Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Huu ndio ukweli wa wazi kabisa, kwamba kauli za polepole kwamba waliotoa rushwa watafundishwa adabu zichukuliwe kama porojo za kunogesha mazungumzo yake tu, hazina ukweli wowote na hata kwa cheo alichonacho hana mamlaka ya kumuengua mtu yeyote kwa tuhuma zozote (soma majukumu wa katibu mwenezi wa CCM)
Kingine ni kwamba Polepole si mtu wa kuaminika na wala hajawahi kuaminika, kwa mfano akiwa mjumbe wa Tume ya Katiba mpya chini ya Mzee Warioba alitamka hadharani na kupigia kampeni kuondolewa kwa cheo cha Wakuu Wa Wilaya, kwa hoja kwamba wakurugenzi wanatosha kusimamia majukumu Wilayani, akaungwa mkono karibu na kila mwenye akili nchi nzima, lakini cha kushangaza alikubali kuteuliwa na kuapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwenye awamu ya 5!
Pia kwenye tume hiyo hiyo alisema na kurekodiwa kwamba Tume huru ni lazima na akaiponda ccm na kuiambia wazi kwamba ikiwa uchaguzi ukiwa huru na haki basi ijiandae kukabidhi Ikulu , lakini yeye kwa sasa ni miongoni mwa watu wachache sana ndani ya ccm wanaopinga kabisa Katiba Mpya ( nitaambatanisha ushahidi wa video )
Ili kukuhakikishia kwamba Polepole si lolote ndani ya CCM ni kurudi kwa Lowassa ndani ya CCM, Kwa kumbukumbu ya wanajf na wengine wageni , Kwenye awamu ya 5 Polepole ndio kiongozi wa CCM aliyemtukana zaidi Lowassa labda kuliko wengine wote , kwa kutuaminisha kwamba huyu mtu ni fisadi wa kutisha , lakini siku ya kurudi Lowassa aliufyata na hajatukana tena hadi leo , huyu angekuwa na msimamo basi angeondoka ccm siku ileile.
Kwa ufupi ni kwamba Polepole wala CCM hakuna mwenye uwezo wa kupinga rushwa , taarifa zinadokeza kwamba hata Takukuru kuwarejesha waliodaiwa kutoa rushwa CCM ni matakwa ya ccm yenyewe baada ya kutathmini hali ya mambo , uliona wapi watuhumiwa wakapelekwa kwa aliyewatuhumu ili awachukulie hatua badala ya Mahakamani ? ni vigumu mno kwa CCM kuwaengua wagombea kwa tuhuma za rushwa , ikifanya hivyo basi itaengua wote na Wapinzani watapita bila kupingwa , kwa mfano kwenye jimbo la kyela wagombea karibu wote walitoa rushwa , kuanzia pikipiki , cash iliyofikia hadi laki 3 kwa mtu mmoja na pombe , hivi kwenye jimbo kama hili unamuengua nani na unamuacha nani ?
Itaendelea......