Uchaguzi 2020 CCM imechokwa na Watanzania tuache utani kabisa

Kwani kuna mtu asiyejua kuwa mnawanunua kwa pesa za walipa kodi!
 
Safari hii pesa zote za Nchi mtamkabidhi Kamanda Siro la sivyo mtakuwa ktk vitabu vya historia.
 
Twakimu zipi twaweza au nimejaribu kupitia comment zilizopo ziko kama 66 lakini 2 tu ndo zakuunga mkono juhudi za Magufuri zingine zote zimechoka
 
Twakimu zipi twaweza au nimejaribu kupitia comment zilizopo ziko kama 66 lakini 2 tu ndo zakuunga mkono juhudi za Magufuri zingine zote zimechoka
Hiyo ndiyo hali halisi Mkuu, na ndiyo maana hii CCM imatumia nguvu kubwa sana ili isianguke. Lakini bahati mbaya is too late. CAG Anatoa ripoti ya Upotevu wa 1.5 Trilion CCM wanapita ktk Majukwaa kuipingaa, sasa ukiangalia wanaoipinga hata kusoma na kuandika vizuri hawajui. Haya ni maajabu ya karne, Ati Wanawatuma Akina Musiba na wajinga wa dizain hizo kuja kukanusha kwa maneno maneno tu. Nasema CCM Ilishakata Roho, Ni ya kufukia tu
 
Ni kweli CCM imeongoza mda mrefu na imechoka, lakini ni chama gani mbadala kinaweza kuongoza nchi?? Dr slaa ambaye alipendwa chadema alitoka CCM, Lowasa wa mabadiliko alitoka CCM, akina sumaye, nyalandu, nk.... CCM ni dubwana kubwa!! Unaweza kukuta mashinji na zitto wote ni CCM

Pili, vyama vya upinzani havijajijenga kitaasisi, ukiangalia cuf ni kama chama cha waisilamu wa pwani, CHADEMA ni wachaga wa kaskazini toka miaka ya 90s mwenyekiti ni yule yule mchaga... viongozi waandamizi akina sumaye, lema, selasini, nk. Ukija kwa vijana akina malisa, ben saanane nk wote wachaga wa kaskazini.... vyama vya upinzani vinaonekana kuwa vya watu binafsi kuliko taasisi

Tatu, sera za upinzani hazipo wazi, haijulikani wanapigania nini hasa, wao ni kudandia hoja kwa juu na kutukana. CCM Wanamtumia makonda kuwachezesha muziki CDM. Makonda haishi vituko, chadema nao wanakazana kucheza nae, wanapoteza mda wa vitu vya msingi vya kupigania....

Nne, muundo wa upinzani upo hasa mijini, hawajashuka hadi kwenye ngazi ya shina kama ilivyo CCM. leo hii chadema kukuta wana ofisi kwenye kata tu ni mtihani.... wao wanasubir uchaguz waandamane....

Mwisho. Upinzani na CCM ni watu walewale, wapo kwa ajili ya matumbo yao.... wao ni wanasiasa na siasa kwao ni kazi kama kazi zingine... mabadiliko ya kweli yataanzia kwa mwananchi mmoja mmoja kujitambua, kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu.

"Mimi nang'atuka lakini naendelea kuamini kwamba, bila CCM imara nchi yetu itayumba." Mwalimu jk Nyerere
 
Mwaka 2015 nilimpa kura jiwe, ila kwa mambo yanavyoenda Kuna wakati nawaza malaika washuke waje wamchukue jiwe wamrudishe mengi
 
Mungu akuepushe na vitu vyenye ncha kali , Amina
 
Kila Uchaguzi unapofika CCM wamezoea kuvunja Benki kuu na Kukwapua pesa kwa ajili ya kuhonga. Msifikiri tumesahau sarakasi mlizofanya za kujifanya Gavana wetu Balali ati amefarik wakati Jamaa anadunda Mitaani mpaka Leo, tukiwaambia CCM ni Wakala wa Shetani mnakataa. Ipo Siku Tu. Na wote mnaohusika na huu wizi wa pesa za wananchi ili mradi mbaki kuwa Madarakani na huku mkiwaacha Wananchi wakitaabika ktk Nchi Yao Mungu aliyoijalia Asali na Maziwa mtalipa tu,
 
Mungu akuepushe na vitu vyenye ncha kali , Amina
Mkuu tukiogopa kufa kwa kuitetea Nchi yetu Tutakuwa tunafanya Dhambi kubwa. Mbona CAG yeye Haogopi kufa?, hivi Unaijua Vita ya CAG na Huu Wizi wa CCM ilivyo kubwa?, na Swali langu, je Kati yetu kuna Atakayeishi Milele?. Kwa hiyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunaisimamia haki hapa Duniani. CCM wameshaikongoroa hii Nchi imebaki mifupa, Wananchi wanaojitambua wameshawachoka lakini wao wanalazimisha kuwatawala. Hivi Mwl Nyerere yeye hakuogopa kufa?, je Bila Nyerere tungepata huu Uhuru?. Tunataka Haki kwa kila mtu ktk Nchi hii, CCM haiwezi tena Hata tufanyaje, haiwezi.
 
