Uchaguzi 2020 CCM hatuupendi ukweli, tusione ajabu mgombea wetu akashindwa vibaya uchaguzi huu

Uchaguzi 2020 CCM hatuupendi ukweli, tusione ajabu mgombea wetu akashindwa vibaya uchaguzi huu

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Mara nyingi nimekua nikisema kuwa sisi wana CCM tumekua waoga sana wa kuusema ukweli, ipo siku tutakua kwa aibu maana tukiendelea kutegemea Polisi kama alivyowahi kutuambia Rais mstaafu awamu ya 4 Dr JK. Hivi vyombo kuna wakati vitaamua kusimamia sheria ya nchi bila kuonea mtu, siku wakichoka ndio tutabaki wenyewe.

Tunahangaika na kubisha pamoja na kutukana tu badala ya kuhangaika na sera zetu. Hatumwambii ukweli Mwenyekiti wetu wa chama taifa kua maisha ni magumu kila nyanja, biashara haziendi vizuri, watoto wa maskini wengi wanakosa mikopo, ajira ni tatizo kubwa.

Badala yake tumebaki tunfisia tu na kujipendekeza, tofauti na hapo tunawatukana wapinzani badala ya kueleza ni vipi tutazikabili changamoto ambazo bado ni tatizo.

Tusishangae kuona hawa wapinzani wakitupiana chini na wakakata kuonewa, hivi vyombo vikichoka watasema wacha tusimame na sheria za nchi, tutaficha wapi aibu zetu?

Raia wa nchi ya Malawi walifanyiwa vibaya na watawala wao na matokeo yake tulichokiona ndio hicho, siku yakitugeuka tusilalamike.

Haya makubwa aliyofanya Rais wetu tufikishe ujumbe kwa jamii kwa kuwaambia nini kimefanyika. Siyo kila siku Lisu Lisu! Lisuuu!

Twendeni tujibu hoja zenye mashiko za upinzani.
 
Tatizo ni kuamini katika utawala wa milele. Hata kama yanafanyika mazuri sana, kutawala milele haiwezekani. Akili kubwa ingetengeneza mamluki na kumpa uraisi kwa chama kingine angalau kwa miaka hata 5 halafu unarudi unatawala 20 yrs then unacheza tena huo mchezo n.k.
 
Umemsikia mgombea yeyote wa ccm akikimbia hoja??? kwanza ccm bado wako kwenye mchujo wewe umeyatoa wapi hayo, umbeyaumbeya tuuuuu
jenga hoja acha mashushu mkuu....kisiwe kijiwe cha wahuni hiki..tunapoteza uweredi wa mada husika na kuanza mambo ya mashamsham hapa...tuwaachie akina dida na babu idd mambo hayoo
 
Hayo madaraja yanafaida gani, iwapo maisha yamekua magumu mtaani?
kwahiyo unanitukana mie ambaye mkewangu ni mjamzito na natakiwa kumwaisha hospitali..maanake hayana umuhimu aua hayafai sio???sio jibu zuri kwa hapo
 
Tatizo ni kuamini katika utawala wa milele. Hata kama yanafanyika mazuri sana, kutawala milele haiwezekani. Akili kubwa ingetengeneza mamluki na kumpa uraisi kwa chama kingine angalau kwa miaka hata 5 halafu unarudi unatawala 20 yrs then unacheza tena huo mchezo n.k.
usisahau kulikuwa na ngome ya roma....ilifika sehemu ikafa tu..kumbuka nature alwys take place
 
kwahiyo unanitukana mie ambaye mkewangu ni mjamzito na natakiwa kumwaisha hospitali..maanake hayana umuhimu aua hayafai sio???sio jibu zuri kwa hapo
Nani kakutukana? Kila mtu na mtazamo wake bhana!
 
