jee kwa maoni yako upinzani umejitayarisha kuchukua nchi? Tafadhari tuhabarishe ili tueneze injili.
 
Ukitaka kujua Upinzani ni hovyo hata CCM ikiwa dhaifu bado wanashindwa kuitoa. November utaona watakavyopotea. Inasikitisha.
 
Upinzani ni cowards kama mnauchungu kweli tokeni nendeni mkadai haki zenu mkiendelee hivi mtakufa mnalalamika tu.
 
Reactions: nao
Hufai wewe...katika vyama bora Africa CCM ni namba one, wakifuatiwa na ANC
Usitoe sifa sana maana ANC inaongoza kwa rushwa na kuiangusha SA kiuchumi kiasi hata familia moja ya wahindi kushikilia uchumi wa nchi. CCM hali ikoje? Unawakumbuka akina Rostam Aziz hadi kuitwa waweka hazina wa CCM? Wakaingiza wabunge kwa pesa yao na kuwapa uwaziri watu wadhaifu kabisa kama akina Ngereja? Kwa ujumla vyama hivi vikongwe, vimekuwa ni vichaka vya rushwa na vikwazo vya maendeleo.
 
Ukitaka kujua Upinzani ni hovyo hata CCM ikiwa dhaifu bado wanashindwa kuitoa. November utaona watakavyopotea. Inasikitisha.
Nakuunga mkono! Hawa ni wapinzani hovyo!! CDM ilipopata wabunge wengi ikaamini itaendelea kupaa na haikuhitaji vyama vingine kwenye serikali kivuli. Mbowe akaanza kupozi kama naye ni rais. Wameanguka sasa haonekani hata majukwaani.

Hawa ngoja waondoke bungeni ndo akili iwajae, waanze kuona umuhimu wa kuwa pamoja. Badala ya kukusanya nguvu, wao wanaamini umati unaoshangilia mtu mitaani ni kura.
 
Jee kwa maoni yako upinzani umejitayarisha kuchukua nchi? Tafadhari tuhabarishe ili tueneze injili.
Hata M/kiti haijulikani yuko wapi! Juzi tu wakichagua viongozi Mlimani City, walijidai kuimarisha chama 'kisayansi.' Sijui ilikuwa sayansi gani hiyo kwa wasiomaliza shule. Leo hii Mgombea anatwanga mitaani peke yake kwa magari. CCM wameiona hiyo, wnakanyaga kwa umoja; M/kiti, waziri mkuu na makamu wa rais. wao ni mmoja kona zote amalize kilometa za mraba zaidi ya laki 9! Wazembe tu!
 
Vumilia wewe na familia yako , utawala na tabia za kihutu zimetochosha .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…