Wananchi walitaka kuunda Katiba mpya ya jiinsi wanavyotaka Nchi Yao iendeshwe hawa CCM wakaivuruga hadi kufikia hatua ya kumpiga Waziri wetu Mkuu Warioba. CCM Hawataki kabisa Jambo lolote jema litokee ktk Nchi Hii, na Najua kabisa 80% ya CCM wenyewe hawapendezwi na jinsi mambo yanavyokwenda ktk Nchi hii, ila kuna kikundi kidogo sana ndani ya chama ambao ndio wanufaika wakuu wa Udhalimu huu wanaofanyiwa Watanzania wenzetu na hawa ndio wanaoitafuna hii Nchi. Hawatakaa watosheke. Ndiyo maana wako tayari hata kuwapiganisha Vita Watanzania ili mradi tu wao waendelee kufaidii. Hawajali chochote.
 
wewe ndiyo umeichoka ccm.sisi tunaipenda ccm muda wote,inatekeleza ahadi zake kwa vitendo.watu wajinga kama wewe wanaichukia ccm
 
Tumia akili wala basi braza..eleza mambo kama mtu unayejitambua..uiondoe ccm uweke chama kipi..sasa..maana huwezi kutuingiza mkenge halaf unatuacha hewani mzee, tutakunyonya macho yako...usizungumze vitu kwa ushabiki..hii forum sio saizi yako..nahisi bado unasoma shule wewe..,, you are a minor..my friend..
 
Hujielewi wewe, sasa fisadi ni nani? Tangu Nchi hii iumbwe hakujawahi kutokea upotevu mkubwa wa pesa kiasi hiki cha 1.5 Trilion, na nyie mnaotetea huu wizi inaonekana ndiyo wanufaika wakuu, mtuondokee salama mtuachie Tanzania yetu
Hahahaha huu wizi nani kausema..CAG alishasema hakuna wizi, sasa wewe ni nani kusema hivyo..fuatilieni mauwizi kwenye mavyama yenu ya mabilioni ya fedha..haya walau CAG ameyatamka kuwa ni ufisadi..msioneane aibu kamanda..ndio maisha yalivyo
 
Ningekuwa na nafasi Kama ya Siro, haki ya Mungu CCM wangenikoma. Yaani ingekuwa nipe nikupe, ningehakikish Mimi na jamaa wa jamaa zangu na mpaka vitukuu tunakuwa matajiri. Maana Siro akiamua hata kesho CCM ifutike inafutika.no way
Hawez yy mwenyewe anasubir uteuz
 

Utaratibu wa ccm ndio ambao Magufuli alipata kura 100% bila hata kura moja kumkataa au kuharibika.
 
Ni kweli CCM imechokwa lakini bado hakijatokea Chan's mbadala ndio maana CCM itaendelea kushinda. Chadema imejaa waizi na fisadi kama akina Mbowe na ukanda zaidi. Nafasi muhimu za chama wanapewa wachagaa tuu. CUF nayo ilijaa udini nafasi zote za juu zilishikwa na waislam na ndio maana ilikuwa chaguo la watu wa Zanzibar na pwani . ACT nayo inaeekea itaenda kurithi Yale yaliyokuwa ni ya CUF. ACT itajikita kwenye uislam zaidi hivyo kupoteza mvuto. Vyama vingine vya upinzani ni kama havipo. Chama mbadala kitapopatikana chenye kulenga makundi yote bila kuwa na maslahi ya ukanda, ukabila, udini na harufu za ufisadi ndio kutakuwa na uwezo wa kuiondoa CCM madarakani. Mimi nilisimamia uchaguzi kituo kimoja mwaka 2015 CCM ilishinda asubuhi mapema. Kwahiyo bado chama mbadala hakijapatikana
 
To begin with, ccm hawana idadi hiyo ya wanachama, otherwise, utupe ushahidi. Wanachama wao kama ni wengi hawazidi 4 million na 80% ya hao ni wanachama wafu.

Pili, watanzania kama tuko 59 million, ujue hiyo idadi ni pamoja na watoto wanaopakatwa na woote under 18 years ambao wanaweza wakafika hata 30 million.
 
Kwel kabisa magamba na mwenyekit wao yamebaki kupeana vyeo mfano igp, judge mkuu, mkuu was majeshi, pamoja na mawazir wengi wrote in ukanda na ukabila aisee ngoja sisi kanda ya ziwa tuinjoi.hahahaaaa Lumumba kwa buku7 kama nguruwe alie kwenye shamba la miwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…