Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Tuna chama tawala kinachojitambua. Kipindi cha Kikwete porojo ilikuwa ni umeme wa gas kwani umeme wa maji tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. na hadithi ikawa gas ni muarobaini wa tatizo la nishati nchini. Kaingia Magufuli anasema umeme wa maji ni wa gharama nafuu, ccm wote wanashangilia lakini wamesahau chini ya miaka mitano walisema umeme wa maji tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi!Umeongea ukweli mtupu mkuu,kifupi hatuna vyama upinzani nchi hii kuna madalali wa kisiasa, mbaya zaidi hawajifunzi kbs wanaona wako sahihi tu
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Juzi wakati Magufuli yuko hai anasema hakuna corona kisha anaficha data, chama chake kinamsifia kwa kupambana na Corona, akaagiza mambo ya nyungu mpaka kibanda cha ushirikina kujengwe hospitali kubwa kabisa ya nchi. Viongozi wanaojifanya wasomi wakawa brainwashed akina Kabudi wanakunywa dawa za mitishamba hadharani, akina Jafo wanajifukiza na kujivunia tiba zetu. Chini ya siku 100 baada ya kifo cha Magufuli hakuna anayetaka nyungu, mwendo ni barakoa, kibanda cha ushirikina kikaondolewa hospital ya muhimbili kwa aibu. Hicho ndio chama tawala kinachoonekana kiko sawa! Acha wazungu waendelee kutuita manyani.