Friends and Enemies,
From Monopartisim to Multipartism 1992 to 1995,nchi yetu imepitia chaguz kadhaa ambazo tunaweza sema nchi bado ilikua changa kwenye Siasa za vyama vingi,na wakati mwingine tunaweza sema kwamba tumepitia siasa ya aina yetu na ya kipekee kama Taifa ambayo hatuwez jifananisha na nchi yoyote ya kiafrika kwa ujumla,
Mfano mzur wa nchi ya kidemokrasia kwa Afrika ni Ghana,wengine tuna safar ndefu kidogo ila ni muhim kuzid kujenga vyama imara vya upinzan ambavyo vitakuwa tayar kuongoza nchi bila ya kuwa na chembe chembe za ubaraka kutoka nchi za magharibi,
Tuwe wakweli,kuongoza Taifa siyo jambo la kufanya Rehearsal ndug zangu,wapinzan tulionao bado wanatia shaka Sana kuwaamin na kuwapa Dola waongoze,labda kama watashirikishwa kwenye serikali ya mseto lakin kiukweli hawana misimamo yenye kueleweka kias Cha kufikia sisi kuwaamin na kuwapa ridhaa ya kuongoza Dola,
Wakati mwingine tuna piga Kura kuwapa upinzan siyo kwamba tuna amin Wana uwezo huo,Bali ni kukosa matumain na baadhi ya mienendo ya CCM,sasa CCM ikijirekebisha na kuwatumikia watanzania kwa haki na usawa,upinzan huu tulionao hautaweza fananishwa hata kidogo na uongoz wa ccm,
Wapinzani tunawahitaji kwa mustakabali wa Taifa letu lakini wana Kazi ya kufanya kwa miongo kadhaa kupata ukomavu huo wa kuongoza Dola.