CCM haikujenga uwanja wa Sokoine Mbeya, iliwapora wananchi. Uwanja urudishwe kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya

CCM haikujenga uwanja wa Sokoine Mbeya, iliwapora wananchi. Uwanja urudishwe kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya

Issue ya viwanja ngumu Sana. Sikujenga uwanja WA majimaji lkn Baba yangu wakati huo walishiriki KAZI ya ujenzi wa uwanja huu kwa majitoleo. Cha kushangaza Timu imeachwa ipamambane lkn uwanja wakachukua.
Kimsingi aliyeleta madhara yote haya ni Yule yule aliyeshauri Mali zote zilizomilikiwa na chama wkt wa mfumo WA chama kimoja ziende Serikalini tar 1.7.1992 vilipoanza vyama vingi vyama vyote vianze upya. Ccm hawakukubali kukabidhi Mali zote hizo vikiwemo viwanja na majengo. Ila naamini ni suala la Muda Tu. Atatokea Rais hukohuko Ccm mwaka wake atakabidhi kwa upendo Tu ili mambo yasiwe mengi

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Ikirudi halmashauri si ndiyo hao hao ccm [emoji1]

Ova
 
Uwanja wa biafra wenyewe wameuchukua lakini haukua wao

Ova
 
Sisi wana Mbeya ni wahanga wa matukio ya kibabe ya kidhalimu yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na chama hiki mumiani. Miongoni mwa udhalimu huo ni kuporwa kwa uwanja wa wananchi, uwanja wa Sokoine kisha CCM kujimilikisha.

Uwanja wa Sokoine ulijengwa na wananchi wa Mbeya Mjini, kisha ukapewa jina la uwanja wa Mapinduzi, kabla ya mwaka 1984 haujabadilishwa jina na kuitwa uwanja wa Sokoine, baada ya kifo cha waziri mkuu ndugu Edward Moringe Sokoine.

Wananchi walihamasika kujenga uwanja huu kwa nguvu zao wenyewe baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kukataa msaada wa kujengewa uwanja wa kisasa na serikali ya China kwa sharti uitwe kwa jina la kiongozi wao, Mao Tse Dong.

Wananchi ndio walichanga fedha zao, walifyatua matofali, na walijitoa kikamilifu kwa moyo mmoja hadi kukamilika kwa uwanja. Mwaka 1992 Augustino Lyatonga Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani alitembelea mkoa wa Mbeya na kuhutubia kwenye uwanja wa Sokoine.

Kipindi hicho ndio vyama vya upinzani vimeruhusiwa kufanya siasa. Akaikuta bendera ya NCCR MAGEUZI inapepea uwanjani hapo, sanjari na bendera bendera ya Taifa huku bendera ya CCM ikiwa haipo kabisa uwanjani hapo.

Mrema kwa hasira akasema hawezi kuhutubia bendera ya chama pinzani ikiwa inapepea. Akaamuru bendera hiyo ishushwe na kuanzia hapo uwanja ni mali ya CCM.

NCCR MAGEUZI ni chama kilichokubalika sana enzi hizo mkoani Mbeya, kiliweza kuibwaga CCM kwenye uchaguzi wa diwani jimbo la Mbeya Mjini chini ya mgombea wake Mwalimu Polisya Sikumbula Mwaisyeje.

Sasa ni wakati sahihi kwa CCM kurejesha kwa wananchi uwanja huo, kwani haujawahi kuwa mali yao na wala CCM haikuwahi kuutolea jasho kwa namna yoyote.

Uwanja wa Sokoine sio mali ya CCM, Mbeya sio mali ya CCM. kataa CCM, kataa dhuluma.
Hata majimaji songea tulishiriki kubeba matofali Yali fyatuliwa MTO matarawe,jeshi walitugawia maharage ya kopo na biskuti ngumu Sana kutafuna.
 
Uwanja wa Sokoine ulijengwa enzi za Chama kimoja, na michango ilipita kwa wana Mbeya wa wilaya zote. Na ukumbuke kuwa wakati huo, Mbeya ilikuwa haijagawanywa kama ilivyo sasa. CCM ndiyo ilisimamia serikali katika utekelezaji wa ule mradi, na chama kilishika hatamu kwelikweli.

Kwahiyo, hata kama CCM itakosa uhalali wa umiliki wa kiwanja cha Sokoine, bado hakiwezi kuwa mali ya Mbeya jiji,kwa sababu hakikujengwa na wana Mbeya jiji peke yao.
Kwahiyo uwanja uwe Mali ya nani?
 
Back
Top Bottom