Uchaguzi 2020 CCM haina uwezo wa kumuondoa mgombea yeyote kwa sababu ya kutoa rushwa, labda iwe kwa sababu nyingine

Huu ndio ukweli wa wazi kabisa, kwamba kauli za polepole kwamba waliotoa rushwa watafundishwa adabu zichukuliwe kama porojo za kunogesha mazungumzo yake tu, hazina ukweli wowote na hata kwa cheo alichonacho hana mamlaka ya kumuengua mtu yeyote kwa tuhuma zozote (soma majukumu wa katibu mwenezi wa CCM)

Kingine ni kwamba Polepole si mtu wa kuaminika na wala hajawahi kuaminika, kwa mfano akiwa mjumbe wa Tume ya Katiba mpya chini ya Mzee Warioba alitamka hadharani na kupigia kampeni kuondolewa kwa cheo cha Wakuu Wa Wilaya, kwa hoja kwamba wakurugenzi wanatosha kusimamia majukumu Wilayani, akaungwa mkono karibu na kila mwenye akili nchi nzima, lakini cha kushangaza alikubali kuteuliwa na kuapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwenye awamu ya 5!

Pia kwenye tume hiyo hiyo alisema na kurekodiwa kwamba Tume huru ni lazima na akaiponda ccm na kuiambia wazi kwamba ikiwa uchaguzi ukiwa huru na haki basi ijiandae kukabidhi Ikulu , lakini yeye kwa sasa ni miongoni mwa watu wachache sana ndani ya ccm wanaopinga kabisa Katiba Mpya ( nitaambatanisha ushahidi wa video )

Ili kukuhakikishia kwamba Polepole si lolote ndani ya CCM ni kurudi kwa Lowassa ndani ya CCM, Kwa kumbukumbu ya wanajf na wengine wageni , Kwenye awamu ya 5 Polepole ndio kiongozi wa CCM aliyemtukana zaidi Lowassa labda kuliko wengine wote , kwa kutuaminisha kwamba huyu mtu ni fisadi wa kutisha , lakini siku ya kurudi Lowassa aliufyata na hajatukana tena hadi leo , huyu angekuwa na msimamo basi angeondoka ccm siku ileile.

Kwa ufupi ni kwamba Polepole wala CCM hakuna mwenye uwezo wa kupinga rushwa , taarifa zinadokeza kwamba hata Takukuru kuwarejesha waliodaiwa kutoa rushwa CCM ni matakwa ya ccm yenyewe baada ya kutathmini hali ya mambo , uliona wapi watuhumiwa wakapelekwa kwa aliyewatuhumu ili awachukulie hatua badala ya Mahakamani ? ni vigumu mno kwa CCM kuwaengua wagombea kwa tuhuma za rushwa , ikifanya hivyo basi itaengua wote na Wapinzani watapita bila kupingwa , kwa mfano kwenye jimbo la kyela wagombea karibu wote walitoa rushwa , kuanzia pikipiki , cash iliyofikia hadi laki 3 kwa mtu mmoja na pombe , hivi kwenye jimbo kama hili unamuengua nani na unamuacha nani ?

Itaendelea......
Hawa watu wameoza kwa rushwa!

Ccm hawastahili kuwepo uraiani, wote kuanzia mwenyekiti wao mpaka mfagiaji wa Lumumba!

Wamewaaminisha watanzania kuwa upinzani ni dhambi, ujinga wa watanzania ndo mtaji wao wa kisiasa
 
Nakumbuka mlianza nguvu ya soda nguvu ya soda mara nilikuwa nasikia mfumo mfumo leo hii sisikii chochote, nadhani muda utaongea kama ulivyoongea kwa yaliyopita. Tuliposema CCM na Tanzania mpya utaelewa tu subiri acha ku..
Jiandaeni kwa maumivu makali ambayo hamjawai kuyapata maana baada ya JPM kushinda tunamwongezea miaka 10 zaidi sisi tunajua mtanyooka na kuwa na hishima.

Unahisi chadema ndo watakaonyooka? huoni mmeanza nyie kunyooka hadi unafikiria kufanya upuuzi ambao haumithiliki? vipi akimaliza miaka yote hiyo unayofikiria kumpa then akaja kiongozi wa hovyo zaidi? mtabadilisha tena iwe miaka miwili? GrowYourBrainUpDude!
 
Huu ndio ukweli wa wazi kabisa, kwamba kauli za polepole kwamba waliotoa rushwa watafundishwa adabu zichukuliwe kama porojo za kunogesha mazungumzo yake tu, hazina ukweli wowote na hata kwa cheo alichonacho hana mamlaka ya kumuengua mtu yeyote kwa tuhuma zozote (soma majukumu wa katibu mwenezi wa CCM)

Kingine ni kwamba Polepole si mtu wa kuaminika na wala hajawahi kuaminika, kwa mfano akiwa mjumbe wa Tume ya Katiba mpya chini ya Mzee Warioba alitamka hadharani na kupigia kampeni kuondolewa kwa cheo cha Wakuu Wa Wilaya, kwa hoja kwamba wakurugenzi wanatosha kusimamia majukumu Wilayani, akaungwa mkono karibu na kila mwenye akili nchi nzima, lakini cha kushangaza alikubali kuteuliwa na kuapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwenye awamu ya 5!

Pia kwenye tume hiyo hiyo alisema na kurekodiwa kwamba Tume huru ni lazima na akaiponda ccm na kuiambia wazi kwamba ikiwa uchaguzi ukiwa huru na haki basi ijiandae kukabidhi Ikulu , lakini yeye kwa sasa ni miongoni mwa watu wachache sana ndani ya ccm wanaopinga kabisa Katiba Mpya ( nitaambatanisha ushahidi wa video )

Ili kukuhakikishia kwamba Polepole si lolote ndani ya CCM ni kurudi kwa Lowassa ndani ya CCM, Kwa kumbukumbu ya wanajf na wengine wageni , Kwenye awamu ya 5 Polepole ndio kiongozi wa CCM aliyemtukana zaidi Lowassa labda kuliko wengine wote , kwa kutuaminisha kwamba huyu mtu ni fisadi wa kutisha , lakini siku ya kurudi Lowassa aliufyata na hajatukana tena hadi leo , huyu angekuwa na msimamo basi angeondoka ccm siku ileile.

Kwa ufupi ni kwamba Polepole wala CCM hakuna mwenye uwezo wa kupinga rushwa , taarifa zinadokeza kwamba hata Takukuru kuwarejesha waliodaiwa kutoa rushwa CCM ni matakwa ya ccm yenyewe baada ya kutathmini hali ya mambo , uliona wapi watuhumiwa wakapelekwa kwa aliyewatuhumu ili awachukulie hatua badala ya Mahakamani ? ni vigumu mno kwa CCM kuwaengua wagombea kwa tuhuma za rushwa , ikifanya hivyo basi itaengua wote na Wapinzani watapita bila kupingwa , kwa mfano kwenye jimbo la kyela wagombea karibu wote walitoa rushwa , kuanzia pikipiki , cash iliyofikia hadi laki 3 kwa mtu mmoja na pombe , hivi kwenye jimbo kama hili unamuengua nani na unamuacha nani ?

Itaendelea......
Yametimia
Talimba
Taletale
Shigongo
Zungu
Mwakasaka
👆Walitoa rushwa

Badala yake ameunguliwa kapuya kawekwa mkwewe mkulu, au kimei kapata upendeleo, silinde na gekul
 
Mgombea wa ccm kyela aliongoza kwa kutoa rushwa nzito zikiwemo pikipiki kwa makatibu kata wote
 
Back
Top Bottom