Uchaguzi 2020 CCM ikishindwa uchaguzi hata Polepole atahamia CHADEMA

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Polepole bado Ni kijana, na hakuna kijana anaipenda CCM Ila kwa maslahi ya kuwa chama tawala. Hivyo Kama siku CCM (Mungu apishie mbali) ikianguka kwenye uchaguzi CCM itakimbiwa na wengi hata usiowatarajia. Wakwanza kuhamia Chadema anaweza kuwa mh. Polepole.

Kila anayesema CCM Oyeee mtizame usoni utaona kitu kilichojificha machoni na usoni mwake. Hapa haijalishi Ni Rais mstaafu, makamu, Waziri Mkuu au mwananchi wa kawaida.

Kwahiyo Ni vema hata viongozi wa chama na serikali waliopo wakaweka akiba ya maneno na vitendo.

Kazi ya Baba wa taifa kuwakosoa viongozi ameiacha kwa vyama vya upinzani, hasa Chadema. Mfano, Kama Baba wa taifa angekuwa hai bado uwanja wa ndege wa chato huenda usingejengwa.
 
Ka polepole ni kanafiki kale, sidhani kama watakapokea... Labda kapewe kazi ya kufagia Ikulu..
 
Mungu amekuwa amiwaonyesha njia ya haki,Ila wamekuwa wakijaribu kuikataa kwa nguvu,zao ila wamesahau Hilo wataliweza kwa kipindi,tu kwani mwisho wao uukaribu Sana.
 
Huyu hapa
Your browser is not able to display this video.
 
Ila ndio hivyo ccm haiwezi kushindwa, sio uchaguzi huu tu, hata baada ya miaka 50
 
I LOATHE SLUG SLIME TRACKS, AND THAT GUY KEEPS REMINDING ME OF JUST THAT!
🤮🤮🤮🤮🤮💥
 
Polepole ana kadi ya Chadema. Tunamjua toka akiwa Aza Boy
 
Nakubaliana wewe. Polepole amejidhihirisha kuwa mchumia tumbo. Hata Rungwe akiukwaa, Polepole ataomba uenezi huko.
 
Ka polepole ni kanafiki kale, sidhani kama watakapokea... Labda kapewe kazi ya kufagia Ikulu..
Kale ni kakufungia kwenye kizimba na kulishwa pumba na maji ya kunywa kidoogo kawe kama kivutio cha utalii
 
Truth be told, mpaka siku NEC ikifanyiwa major overhaul au Jeshi liamue kufanya yake, CCM haitong’oka pale madarakani.

You can take this to the Bank...
 
Ila ndio hivyo ccm haiwezi kushindwa, sio uchaguzi huu tu, hata baada ya miaka 50
Kwani akina Gaddafi omary Ali bashiri nao walikuwa wanaona watakaa mpaka vitukuu vyao Leo hii wako wapi nchi sio ya ccm ni ya watanzania wote
 
Hii ni moja ya miracles.

Ila 2020 nitakuja chama cha biashara CHADEMA, Nasimama kama mgombea wenu wa urais..Nikiloose tu huyo nageuka zangu CCM.😂
 
Hayati baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere angekuwa yupo hai angeshajiunga na Chadema muda mrefu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni binadamu tu kama mm. Hata kesho yako huijui utajua ya miaka 50 ijayo? Makabwela bwn kwa kujimwambafai??!! Hahahahahah........
Mkuu CCM imefanikiwa kuongoza na kuwatawala watanzania kwa kuwa 70% ya watanzania ni wajinga Mtaji wa watawala ni elimu mbovu inayozuia mtu kujitambua, kutambua umuhimu wa siasa, uhuru na haki kuwa ndio tunu za taifa lenye maendeleo watanzana huona siasa ni kama ushabiki Simba na Yanga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Truth be told, mpaka siku NEC ikifanyiwa major overhaul au Jeshi liamue kufanya yake, CCM haitong’oka pale madarakani.

You can take this to the Bank...
Yaani wananchi mkae tuuuuu muwe mnaridhika na state of affairs halafu mtegemee jeshi au NEC liwafanyie mabadiliko hiyo haitatokea kamweeeeeee labda kama nchi yetu ingekuwa nchi ya kijeshi.

Nchi zote zenye mkwamo kama yetu mabadiliko lazima yaanzie kwa wananchi kuandamana pasi na kikomo kuikataa serikali iliyopo madarakani , rais akitia ngumu ndipo sasa jeshi uingilia kati., upo hapo ?

Yaani wewe uendeleze uoga wako halafu unategemea jeshi likufanyie kazi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…