MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Mara nyingi nimekua nikisema kuwa sisi wana CCM tumekua waoga sana wa kuusema ukweli, ipo siku tutakua kwa aibu maana tukiendelea kutegemea Polisi kama alivyowahi kutuambia Rais mstaafu awamu ya 4 Dr JK. Hivi vyombo kuna wakati vitaamua kusimamia sheria ya nchi bila kuonea mtu, siku wakichoka ndio tutabaki wenyewe.
Tunahangaika na kubisha pamoja na kutukana tu badala ya kuhangaika na sera zetu. Hatumwambii ukweli Mwenyekiti wetu wa chama taifa kua maisha ni magumu kila nyanja, biashara haziendi vizuri, watoto wa maskini wengi wanakosa mikopo, ajira ni tatizo kubwa.
Badala yake tumebaki tunfisia tu na kujipendekeza, tofauti na hapo tunawatukana wapinzani badala ya kueleza ni vipi tutazikabili changamoto ambazo bado ni tatizo.
Tusishangae kuona hawa wapinzani wakitupiana chini na wakakata kuonewa, hivi vyombo vikichoka watasema wacha tusimame na sheria za nchi, tutaficha wapi aibu zetu?
Raia wa nchi ya Malawi walifanyiwa vibaya na watawala wao na matokeo yake tulichokiona ndio hicho, siku yakitugeuka tusilalamike.
Haya makubwa aliyofanya Rais wetu tufikishe ujumbe kwa jamii kwa kuwaambia nini kimefanyika. Siyo kila siku Lisu Lisu! Lisuuu!
Twendeni tujibu hoja zenye mashiko za upinzani.