Heci
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 3,591
- 6,114
Sisi wana Mbeya ni wahanga wa matukio ya kibabe ya kidhalimu yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na chama hiki mumiani. Miongoni mwa udhalimu huo ni kuporwa kwa uwanja wa wananchi, uwanja wa Sokoine kisha CCM kujimilikisha.
Uwanja wa Sokoine ulijengwa na wananchi wa Mbeya Mjini, kisha ukapewa jina la uwanja wa Mapinduzi, kabla ya mwaka 1984 haujabadilishwa jina na kuitwa uwanja wa Sokoine, baada ya kifo cha waziri mkuu ndugu Edward Moringe Sokoine.
Wananchi walihamasika kujenga uwanja huu kwa nguvu zao wenyewe baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kukataa msaada wa kujengewa uwanja wa kisasa na serikali ya China kwa sharti uitwe kwa jina la kiongozi wao, Mao Tse Dong.
Wananchi ndio walichanga fedha zao, walifyatua matofali, na walijitoa kikamilifu kwa moyo mmoja hadi kukamilika kwa uwanja. Mwaka 1992 Augustino Lyatonga Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani alitembelea mkoa wa Mbeya na kuhutubia kwenye uwanja wa Sokoine.
Kipindi hicho ndio vyama vya upinzani vimeruhusiwa kufanya siasa. Akaikuta bendera ya NCCR MAGEUZI inapepea uwanjani hapo, sanjari na bendera bendera ya Taifa huku bendera ya CCM ikiwa haipo kabisa uwanjani hapo.
Mrema kwa hasira akasema hawezi kuhutubia bendera ya chama pinzani ikiwa inapepea. Akaamuru bendera hiyo ishushwe na kuanzia hapo uwanja ni mali ya CCM.
NCCR MAGEUZI ni chama kilichokubalika sana enzi hizo mkoani Mbeya, kiliweza kuibwaga CCM kwenye uchaguzi wa diwani jimbo la Mbeya Mjini chini ya mgombea wake Mwalimu Polisya Sikumbula Mwaisyeje.
Sasa ni wakati sahihi kwa CCM kurejesha kwa wananchi uwanja huo, kwani haujawahi kuwa mali yao na wala CCM haikuwahi kuutolea jasho kwa namna yoyote.
Uwanja wa Sokoine sio mali ya CCM, Mbeya sio mali ya CCM. kataa CCM, kataa dhuluma.