CCM hawakurupuki kwenye mambo yao na mtu akizingua anafinywa ndani huwezi kuta wanaparuana nje. Hapa ndio CHADEMA mnafeli

CCM wanatumia polisi kuwatisha watu wao mumesahau ya NAPE bila polisi ccm 🚻
 
CCM ukiongelea hadharani unauawa. Ndugai alitoa maoni ya kweli kabisa unakumbuka alivyosulubiwa?
Alijisulubu yeye mwenyewe. Barua ya kujiuzulu alisema ameamua kwa hiari yake bila kushurutishwa na mtu. Na akaangua na Saini.
Alipotea kidogo tu barua aliipeleka kwa katibu wa chama badala ya katibu wa bunge. Na kupotea bungeni kwa muda mrefu watu wakadhani alikua amewekwa under house arrest, kumbe ni Soni tu ya kuachia ukubwa.
 
Kitu ambacho Chadema wanafanyia ndiyo demokrasia ya kweli. Mtu ana uwezo wa kumpinga mwenyekiti bila kuogopa. Siamini kama nyiye man uwezo wa kushindana na mwenyekiti. Wengi wanaogopa kuliwa kichwa. CCM Ina wenyewe mkuu wengine ni wasindikizaji. Kuna mengi ya CCM tunajua tunabaki kuangalia tu.
 
CCM wana serekali bila serekali CCM ni zaidi ya genge la machokoraa.
 
Fedha alizotoa Mustapha Sabodo hazikuwa rushwa.
Sabodo aliandika barua ya wazi kwa rais/mwwnyekiti wa ccm akilalamika upigaji unaofanywa serikalini, tofauti na malengo ya ccm kama ilivyokuwa wakati wa Nyerere.
Alisema anasikitika kuona yeye wafanyabiashara fulani wapigaji na wakwepa kodi wanavyohujumu nchi na serikali ya ccm kutochukua hatua.
Sabod hakujibiwa na mwenyekiti wake. Ndipo akasema hadharani atatoa mchango wake kwa Chadema ili zisaidie katika mikakati yao kwa vile kuibua kwao upigaji kunawafanya waonekane wazalendo kwa nchi kuliko walioko madarakani.
Hiyo utaiitaje rushwa?
 
CCM DAIMA SAMIA MITANO TENA
 
Ungesema mtu akizingua anaweza pewa kesi uraia. Au uhujumu uchumi. Sasa chadema nje ya kumfuta mtu uanachama watafanya nini maana wao sio watawala hawawez kumpa mtu kesi
 
Kabla ya kumuamini Lisu moja kwa moja someni kitabu kinachoitwa "The dangers of a single story" mwandishi ni Chimamanda Adichie.
 
Unamkumbuka JAK ZOKA? Mtu yeyote anayejua siasa za Nchi hii huwezi kuilaumumu chadema kwa kushindwa kuwadhibiti wapenzi wake.

1. Ccm inatumia dola kudhibiti wapinzani wa nje na ndani.(tiss)
2. Upinzani ukitumia mbinu hizohizo za ccm za kudhibiti upinzani wa ndani mfano (kuteka na kuuwa) itakuwa ni jinai ambayo kule kwa ccm hutawaona polisi na mahakana ila yakifayika hayo kwa upinzani haraka sana utawaona policcm na mahakana on the crime scene.
Shortly ccm ni mafia gang.
 
Nguvu kubwa ya vyama tawala kwa nchi masikini ni serikali na vyombo vya dola wakati upinzani hutegemea watu binafsi.
Vyama vingi vya upinzani hushindwa kujiendesha au kukua kwa sababu ya u masikini, hivyo kubaki kuwepo kwa majina tu.
 
Sisi CCM hata sumu huwa tunapeana kimya kimya kama alivyofanywa Mangula.
 
Kwani hao CHADEMA ni mawe hawawezi kujiongeza na kujifunza? Hata ukiweka dola pembeni, CCM wanajua jinsi ya kupangilia their 'shit'
 
Hata sijaelewa, ushetani wa kujua jinsi ya kujipanga na kumvuruga mpinzani wako?
 
Mkuu unatupiga hapa, kwamba nje unakuta upande mmoja unaparuana hivi bila stratergy utafikiri hawana vichwa?🤔
 
Hao mafisadi si ni chain Mkuu, mpaka mtu anatoka kuongea kuna mtu anakuwa kazingua, lkn huko mwanzo kote wanaenda kama timu... kama nilivyosema, wapo vizuri kwenye mipango iwe MIBAYA au mizuri, na ikitokea imeshindakana kudeal nae ndani wana🌚🌚..... unapojifunza kwa mwenzako hutakiwi kuwa zuzu na kubeba kila kitu hadi cha ovyo, inabidi uboreshe uwazidi na kete
 
Hili sina ufahamu nalo Mkuu, bila discipline sehemu yoyote lazima kitu kife, hawahitaji kuwa na amiri jeshi ili wawe disciplined
 
Hili sina ufahamu nalo Mkuu, bila discipline sehemu yoyote lazima kitu kife, hawahitaji kuwa na amiri jeshi ili wawe disciplined

..Mwenyekiti wa Ccm anakata wagombea walioshinda kura ya maoni kwasababu anajua ana vyombo vya dola nyuma yake. Na waliokatwa hawafurukuti sio kwasababu wana nidhamu bali kwasababu ya kuogopa mamlaka ya kijeshi aliyonayo Mwenyekiti wa Ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…