CCM haikujenga uwanja wa Sokoine Mbeya, iliwapora wananchi. Uwanja urudishwe kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya

Njaa mbaya sana. Hivi na huko mmbea kuna shida ya chakula?
 
una shilingi ngapi hadi muda huu mleta uzi? ndio nyie mnakaa kwenye vijiwe vya retco, sokomatola , panapouzwa magezeti na washona viatu na kupiga stori za kijinga sana , wewe una hakika hati ya ardhi ya eneo hilo inasomaje ,
Thibitisha kama Heci ni mzee wa vijiweni
 
Hata ikirudi halmashauri huko si ccm

Ova
 
huyu ni mtu wa kijiweni huoni hoja za kitoto hizi anazatoa, kuanza kufikiri kiwanja kinamilikiwa na nani huku hajui hati ya umiliki inasomaje ni kipimo cha kuwa huna kazi maalumu mjini
Please attach the title deed
 
huyu ni mtu wa kijiweni huoni hoja za kitoto hizi anazatoa, kuanza kufikiri kiwanja kinamilikiwa na nani huku hajui hati ya umiliki inasomaje ni kipimo cha kuwa huna kazi maalumu mjini
Hebu wewe mwenyewe hati ya kiwanja, kwa heshima na taadhima twakuomba uiweke
 
Nyie chadema nyinyi mnajua kuchangisha watu hela hamjawahi miliki hata mita 100 ya kiwanja Cha ujenzi. Ukweli Ni kwamba uwanja huo tulijenga ss vijana wa TANU Enzi hizo za miaka ya 70's
 
Tanu ipi?
 
Sisi wana Mbeya ni wahanga wa matukio ya kibabe ya kidhalimu yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na chama hiki mumiani. Miongoni mwa udhalimu huo ni kuporwa kwa uwanja wa wananchi, uwanja wa Sokoine kisha CCM kujimilikisha.

Uwanja wa Sokoine ulijengwa na wananchi wa Mbeya Mjini, kisha ukapewa jina la uwanja wa Mapinduzi, kabla ya mwaka 1984 haujabadilishwa jina na kuitwa uwanja wa Sokoine, baada ya kifo cha waziri mkuu ndugu Edward Moringe Sokoine.

Wananchi walihamasika kujenga uwanja huu kwa nguvu zao wenyewe baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kukataa msaada wa kujengewa uwanja wa kisasa na serikali ya China kwa sharti uitwe kwa jina la kiongozi wao, Mao Tse Dong.

Wananchi ndio walichanga fedha zao, walifyatua matofali, na walijitoa kikamilifu kwa moyo mmoja hadi kukamilika kwa uwanja. Mwaka 1992 Augustino Lyatonga Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani alitembelea mkoa wa Mbeya na kuhutubia kwenye uwanja wa Sokoine.

Kipindi hicho ndio vyama vya upinzani vimeruhusiwa kufanya siasa. Akaikuta bendera ya NCCR MAGEUZI inapepea uwanjani hapo, sanjari na bendera bendera ya Taifa huku bendera ya CCM ikiwa haipo kabisa uwanjani hapo.

Mrema kwa hasira akasema hawezi kuhutubia bendera ya chama pinzani ikiwa inapepea. Akaamuru bendera hiyo ishushwe na kuanzia hapo uwanja ni mali ya CCM.

NCCR MAGEUZI ni chama kilichokubalika sana enzi hizo mkoani Mbeya, kiliweza kuibwaga CCM kwenye uchaguzi wa diwani jimbo la Mbeya Mjini chini ya mgombea wake Mwalimu Polisya Sikumbula Mwaisyeje.

Sasa ni wakati sahihi kwa CCM kurejesha kwa wananchi uwanja huo, kwani haujawahi kuwa mali yao na wala CCM haikuwahi kuutolea jasho kwa namna yoyote.