Nani kakutukana? Kila mtu na mtazamo wake bhana!
mtazamo lazima uwe na uweredi lakini kaka....kwahiyo kama ni mtazamo ndo useme maisha yako magumu kwakuwa road zinajengwa au???ndege za atcl sio lazima tupande mm na ww hapana..kuna watu wanafanya trip day to night wanazihtaji sana hizo kuliko kingne chchte kile..jenga hoja that's my point
 
Hivi kati ya Cdm? Na ccm nani ahangaike na sera zake uchaguzi huu??. Embu usiteletee unazi hapa na kujifanya wewe CCM!.Hivi wewe akili yako unaona Kuna uwezekano wa wapinzani kushinda uchaguzi huu? Walishindwa 2015 kwa CCM ile! ,walipoungana! Watawaiweza hii CCM ya Magufuli?.Kwanza huyo tundu kaongea nini mpaka sasa zaidi ya ku mu attack jpm!. Mnandanganyika na umati unaoenda kwa lissu kumdhamini ndo unafikili kwamba atashinda?.. Hivi Jpm naye angeamua kutembea na Gari kutafuta wadhamini mikoani unafikili ingekuaje?.. Au kwa vile unaona CCM wametulia tu?. Subiri kampeni zianze ndo utajua hujui!..
 
mtazamo lazima uwe na uweredi lakini kaka....kwahiyo kama ni mtazamo ndo useme maisha yako magumu kwakuwa road zinajengwa au???ndege za atcl sio lazima tupande mm na ww hapana..kuna watu wanafanya trip day to night wanazihtaji sana hizo kuliko kingne chchte kile..jenga hoja that's my point
Sasa kama toka 2015 sijaengezewa mshara wala kupandishwa cheo unataka niseme nini?
 
CCM washapagawa wao wanamfatilia lissu tu badala ya kutangaza sera zao.
 
Tatizo ninaloliona mimi ni kwamba generation mpya inahitaji vyama vipya haijui story za sijui Tanu ilileta uhuru,sijui Nyerere aliwafanya nini mabeberu etc.

Generation ya wazee ambao walikua wanamjua Nyerere/Mwinyi/Mkapa inaenda inapungua,kwa sasa watoto hawa wa 2000's hawaelewi chochote kile khs CCM.

Yaani kwa sasa hata CCM ifanye mazuri kiasi gani,hata ijenge nini,hata impe pesa kila mtu mfukoni muda wake wake wa kufa umeshafika kama ambavyo itafika kipindi vyama vingine vya upinzani navyo vitachokwa/kufa.

Nadhani zile stage za kuzaliwa,kukua mwishowe kufa zimeshapitiwa na CCM kwa hio kushindana na graph hio ni kupoteza muda tu.
 
Tatizo ni kuamini katika utawala wa milele. Hata kama yanafanyika mazuri sana, kutawala milele haiwezekani. Akili kubwa ingetengeneza mamluki na kumpa uraisi kwa chama kingine angalau kwa miaka hata 5 halafu unarudi unatawala 20 yrs then unacheza tena huo mchezo n.k.
Hili wazo lingewezekana mwaka 1995 wakati Mrema ni mgombea wa NCCR-Mageuzi. Nadhani kwa sasa intelijensia za upinzani zimesoge mbele kidogo, rahisi kuwajua mamluki. Lakini all in all ni wazo zuri sana kwa kweli
 
Tatizo ninaloliona mimi ni kwamba generation mpya inahitaji vyama vipya haijui story za sijui Tanu ilileta uhuru,sijui Nyerere aliwafanya nini mabeberu etc.

Generation ya wazee ambao walikua wanamjua Nyerere/Mwinyi/Mkapa inaenda inapungua,kwa sasa watoto hawa wa 2000's hawaelewi chochote kile khs CCM.

Yaani kwa sasa hata CCM ifanye mazuri kiasi gani,hata ijenge nini,hata impe pesa kila mtu mfukoni muda wake wake wa kufa umeshafika kama ambavyo itafika kipindi vyama vingine vya upinzani navyo vitachokwa/kufa.

Nadhani zile stage za kuzaliwa,kukua mwishowe kufa zimeshapitiwa na CCM kwa hio kushindana na graph hio ni kupoteza muda tu.
Umeongea ukweli mkuu.
 
Wasiojua watashia kukutukana na kukukejeli badala ya kuchangia hoja.
 
Back
Top Bottom