Uwanja wa Sokoine sio mali ya CCM, Mbeya sio mali ya CCM. kataa CCM, kataa dhuluma.
Likewise:
Jengo la makao makuu ya ccm mkoa wa Kilimanjaro, lilijengwa na wananchi kwa njia ya makato waliyokatwa kwenye mauzo ya kahawa. Hiyo ilikuwa miaka ya 80, kabla ya mfumo wa vyama vingi. Baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza, ccm walijimilikisha jengo hilo ambalo kiuhalisia ni mali ya umma. Ni mali ya umma kwa sababu wale wananchi waliolijenga baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi kila mmoja alienda kwenye chama alichokitaka, hivyo mali ile ingebaki kuwa mali ya umma. Jengo like na uwanja aliotaja mleta mada ni mifano miwili tu, lakini kuna mali nyingi ccm wamejomilikisha kinyemela na Kuna siku zitarudi kuwa mali ya umma. Kumbuka hapo Kenya baada ya KANU kuondoka madarakani mambo kama haya yalitokea.
 
WWewe

Wewe mwandishi ulikua Chama gani Cha siasla wakati uwanja wa sokoine unajengwa?Hivi wakati jumuiya ya afrika mashariki inavunjika Mali zake zilirudishwa nchi ganii?
Following the dissolution of the former East African Community in 1977, the Member States negotiated a Mediation Agreement for the pision of Assets and Liabilities, which they signed in 1984.
 
Sisi wana Mbeya ni wahanga wa matukio ya kibabe ya kidhalimu yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na chama hiki mumiani. Miongoni mwa udhalimu huo ni kuporwa kwa uwanja wa wananchi, uwanja wa Sokoine kisha CCM kujimilikisha.

Uwanja wa Sokoine ulijengwa na wananchi wa Mbeya Mjini, kisha ukapewa jina la uwanja wa Mapinduzi, kabla ya mwaka 1984 haujabadilishwa jina na kuitwa uwanja wa Sokoine, baada ya kifo cha waziri mkuu ndugu Edward Moringe Sokoine.

Wananchi walihamasika kujenga uwanja huu kwa nguvu zao wenyewe baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kukataa msaada wa kujengewa uwanja wa kisasa na serikali ya China kwa sharti uitwe kwa jina la kiongozi wao, Mao Tse Dong.

Wananchi ndio walichanga fedha zao, walifyatua matofali, na walijitoa kikamilifu kwa moyo mmoja hadi kukamilika kwa uwanja. Mwaka 1992 Augustino Lyatonga Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani alitembelea mkoa wa Mbeya na kuhutubia kwenye uwanja wa Sokoine.

Kipindi hicho ndio vyama vya upinzani vimeruhusiwa kufanya siasa. Akaikuta bendera ya NCCR MAGEUZI inapepea uwanjani hapo, sanjari na bendera bendera ya Taifa huku bendera ya CCM ikiwa haipo kabisa uwanjani hapo.

Mrema kwa hasira akasema hawezi kuhutubia bendera ya chama pinzani ikiwa inapepea. Akaamuru bendera hiyo ishushwe na kuanzia hapo uwanja ni mali ya CCM.

NCCR MAGEUZI ni chama kilichokubalika sana enzi hizo mkoani Mbeya, kiliweza kuibwaga CCM kwenye uchaguzi wa diwani jimbo la Mbeya Mjini chini ya mgombea wake Mwalimu Polisya Sikumbula Mwaisyeje.

Sasa ni wakati sahihi kwa CCM kurejesha kwa wananchi uwanja huo, kwani haujawahi kuwa mali yao na wala CCM haikuwahi kuutolea jasho kwa namna yoyote.

Uwanja wa Sokoine sio mali ya CCM, Mbeya sio mali ya CCM. kataa CCM, kataa dhuluma.
Wananchi bado wako, tena wako wengi kwani idadi yao imeongezeka; kama nchi bado tuhahitaji viwanja tena vingi, onyesheni uwezo wenukwa kuhamsisha watu wasombe mawe mjenge viwsnje kwanimaeneo yako mengi- ila kwa vile akili yenu imeishia kwenye maandamano mtabaki kusema viwanja n vyenu.
CCM ina hati miliki ya viwanja hivyo- kuwanyang'anya ina wezeaka but wit a price- FIDIA
 
Back
Top Bottom